Everything is funny as soon as it is happening to somebody else

Everything is funny as soon as it is happening to somebody else

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Huu ni msemo ambao uko na ukweli mwingi ndani yake. Leo ningependa kupima validity ya huu msemo kwa kutumia kauli za viongozi wa Tanzania. Kimsingi watz wengi hatuna ushirikiano na tuko kibinafsi zaidi. Mf ni yule bi mkubwa aliyevuliwa hijab kule Iringa waislamu wali Rise ila walivyojua ni mkristu wakanyamaza nilitafsiri kuwa wakristu hawana haki ya kujistiri...

Katika kipindi cha katikati kumekuwa na kauli mbovu kutoka kwa DR. John Magufuli na watu wakazifurahia kwa kuwa hazikuwa kauli zilizogusa maslahi yao moja kwa moja. Ila hawakuzichunguza zile kauli kwa undani wake. watu waliona raha na utani(funny because it was to others not themselves).

Juzi JUzi hapa waziri mkuu nae kasema raia wagongwe marungu. Watu ndo wakaanza kupaza sauti zao za mafua..eti watu wanapigania haki zao..kwani makandarasi na wananchi wa kigamboni walikuwa wanapigania haki ya nani kama sio haki zao? mbona mlizifurahia kauli za magufuli?

Jana naibu waziri wa elimu kawaambia wanafunzi wa elimu ya juu wakauze mbuzi na ng'ombe ili wajisomeshe. je ni nani amejiuliza usahihi wa kauli hii? Wote tupo kimya na kuona kuwa kiongozi kasema sahihi..naona wazi taswira ya mawazo ya Shaaban Robert kama tulipata kusoma kitabu cha KUSADIKIKA. Ndio haya, hadi waandisha waanze kuandika ndio watu wataanza kusema ni Kweli! ni kweli!...kumbe hatutumii mawazo yetu ila mawazo ya waandishi...everything is funny as soon as it is happening to somebody else.

Tupende kushikamana watz ili kufikia maendeleo kwa kila sekta, tuangalie haki na sio upendeleo. Wabunge hufurahi kupata posho kwa kulala bungeni, na wanazipigania. walimu wakisistiza haki zao wanaonekana wakorofi. Usiponisaidia ktk shida zangu kwa sababu unaona hazikuhusu usije ukaniomba msaada wakati wa shida zako
 
Back
Top Bottom