Everton vs Saigon 1967


Na atakua amevaa hilo vazi huku akinywa alikasusu.
 

No wonder kipindi kile wale jamaa wa pale airport ilibidi wakutengee choo chako ili waangalie kama umebeba ngada.
 
Ndugu zanguni note mnaofuatilia huu mjadala kama London alivyoshauri ni kweli hapana tija ya mimi kumjibu huyu ndugu yetu.

In Shaa Allah nitakuleteeni mkasa wa uchaguzi wa 1995 Dodoma kupata jina la mgombea wa CCM.
Hauna sababu ya kumjibu nakereka sana unapojibu kwa hekma yeye analeta dhihaka na matusi!
 
Ndugu zanguni note mnaofuatilia huu mjadala kama London alivyoshauri ni kweli hapana tija ya mimi kumjibu huyu ndugu yetu.

In Shaa Allah nitakuleteeni mkasa wa uchaguzi wa 1995 Dodoma kupata jina la mgombea wa CCM.
Itakua vzr mno Muft
 
Itakua vzr mno Muft
Muuza...
Mimi si Muft wala si Ustaadh.

Nimerudia mara kadhaa hapa kutahadharisha kuhusu hili.

Hizo ni fani za wengine mimi sikujaaliwa na kwa kuwa ni vyeo katika Uislam si vitu vya kufanyiwa maskhara kwa kunitumia mimi.

Haipendezi.

Ikiwa unapendezewa kunivika joho basi nifunge kilemba kwa sifa nilizonazo si kwa elimu ambayo sina.

Mimi ni huyo hapo chini:

PUBLICATIONS/RESEARCH PAPERS/ARTICLES
The Life and Times of Abdulwahid Sykes 1924 –1968 The Untold Story of the Muslim Struggle against British Colonialism in Tanganyika, Minerva Press London, 1998 translated into Kiswahili as Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes 1924-1968 Historia Iliyofichwa Kuhusu Harakati za Waislam Dhidi ya Ukoloni wa Waingereza, Phoenix Publishers, Nairobi, 2002
The Torch on Kilimanjaro, Oxford University Press, Nairobi, 2006
Contributing author for an African anthology: The Mermaid of Msambweni and Other Stories, Oxford University Press 2007, Nairobi.
Contributing author Dictionary of African Biography (DAB), Oxford University Press 2011, New York
Uamuzi wa Busara, Abantu Publications 2008, Dar es Salaam
Watu Mashuhuri Katika Uhuru wa Tanganyika No. 1, Ibn Hazm Media Centre, 2018, Dar es Salaam
Watu Mashuhuri Katika Uhuru wa Tanganyika No.2, Ibn Hazm Media Centre 2018, Dar es Salaam
Dar es Salaam na Wazalendo Wake Mashujaa Katika Kupigani Uhuru wa Tanganyika Ibn Hazm Media Centre 2018, Dar es Salaaam
Watu Mashuhuri Katika Kuulingania Uislam Tanzania, Sheikh Ilunga, Ibn Hazm Media Centre 2018, Dar es Salaam
Dola, Kanisa na Tatizo la Udini Tanzania, Ibn Hazm Media Centre, 2018, Dar es Salaam
The School Trip to Zanzibar, Africa Proper Education Network 2020, Dar es Salaam
Rajabu Ibrahim Kirama, Jemadari wa Vita Kuwa Jemadari wa Uislam, Readit, 2020, Dar es Salaam
In Praise of Ancestors (1987) Africa Events (London)
Abdulwahid Sykes: Founder of Political Movement (1988) Africa Events (London)
Islam and Politics in Tanzania (1989) Al Haq International (Karachi)
The Plight of Tanzanian Muslim (1993) Change (Dar es Salaam).
Tanzania - The "Secular" Unsecular State (1995) Change (Dar es Salaam)

The Question of Muslim Stagnation in Education in Tanzania - A Muslim Riddle (Paper presented at the Conference of the Global World of the Swahili Intercultural Dialogue on the Indian Ocean Zanzibar, February 20 - 23, 2003)

