tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 24,225
- 22,632
Naingia kwenye mada moja kwa moja. Hakika nilijisikia vibaya na mnyonge sana baada ya JF kutokuwa hewani kwa takribani miezi miwili na ushee. Nilitamani hata niache kabisa kuingia kwenye mtandao wowote wa ikjamii ikiwa JF “isingefufuka”. Lakini kwa kuwa Mungu hawatupi waja wake, hatimaye wanaJF tumerejea tena kilingine kuendeleza gurudumu letu pale tulipoishia.
Mungu ni mwema. Hongera sana viongozi wa JF lakini poleni kwa misukosuko mliyopitia hadi kuturejesha tena hewani. Katika siku zote ambazo JF haikuwa hewani kwa sababu za kidikteta nimekuwa mnyonge sana huku nikiendelea kuvuta subira na kujipa matumaini kuwa ipo siku Mungu atatenda muujiza.
Je, wewe mwanaJF na mtumiaji sugu wa mtandao huu ulijisikiaje kipindi hiki ulipokuwa nje ya ulingo wa JF?