Ewe,mjasiriamali jenga uhusiano mzuri na wateja wako.

Ewe,mjasiriamali jenga uhusiano mzuri na wateja wako.

Jack Daniel

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2021
Posts
2,912
Reaction score
12,904
Salaam jamiiforum

Biashara ndiyo mfumo wa maisha tangu enzi na enzi,watu wananunua na kuuziana bidhaa,

Wengi nadhani tunajua habari za Trans Saharan trade,bater trade n.k.

Leo tuangazie procedures za mfanyabiashara mdogo au mjasiriamali wanao miliki biashara chini ya milioni hamsini hadi kumi

Siongelei madon na mafogo wakubwa,ambao wanaweza kufunga Duka wateja wakiwa wapo,ukiuliza muda umeisha au anawahi kikao.au sabato imeingia au anawahi masjid n.k

Wakati wewe mjasiriamali mdogo ukibembeleza wateja ,kuna watu wanabembelezwa,yaani muuzaji anaringa na kujulikana kama ana Kiburi lakini hakuna wa kumzingua,

Unaweza sema anatumia ndumba ama uchawi,hapana.

Ni uwekezaji mkubwa alioufanya,na unakuta kuna bidhaa hazipatikani popote isipokuwa kwake

Lakini mwenzangu na Mimi ukifanya hivyo unaweza kufunga hicho kiduka chako na ukatafuta mchawi.mwisho ukarudi kwenye umasikini

Fanya hivi kudumisha ukaribu na wateja wako

1.Lugha nzuri Kwa wateja.

Hii inasaidia Sana kumfanya mteja arudi wakati mwingine

2.Kuheshimu kila mteja (kutokubagua)

Mfano kuna mtu anataka bidhaa ya elfu tatu.,lakini kabla hujamuhudimia amekuja mteja anataka bidhaa ya laki tatu,halafu unaanza kumsikiliza mwenye hela nyingi kiasi cha Yule mwenye buku tatu aliyetangulia anajisikia vibaya

3.Usiweke vitu vyenye kuleta matabaka

Utakuta mtu kaning'iniza rozali au tasbih dukani kwake , binafsi nadhani haijakaa vizuri kwani inaleta kaubaguzi fulani.

4.Bango la biashara

Ni vyema kuweka bango zuri lenye jina linalovutia wateja kuliko kuweka maneno mabaya yenye kufurahisha watu wachache huku wengi wakikukimbia

5.Usafi katika biashara yako.

Hii iko Kwa wauzaji wa vipuri vya magari na motors zote ,unakuta umeenda kununua bearings,ni mpya lakini inaonekana kama ya zamani ,pakiti ina maoili mara Grease,aisee siyo vizuri.

6.Mpangilio wa bidhaa.

Wateja wengi wanapenda kununua bidhaa kwenye Duka lililojaa,unakuta frem ni dogo lakini vitu vimejaa Hadi raha,usipende kuweka bidhaa ambazo ni chache kwenye frem kubwa.
Utaonekana kama umefilisika kumbe ndiyo unaanza biashara

7.Rangi ya eneo husika

Rangi ina ushawishi mzuri Sana japo unaweza kuta kama hakuna maana ,lakini rangi nzuri huvutia wateja ,lodge, hotels migahawa n.k

8.Kuwa muwazi na mwaminifu.

Bidhaa kama inasumbua ni vema ukamtaarifu mteja mapema kuliko kuuza kitu au spear mbivu ili mradi upate faida. Lakini pia wapo wateja wenye kukuamini wakakuachia pesa ili bidhaa fulani uwaletee,sasa di vizuri kuingiza tamaa Kula pesa ya mteja na kuanza kumzungusha.utaua biashara yako mapema tu

9.Nguvu za miujiza,

Hii ni dhana tu,lakini Kwa Imani watu wanatumia kama ulinzi kwenye biashara zao, uchawi,ndumba,nguvu ya maombi, miraculous, illusion na vingine vingi .

Utadumu na biashara yako itadumu
 
Back
Top Bottom