Zemanda
JF-Expert Member
- Jan 10, 2021
- 8,323
- 18,051
Boy child, sorry kwa andiko refu, sipendi kuandika sana ila ni muhimu usome hadi mwisho, jikaze usome hadi mwisho.
Wengi huwa tunastaajabu jeuri/kiburi, dharau, kutokujali /na ukatili wa mwanamke kuondoka nyakati ngumu ambazo huwa tuna declare bankruptcy na kufeli uchumi na maisha kwa ujumla.
Ni ukweli wa wazi kuwa katika nyakati hizi huwa haikwepeki mwanamke kulaumiwa na kupondwa mawe kwa tabia yake mbaya ila pia ndio wakati wako wa majuto na maumivu kukuvaa mwanaume na ukiwa lelemama unaweza ndio ukawa mwisho wako hapa duniani sababu wengine huamua kujitoa maisha au kuchanganyikiwa moja kwa moja.
Leo naomba kuzungumza na that "inner Boy child" ambaye amenyong'onyea au ambaye ameduwaa hajui nini kinaendelea ila anajua tu kuwa mwanamke hukimbia nyakati ngumu na kukuacha solemba bila kukusaidia au kushikamana.
Mwanamke ni kama mfanyakazi wa kampuni yako kubwa wewe ukiwa ndie CEO. Je, wakati kampuni ikiwa active na profitable, huyu muwajiriwa wako huwa mnakuwa nae meza kuu katika vikao vya namna ya kuendesha kampuni, je mgao wa profits za kampuni huwa na yeye yumo nje ya mshahara wake, je anakuwamo ndani ya vikao vya bodi, je, hisa na mtaji wa kampuni unavyokua mkubwa exponentially na yeye huwa mshahara wake unakua exponentially tena kwa rate kubwa? [emoji848]
Sasa jiulize tena, siku kampuni yako ikianza kuanguka na hatimae kupata hasara na kushindwa kujiendesha, unategemea huyu mfanyakazi ataendelea kuwapo hapo ofisini hadi kampuni itakapoweza kusimama tena, huku yeye akija bila matumaini yoyote na anabills za kulipa huko nyumbani, hana uhakika kama kampuni itakufa ama la? Unadhani ataweza? [emoji848]
Unadhani ni kwasababu gani asianze kutuma maombi kampuni zingine kisirisiri au hata wazi wazi na kukupa barua ya kuomba kuacha kazi sababu hakuna anachopata hapo ofisini kwako.
Nakupa scenario nyingine.
Imagine wewe umekutana na mfanyabiashara mwenzako na mkashare hisa za mtaji, faida na hasara ni zenu nyote, uendeshaji wa kampuni ni wa kushirikiana na hakuna ambaye anaweza mtegea mwenzake. Hapa hata siku kampuni ikitetereka huyu partner anaondokaje na hela zake ni sehemu ya mtaji wa kampuni yenu. Ukiumwa anachanganyikiwa sababu wewe una influence kubwa ya uendeshaji wa kampuni na kukosekana kwako kampuni itaanguka na kumuelemea na anaweza choma mtaji na kufilisika akawa masikini.
Hizi scenario mbili zikupe picha ya namna mahusiano ya leo yanakwenda.
Wanawake tunao ingia nao kimahusiano huingia kama waajiriwa na hutegemea kulipiwa kila kitu hata kama wao pia wanakazi na kipato kikubwa kutushinda ( a.k.a hela ya mwanamke ni ya mke ya mume ni ya wote). Hapa ndipo ugonjwa ulipo. Siku wewe utapoanguka wadhani yeye atabakia kufanya nini tena hapo na hakuna maokoto tena? Je, kama wewe inamlipia kila kitu, wadhani yeye pesa yake atsirejesha kwako mwajiri wake kama mchango wa mtaji wa kampuni aliyoajiriwa ili iwaje?
Hivi ndivyo wanawake wa sasa wanastruggle kuwaelewa wanaume mnachotaka sababu wao wanaamini matunzo na gharama tunazowapa na kuwalipia sio jambo la fadhila,shukurani,wala kuwajali bali ni malipo au mshahara au labor charge kama ya muajiri anayomlipa mwaajiriwa. Hawezi kushukuru kwa kitu ambacho ni stahiki yake na ndio maana huwa wanafosi kama ni kitu cha lazima kwao kupewa.
