Ewe Mwanachuo unayehitimu, ongeza Maarifa na Stadi za Maisha kwani Ajira siyo uhakika kama zamani

Ewe Mwanachuo unayehitimu, ongeza Maarifa na Stadi za Maisha kwani Ajira siyo uhakika kama zamani

Jack Daniel

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2021
Posts
2,912
Reaction score
12,904
Elimu ni bahari
Elimu ni hazina
Elimu ni ufunguo wa maisha.

Hii ni baadhi ya misemo inayochochea na kuhamasisha umuhimu wa elimu.

Na muamko si mdogo Kwa miaka ya hivi karibuni ,Watu waliograduate ni wengi hali inayosababisha Ajira kuwa chache kwani mahitaji ni machache kuliko bidhaa zilivyojana sokoni.

Sehemu nyingi wanaajiri Kwa kuangalia mtiririko wa shule ulizosoma na vyuo pia.

Vyuo ambavyo siyo maarufu havikupi uwezo wa wewe kuonekana sana hata kama Una ujuzi badala yake ,anatazamwa mtoto wa fulani na kasoma wapi.

Hapa ndipo rushwa za ngono,pesa na udhalilishaji mwingine unapokuja ili mradi tu mtu apate ajira.wapo ambao wanasomq huku Ajira zikiwasubiri,washatengenezewa mazingira,hivyo mwenzangu na Mimi lazima uwe na backup kabla hujarudi kitaa na kujikuta unachanganyikiwa

Ewe kijana wa kiume usishindane na jinsia ke hata mkihitimu pamoja,mwenzio anachotegemea,wee hustle kupata vitu hivi jihangaishe, pambana usingoje Ajira.

1. Vitambulisho vya uhakika.

2. Leseni ya udereva

3. Passport

4. Kufanya kazi kadhaa za mikono

5.jifunze stadi mpya za maisha.

Utatoboa na pengine kusahau hiyo Ajira,au ukaajiriwa ukiwa na miradi yako.

chukua yanayokufaa.
 
lazima vijana waichallenge serikali iwape ajira ni ujinga kuona nchi inashindwa kuajiri graduate ambao ni sawa na 2% ya vijana wote tz
Geuza upepo kua km Mwijaku anachofanya sasa na alichosomea Chuo haviendani kabisa, Zembwela hana hata Certificate
 
Elimu ni ufunguo wa maisha
Ila ukipewa ufunguo unakuta kofuli wamebadilisha kazi ni wewe kuchagua kuvunja mlango au upitia juu ya dari na ukifanya yote hayo bod wanakukata mkopo wao haijalishi unakusanyiwa chench za watu ili ulipwe wewe.

Nb. Wanachuo kama mnaweza msichukue mkopo, ni heri mkope mje kuuza nyanya kuliko kukopa alafu ukasome uje uteseke kulipa mkopo wa bod huku unalala vibarazani na viatu
 
Back
Top Bottom