Kwa nini serikali inapanga bei za mafuta katika uchumi wa soko huria kupitia taasisi yake ya EWURA?
Hili wazo la kuipa taasisi ya kiserikali jukumu la kibiashara kuwapangia bei wafanyabiashara binafsi lilitokana na sababu zipi za msingi na limekuwa na manufaa gani mpaka sasa kwa walaji wa mafuta?
Katika soko huria kama hakuna mapungufu ya kisoko katika ushindani katika biashara husika katika sekta binafsi, uingiliaji wa serikali kwa mtindo huu huwa ni hasara zaidi kuliko faida na ni chanzo cha matatizo mengi zaidi kama uhaba usio wa lazima na "rent seeking".
Kazi na Majukumu ya EWURA
Kwa mujibu wa Kifungu cha 7 cha Sheria ya EWURA, majukumu ya Mamlaka niajukumu hayo ni:-
Kutekeleza kazi zote zilizoanishwa kwenye sheria ya EWURA na Sheria za Kisekta;
Kutoa, kuhuisha na kufuta leseni;
Kuweka na kusimamia viwango vya ubora wa huduma;
Kudurusu na kusimamia bei za huduma,
Kutunga sheria ndogo na kanuni;
Kufuatilia maendeleo ya sekta zinazodhibitiwa kwa kuzingatia upatikanaji, ubora wa huduma, gharama ya huduma, ufanisi wa uzalishaji, uwekezaji na usambazaji wa huduma;
Kusimamia utatuzi wa malalamiko na migogoro;
Kutoa taarifa kuhusu kazi za udhibiti;
Kupata maoni ya mamlaka zingine za kiudhibiti;
na
Kusimamia utekelezaji wa Sura Na 414 ilyoianzisha EWURA.
Katika kutekeleza kazi zake, EWURA ina wajibu wa kukuza ustawi wa Watanzania kwa kuzingatia yafuatayo:-
Kuhimiza ushindani wenye tija na ufanisi kiuchumi;
Kulinda maslahi ya walaji;
Kulinda mitaji ya kifedha ya watoa huduma;
Kuhimiza upatikanaji wa huduma zinazodhibitiwa kwa makundi yote ikiwamo wenye vipato vya chini,makundi maalumu na vijijini;
Kuimarisha utoaji wa elimu kwa umma na kujenga uelewa kuhusu sekta zinazodhibitiwa, ikiwamo haki na wajibu wa watumiaji na watoa huduma zinazodhibitiwa, namna ya kupokea na kutatua malalamiko na migogoro na kazi, wajibu na shughuli za Mamlaka;
Kulinda na kutunza mazingira.