Islamic Education and Intellectualism in Eastern Africa ‘Themes from the Pulpit in Tanganyika (Tanzania Mainland) 1800 – 2000’ (Paper presented at International Symposium on Islamic Civilisation in Eastern Africa Kampala, Uganda organised by the Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA), Istanbul and the Islamic University in Uganda, Mbale December 15th – 17th 2003)

Sheikh Hassan bin Ameir - The Moving Spirit of Muslim Emancipation in Tanganyika (1950 – 1968) (Paper presented at Youth Camp Organised by Zanzibar University, World Assembly of Muslim Youth (WAMY) and Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) 27th February – 4th March 2004)

Islamic Movement and the Christian Lobby in Tanzania - the Experience of the late Prof. Kighoma Ali Malima (1938 – 1995) (Paper Presented to Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) Sokoine University of Agriculture (SUA) Morogoro 11th April 2004)

Terrorism in East Africa the Tanzanian Experience (Paper Presented at the Conference on Islam, Terrorism and African Development University of Ibadan, Nigeria 8th - 10th February 2006)

Al Marhum Sheikh Kassim bin Juma bin Khamis (1940 – 1994) and the Pork Riots of 1993. (Paper Presented at the Regional Conference on Islam in Eastern Africa: Islam Encounter with the Challenges of the 21st Century 1st - 3rd August 2006, Kenyatta University, Nairobi

Muslim Bible Scholars of Tanzania – The Legacy of Sheikh Ahmed Deedat (1918 – 2005) Paper Presented at the International Symposium on Islamic Civilisation in Southern Africa Organised by The Organisation of Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA) The National AWQAF Foundation of South Africa (AWQAF SA 1 – 3 September 2006 University of Johannesburg

Tanzania: A Nation Without Heroes Seminar Organised by IFRA French Institute for Research in Africa and BIEA British Institute in East Africa 23rd and 24th September 2013 at IFRA Nairobi

Awards: Several Awards

Visiting Scholar: (2011)
University of Iowa, Iowa City, USA
Northwestern University, Chicago, Illinois, USA
Zentrum Moderner Orient (ZMO), Berlin, Germany.

OTHER COUNTRIES VISITED
Zambia, Ethiopia, Great Britain, Swaziland, Msumbiji, Zimbabwe, Zambia, Sudan, Egypt, Saudi Arabia, United Arab Emirates, Oman, Yemen, Uganda, Switzerland, Iran, France, Netherlands, Turkey and Abu Dhabi
 
Sawa Ndugu Mwandishi
 
Heshima kwako mkuu, hakika simulizi na uandishi wako hauna mfano, kwa sisi Wakristu tunasema Mungu akubariki sana na akupe maisha marefu ,huu uandishi wako ni mtamu sana, ni kama nasoma vitabu vya Shaaban Robert. Pia leo ndio najua Masimenti kuwa alikuwa anacheza beki kabla ya kwenda Cosmopolitan ya Mansour Magram, mzee wa kukalia mpira! Mungu awarehemu hawa miamba.
 
Nataka kujiunga na klabu yenu, nasikia nyie ndio mnapanga Nani awe Rais wa nchi
Saigon ya sasa sio ile ya akina Kitwana Kondo . Iddi Simba na wageni kama akina Ndolanga, Rage na wengineo ninaowasikia.
 
Mfia...
Amin kwa sote ndugu yangu.

Jumanne tumekuwa pamoja udogoni na kipaji chake cha kucheza mpira kilijitokeza toka utotoni.

Kwa kweli tukimtegemea sana katika kupata ushindi.

Kuna kocha Mjerumani alikuja kufundisha Tanzania alimpa jina la utani Jumanne akamwita, "Tarzan," kwa ajili ya lile umbo lake.
 