Familia ni taasisi na lazima iwe na umiliki. Wanaume huwa tunaonekana tuna full ownership na authority ya familia and therefore wanawake hujiona ni waajiriwa tu wa taasisi ndio maana hukaa kimkataba au mguu moja ndani mwingine nje wakiamini kila kilichopo ndani ya familia ni cha mwanaume, ili kumiliki chake ni aidha akuibie atengeneze chake kando, au akuombee ufe ili yeye ajitwalie kiwe chake. Na ukisema basi umgawie kile chako kiwe chake mfano nyumba, au biashara, sasa atabaki kuajiriwa na wewe kwa faida gani tena na umeshampatia mtaji wa kujiajiri why asubirie laki tano ya kupelekeshwa kila mwezi na anaweza kutengeneza million kwa kujisimamia.
Hapa ndipo mkaranganyiko ulipo sasa na ndipo wanaume wengi hawaelewi kwann katika huu mtego wao ndio hunasa na kulia kilio cha mbwa koko huku wanawake wakichoropoka kwa kicheko cha ushindi.
Mfano wa pili wa partnership ni pale wewe mwanaume umefocus na maisha yako wewe kama wewe 100% bila kuincorporate mwanamke na ukawa na mafanikio kisha katika haya maisha akatokea mwanamke ambaye nae anajimudu na ana ukwasi wake wa kutosha kisha akaja mtengeneze kitu cha pamoja cha kuwalinda nyote yaani familia,na mkagawana majukumu bila wewe mwanaume kufosi huyu mwanamke awepo maishani mwako yaani ukiwa umempa freedom ya conditional entry na free exist bila kuaffect au kudisturb financial position yako.
Kumbuka wanaume wa sasa , kiuhalisia, huamini na kutamani kuwekeza future zao kutokea ndani ya Ndoa kinyume na wanawake wa kisasa wanavyofanya maamuzi yao. Kwa kurejea mfano wa yule CEO ambaye anawekeza zaidi akili yake kwa mfanyakazi na asiwazie siku atapofilisika na akashindwa mlipa mfanyakazi mshahara, akitegemea mfanyakazi atumie akiba yake ya benki kumkopesha yeye, CEO, katika kulipa bili ndogo ndogo za kampuni na hata kubwa kinyume na mkataba wa ajira akitegemea kulipana fadhila baadae, je mfanyakazi atakuwa tayari kuchukua pesa kwenye akaunti yake kujitunza yeye ili kumsapoti muajiri wake badala ya kutafuta green pastures kwingineko ili ajihakikishie maokoto na kuendelea kutunisha akaunti na akiba zake kwa future yake binafsi?
Nimewapa mifano hii miwili ili mjitathimini formula gani huwa inawaletea machozi baadae halafu mnawalaumu wanawake badala ya kuangalia ni utaratibu gani mnajiwekea ambao huwafanya muishie kuwaona wanawake kama tatizo kumbe ni mkataba mliosaini nao tokea awali wao wanaufanyia utekelezaji wakati ninyi mnakuja lalamikia utekelezaji wa mkataba ukiwa unaendelea.
Najua vijana wengi hawapendi kuhangaisha vichwa kufikiri wanapenda sana vitu vya kumezeshwa. Nyakati zimebadilika sasa, mnamezwa na watoto wa kike ndio maana ninyi mnalia sana wao wanacheka sana. Watoto wa kike wanapay attention kwenye details za mafunzo kama haya wakati ninyi mnakaza mafuvu na kunywa Azam energy mkidhania zinawapa nguvu, sasa subiri uzee ufike, wenzenu wana mali ninyi mnasubiria kufika miaka 60 ili mfe sababu mliklemishwa Wanaume hufa kabla ya mwanamke. Upumbavu huu futeni kichwani.
Jitambueni na mbadili formula ya Maisha. Wanawake wanakwenda na upepo wa namna ninyi mnaendesha maisha yenu hawana jeuri ya kuamua dunia inaendeshwaje.