Evo Morales: UN Headquarters should be moved from New York because of US "blackmail" and bullying

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2010
Posts
17,005
Reaction score
20,425
Rais Evo Morales wa Bolivia amesema kuwa makao makuu ya Umoja wa Mataifa yanapaswa kuondolewa New York Marekani na kupelekwa katika nchi nyingine kutokana na siasa za Washington za kutoa vitisho na kutumia mabavu dhidi ya nchi nyingine.

Rais wa Bolivia ambaye alikuwa akihutubia kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, amesisitiza kuwa makao makuu ya Umoja wa Mataifa yanapaswa kuwa katika nchi inayoheshimu sheria na makubaliano yote ya kimataifa na isiyotoa hifadhi kwa magaidi na kuwalinda mafisadi.

Morales amelaani hatua ya Marekani ya kumzuia Rais wa Venezuela kuhudhuria mkutano wa 68 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York na kuongeza kuwa, haiwezekani kwa mtu asiyeamini ubeberu na mfumo wa kibepari kuwa na usalama mjini New York.

Morales vilevile amemkosoa vikali Rais Barack Obama wa Marekani na kusema: Obama hawezi kuzungumzia amani na uadilifu wakati nchi yake inaendelea kuingilia masuala ya nchi nyingine na kufanya dhulma katika nchi hizo.

Naunga mkono msimamo huu na hata comrade Hugo Chavez alisema
 
Jamaa kapasua jipu pwaaa, kama mbwai na iwe mbwai safi sana kaongea bila kuuma kuuma maneno
 
Tatizo liko clear lakini tusisahau kwamba the greatest contributor wa UN ni USA, unaweza kuwa na usawa na bosi kwenye kutoa maoni lakini sio katika kutoa maamuzi.
 
Yericko,
Unaonaje makao makuu yakipelekwa kwenye ile nchi yenu ya Lebanon ambayo Rais wake ni "Snake ze Master"?
 
Amesema kweli lakini USA anachangia asilimia 25+ ya bajeti ya UN!.......
hata kimaamuzi lazima atatofautiana na Thailand au Tanzania ambao bado wapo kwenye 0.001........
 
Tatizo liko clear lakini tusisahau kwamba the greatest contributor wa UN ni USA, unaweza kuwa na usawa na bosi kwenye kutoa maoni lakini sio katika kutoa maamuzi.

Kwenye MoU iliyounda UN kuna kipengele kinachompa nguvu mwanachama mwenye "hisa" kubwa,

Lakini naona nguvu ya muungano wa Uchina, India na Urusi vinatoa uwezo wa kura ya VETO yapamoja inayoweza kuipoka hisa/nguvu zote USA
 
Amesema kweli lakini USA anachangia asilimia 25+ ya bajeti ya UN!.......
hata kimaamuzi lazima atatofautiana na Thailand au Tanzania ambao bado wapo kwenye 0.001........

Mimi napendekeza ihamishiwe China maana wanauwezo wa kuindesha bila michango ya nchi yo yote; si mnajua Marekani ni inaongoza kukopa toka China.
 
Amesema kweli lakini USA anachangia asilimia 25+ ya bajeti ya UN!.......
hata kimaamuzi lazima atatofautiana na Thailand au Tanzania ambao bado wapo kwenye 0.001........

Japo USA yenyewe nayo ipokwenye wadaiwa sugu na UN.
 
Yapelekwe La Paz basi, halafu na fungu analotoa mnyamwezi watoe Bolivia.

Baniani mbaya, kiatu chake dawa.

Kama hujajua historia ya makao makuu ya UN kuwekwa NYC na ku address key reasons, huwezi kuondoa makao makuu hayo Gotham City.

Tena New Yorkers wengine wanaweza kufurahi sana kuondolewa ghasia za gridlock and diplomatic immunity drunk pricks.
 
Kuna yale majamaa yenye roho mbaya yalikuwa yanataka kuhamisha makao makuu ya EA Arusha sijui kwanini yasichangamkie hii tenda.
 
Kuna yale majamaa yenye roho mbaya yalikuwa yanataka kuhamisha makao makuu ya EA Arusha sijui kwanini yasichangamkie hii tenda.
Utayashangaa yote yatajifanya rafiki wa USA na kupinga vikali wazo murua la Mr Evo Morales
 
Haya makao makuu hata yakihamia Somalia au Afghanistan bado Muundo ni ule ule. Kwanza mfumo wa UN (UN charter) ibara ya 17 inatoa fursa kwa wanachama wa kudumu kuchagua mahali pa ofisi za UN. Pili Ibara ya 35 ina masharti ya usalama na mawasiliano ambavyo kwa sasa hata yakititoka NY bado yatahamia London,Tokyo,Paris, Berlin au kwa wanachama wengine wa kudumu au wenye nguvukama Russia au China.Angesema katiba ibadilishwe angepatia. Mkutano mkuu yaani UNGA unawashirikisha wakuu wa nchi zote wanachama wa UN, Je ukihamia Somalia tutwaza kuwahifadhi na kuwalinda hao viongozi wote? Ni maoni tu wakuuOTE=Yericko Nyerere;7422136]Rais Evo Morales wa Bolivia amesema kuwa makao makuu ya Umoja wa Mataifa yanapaswa kuondolewa New York Marekani na kupelekwa katika nchi nyingine kutokana na siasa za Washington za kutoa vitisho na kutumia mabavu dhidi ya nchi nyingine.

Rais wa Bolivia ambaye alikuwa akihutubia kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, amesisitiza kuwa makao makuu ya Umoja wa Mataifa yanapaswa kuwa katika nchi inayoheshimu sheria na makubaliano yote ya kimataifa na isiyotoa hifadhi kwa magaidi na kuwalinda mafisadi.

Morales amelaani hatua ya Marekani ya kumzuia Rais wa Venezuela kuhudhuria mkutano wa 68 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York na kuongeza kuwa, haiwezekani kwa mtu asiyeamini ubeberu na mfumo wa kibepari kuwa na usalama mjini New York.

Morales vilevile amemkosoa vikali Rais Barack Obama wa Marekani na kusema: Obama hawezi kuzungumzia amani na uadilifu wakati nchi yake inaendelea kuingilia masuala ya nchi nyingine na kufanya dhulma katika nchi hizo.[/QUOTE]
 
Kwenye MoU iliyounda UN kuna kipengele kinachompa nguvu mwanachama mwenye "hisa" kubwa,

Lakini naona nguvu ya muungano wa Uchina, India na Urusi vinatoa uwezo wa kura ya VETO yapamoja inayoweza kuipoka hisa/nguvu zote USA

Mkuu nchi kama China, Urusi na India ni wazi haviwezi kuishinda USA. Usisahau kwamba diplomatically USA = UK + Canada + South Korea + Israel + USA yenyewe. Na hao jamaa wa Russia economically wapo very weak kuweza kuleta ushawishi wa HQ kuhamishiwa kwao, ni bahati nzuri kwamba cold war ,mind war bado inawabeba lakini nao “washafulia”.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…