Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,067
- 10,938
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa kutokea Mkoa wa Geita , Evaristi Gerevas amewataka vijana wa chama hicho kuacha tabia ya kuwa wasindikizaji na kubeba mikoba ya wagombea wa nafasi mbalimbali za Uongozi katika kuelekea Uchaguzi Mkuu na badala yake wachukue Fomu kugombea nafasi za Ubunge na Udiwani .
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Hayo ameyaeleza katika Ufunguzi wa Semina iliyowakutanisha Viongozi wa Umoja wa Vijana Mkoa wa Geita wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) iliyofanyika katika Ofisi ya Chama kata ya Magogo Mjini Geita huku akiwataka kugombea nafasi mbalimbali.
"Sisi kama Kamati ya Siasa ya Mkoa tutakuwa bega kwa bega na kijana yoyote atakaekuwa amechukua fomu kuomba nafasi yoyote ile tusiishie kuwa wasindikizaji , tusiishie kuwa wapambe tatizo letu vijana tunatamani nafasi za juu zaidi lakini uongozi unaanzia chini wewe pamoja na Digrii zako pamoja na umri wako usichague nafasi yoyote safari yoyote inaanzia chini kwenda juu." Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa, Evaristi Gerevas.
"Na naamini mkoa wa Geita tunao vijana wenye uwezo na wenye sifa ambao wanastaili kwenda kuomba nafasi wakati unapokuwa umefika lakini tusiishie tuu kwenye nafasi ya Udiwani twende tukachukue nafasi za Ubunge, Mbona mmesita nafasi ya Ubunge haina mwenyewe ni mtu yeyote mwenye sifa haiangalii umri ilimradi uwe una miaka 18 na kuendelea na uwe na sifa kamili" Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Geita, Manjale Magambo.