Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
EVERTON FOOTBALL CLUB MTAA WA NARUNG'OMBE, 1966
Mwaka wa 1966 wastani wa umri takriban sote tuliokuwa Everton ni miaka 15/16.
Kulikuwa na wenzetu mimi sina taarifa zao kabisa na kwa hakika huwa nawakumbuka:
Mashaka De Stefano, Maufi, Mazola, Jalala, Sultani, Twahir, Ali Kikoti, Hamisi Chai Ndogo, Malu...wako wengi wengine siwakumbuki.
Si rahisi kuamini kuwa lei imepita zaidi ya miaka 60.
Hii picha nimepiga Mnazi Mmoja mwaka wa 1966 na camera yangu nimeipa mgongo sasa Titi Street na nyuma ni Soko Mjinga Kisutu na pembeni mkabala na soko ni Msikiti wa Badawy sasa Rawdha.
Siku hii nakumbuka sikutaka kufanya mazoezi hapa niliposimama nawaangalia Everton wanafanya mazoezi:
Atika Kombo, Jumanne Masimenti (Guu la Ngamia), Juma Abeid (Spencer), Salim Khalil (Gordon Banks), Ahmada (Danny Blanchflour), Rashid Vava, Mohamed Awadh (Chico),Khalid Fadhil (George Young), Iddi Waziri Simba (Rumania), Rehani, Hamim, Abdallah Mkwanda (Ingemar Johansonn), Abdul Kigunya, Guy Hamza...list ni ndefu sana.
Najilaumu kwa nini sikugeuza camera yangu nikawapiga Everton mazoezini.
Mwaka wa 1967 Everton ikawa Saigon.
Sent using Jamii Forums mobile app