Melki Wamatukio
JF-Expert Member
- May 3, 2022
- 6,156
- 10,974
Ewe mzazi usimbane bane mwanao wa kike. Wewe na mwanao mtakuja kulia kilio cha mbwa koko
Dhama zimebadilika, mtoto wa kike hachungwi. Hatakiwi kubanwa banwa zaidi ya kupewa elimu ya ujinsia na uzazi ili ajitambue
Hizi habari za eti "Nikikukuta na kijana yoyote wa kiume umesimama naye nitakuvunja taya ya chini" zimepitwa na wakati, atatii kwa kuwa uko karibu naye, siku akipata nafasi ya kusogea mbali na wewe ujue wafwa.
Kuna familia ilihakikisha binti yao hatoki nje ya uzio ili kumuepusha na vijana waharibifu ila mwisho wa siku shangazi mtu alifuma dildo lenye size ya kutosha kwenye begi la nguo la binti, hakutaka kusemea kwa wazazi wa binti. Baada ya matokeo ya kidato cha nne, binti alifaulu na kwenda kidato cha tano, kwenye zile wanaita School Bush za welcome to Form Five alitikiswa tikiswa mapera akajikuta kaachanisha mapaja, kama mjuavyo mkono wa kupokea, binti akapata mimba kiulaiiiiiiini
Mwingine alilelewa kwa viboko vingi sana mpaka akili ikamtune kuwa kukaa ama kuzungumza na mwanaume au tu kucheka naye ni chukizo kubwa sana mbele ya Mwenyezi Mungu, ni kosa kubwa mbele ya wazazi na ni mtizamo mbaya sana katika jamii. O'level alisomea shule ya dini. Advance kaenda ugirlzini. Baada ya kuhitimu kidato cha sita akaenda chuo kwa tiketi ya kukosa mkopo, mwaka wa pili ada ikamshinda kulipa, akaamua kumpatia babu mmoja mzee zee bikra yake kwa eti kile kinachosadikika kusaidiwa kulipa ada, zee limedonyoa vya kutosha na ada haikulipwa. Kama msingembana bana binti yenu, hiyo tunu ya maisha yake si angempatia kijana ambaye angetokea kumpenda! Ona sasa kaunga damu yake swafi na ya mzee, agano la ovyo😭
Usimchunge mwanao wa kike kupita kiasi. Muachie muda wa kusocialize (Kujamiiana) na vijana wenzie, kubadilishana mawazo ya hapa na pale dhidi ya elimu na maisha.
MWambie ukweli kuwa akitokea kijana wa kiume akakudumbukizia dubwasha lake lenye kichwa huko ndani, utapata ujauzito.
Tafuta magazine zinazohusiana na njia za kujikinga dhidi ya magonjwa ya ngono, UKIMWI (ambao siku hizi haupo) na mimba zisizitarajiwa, tupia hata juu ya dining table, wacha hapo yazagae zagae, watoto wa kike ni wadadisi sana, ni lazima atayasoma tu na kugain kitu
Akikwambia Baba naenda kwao Magreth kujisomea, mwambie Nenda, ila rudi mapema kabla ya saa 12. Mtishe kidogo mwambie "Ukipata ujauzito nakutoroka". Hakikisha mwanao ni mdau wa mada za ujinsia, mtengeneze mazingira ya mijadala kama ya Fema & Femina Hip hasa hasa habari za akina mpwenda Aunt.
Usimbane bane mwanao wa kike, maake akipata chance ya kwenda mbali na wewe kikwazo, ujue wafwa.
Mwache mwanao dunia imzoee na yeye aizoee ili tupate kile tunachoita Sweetness Cycle
Msiseme sikuwaambia...