Asante kwa hakika unatupa historia iliyotukuka, hicho kizazi cha akina Jumanne ndio kilikuwa cha mpira hasa, walicheza mpira kwa mapenzi na sio kama ilivyo sasa ambapo mpira imekuwa ni ajira , wachezaji wetu wa sasa hawawafikii hata robo wachezaji wa zamani kwa uchezaji wao, sidhani kama kuna wachezaji wa aina ya akina Mohamed Bakari Tall, Mohamed Kajole , Sunday manara na kaka yake pamoja na mdogo wao, Khalid Abeid, Mambosasa.Ahamed Amasha. Boy Wickens, Adamu Sabu na wengineo wengio ambao ndio wamemalizia kizazi cha mpira uliotukuka.
 
Usisahau kuhusu tukio LA mwaka 1995 aliyepindua meza ndani ya chimwaga na kumuwezesha mwela wa lupaso kuongoza nchi uliahidi utalihadithia
Muuza Viatu,
Mkutano Maalum wa NEC uliitishwa kuchagua mgombea urais kwa tiketi ya CCM na Jakaya Mrisho Kikwete akashinda akifuatiwa na Benjamin William Mkapa, Cleopa Msuya akiwa wa mwisho.

Kwa kuwa Kikwete hakuweza kupata ‘’absolute majority,’’ ikabidi uchaguzi urudiwe.

Ukumbi ulikuwa umegubikwa na ‘’tension,’’ nzito wajumbe wa CCM walipokuwa wanapiga kura kuchagua kati ya Kikwete na Mkapa.

Jiulize msomaji wangu hii ‘’tension,’’ wasiwasi ulisababishwa na nini ilhali wagombea wote ni wa chama kimoja?

Iweje wajumbe wapate shinikizo la damu ghafla?

Walikuwa wanatishwa na jinamizi lipi?

Kuna tofauti gani katika ya hawa wagombea wawili wa chama kimoja?

Mpashaji wangu alinifahamisha kuwa baadhi ya wajumbe walikuwa wakinong’onezana ndani ya ukumbi wakati wa kupiga kura.

Alipofika hapa nikamsimamisha mpashaji wangu nikamuuliza, ‘’Wewe ulitegemea Kikwete ashinde dhidi ya Mkapa?’’

Mpashaji wangu alicheka akasema, ‘’Alipoingia Mkapa katika kinyang'anyiro kile nilijua yeye atakuwa rais wala sikuwa na wasiwasi kwa kuwa naijua nguvu iliyokuwa nyuma yake kwanza na pili nazijua siasa za Tanzania. Mimi nilikuwa natazama ile senema na kuangalia itaishia wapi hasa pale Kikwete alipoingia dakika za mwisho baada ya Prof. Malima. Nilijua sasa kocha anamwingiza mfungaji magoli timu ichukue kikombe.’’

Nikamuuliza mpashaji wangu, ‘’Huyu kocha nanI?’’

''Tulizana tumia ubongo wako utamjua,'' Mpashaji alinijibu.

Duru ya pili Kikwete akabwagwa na hivi ndivyo Mkapa alivyokuja kuwa Rais.

Katika ukumbi ule ule wa Chimwaga mwaka wa 1992 hali inayofanana na hii ya 1995 kati ya Kikwete na Mkapa, Prof Malima alibwagwa alipokuwa anagombea kuingia NEC iliyokuwa na viti 20.

Prof. Malima hakuanguka hivi hivi tu mpango makhsusi ulikuwa umepangwa ndani ya CCM dhidi yake na alipoangushwa wabaya wake walikesha wakisheherekea ushindi wao.

Kikwete kama Prof. Malima halikadhalika hakuanguka hivi hivi.

Kama walivyosheherekea kuangushwa kwa Malima miaka mitatu iliyopita halikadhalika ulifanyika mkesha Dodoma kwa kuanguka kwa Kikwete.

Msomaji wangu huoni kuna ‘’variable,’’ zinazofanana katika yale yaliyotokea kwa Prof. Malima 1992 na haya yaliyomfika Kikwete 1995?

Swali la kujiuliza nani anavuruga hizi kete kwenye dama?

Mwalimu Gurumo wa Msondo Ngoma, Juwata Jazz alikuwa akisema,’’Msondo ngoma akili kichwani mwako.’’
 
Nimekuelewa Mo,Said
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…