Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,067
- 10,938
UTANGULIZI
1. Kwanza kabisa, tunawashukuru kwa mwitikio na kufika kwenu kwenye mkutano huu muhimu. Leo tutazungumza masuala ya kitaifa kuhusu Ushiriki wa Watanzania katika Mradi wa Bomba kutoka Hoima (Uganda) hadi Tanga (Tanzania). Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (pamoja na taasisi zake) inatambua nafasi ya vyombo vya habari katika kuhabarisha na kuwaletea maendeleo wananchi. Kwa kutambua umuhimu huo, tumewaita hapa ili mweze kushiriki kuhabarisha umma kuhusu Mkutano wa Wadau kuhusu fursa za Mradi wa Bomba la Mafuta utakaofanyika tarehe 23 Februari, 2018.
MRADI WA BOMBA LA MAFUTA GHAFI
2. Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi ni Mradi wa Sekta binafsi unatekelezwa katika nchi mbili (Uganda na Tanzania). Mradi huo unakadiriwa kugharimu Dola za Marekani 3.55 bilioni na kuleta ajira za kati ya watu 6,000 na 10,000 ndani ya miaka mitatu (3). Mafuta Ghafi ya Hoima (ya aina yake), yatasafirishwa kutoka Uganda kwenda sokoni nchi za nje, kupitia Tanzania. Mradi wa Bomba umbali wake ni kilometa 1,445 ambapo kilometa 298 zitakuwa nchini Uganda, na kilometa 1,147 zitakuwa nchini Tanzania.
3. Mradi huo utapita katika wilaya 9 nchini Uganda na wilaya 24 nchini Tanzania, kutakuwepo na kambi sita nchini Tanzania zitakazojengwa ili kuendesha Mradi huo. Mradi huo utajengwa kwa Sheria za Uganda na Tanzania, ambazo zitazingatiwa wakati wa kuandaa mikataba. Kwa sasa, Mradi huo unaongozwa na wabia wake wakubwa, TOTAL East Africa Midstream B.V. yenye ofisi nchini Uganda na Tanzania. Mikataba itakapokaribia kutiwa saini, itaanzishwa Kampuni ya East Africa Crude Oil Project (EACOP) ili kuendesha shughuli za Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi.
SERA, SHERIA NA KANUNI
4. Kwa mujibu wa Sera ya Taifa ya Nishati, 2015 (The National Energy Policy, 2015), Sheria ya Mafuta, 2015 (The Petroleum Act, 2015) na Kanuni za Ushiriki wa Watanzania kwenye Tasnia ya Mafuta na Gesi Asilia za Mwaka 2017 (The Petroleum (Local Content) Regulations, 2017) zinayataka kampuni za mafuta na gesi asilia hapa nchini kutoa kipaumbele kwa kampuni za kizalendo kushiriki (si chini ya asilimia 25 ya hisa) kupitia ubia (JV) kwenye fursa za kiuchumi zinazojitokeza kwenye Tasnia ya Mafuta na Gesi Asilia ilimradi kampuni hizo ziwe na uwezo wa kufanyakazi ama kutoa huduma iliyokusudiwa. Fursa zinazolengwa ni pamoja na ajira, kuuza bidhaa na huduma, kupata mafunzo ya kitaalam/kiufundi, na uwezeshaji wa kiteknolojia.
5. Sheria ya Mafuta ya Mwaka 2015 inaipa EWURA nguvu ya kusimamia mkondo wa kati na chini kwenye Tasnia ya Mafuta na Gesi Asilia kwa upande wa Tanzania Bara. Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima hadi Tanga upo kwenye mkondo wa kati hivyo kwa mukhtadha huo shughuli za bomba hilo litasimamiwa na EWURA katika nyanja za kiufundi, kiuchumi na kiusalama (technical, economic and safety). Kampuni itakayoundwa kuendesha shughuli za bomba la mafuta itaomba na kupewa leseni ya shughuli za kuendesha bomba kutoka EWURA.
6. Baada ya kutungwa kwa Sheria ya Mafuta, 2015 Waziri mwenye dhamana ya masuala ya nishati alitunga Kanuni za Ushiriki wa Watanzania kwenye Tasnia ya Mafuta na Gesi Asilia, 2017 (The Petroleum (Local Content) Regulations, 2017). Kanuni hizi ni kwa ajili ya mkondo wa juu, wa kati na wa chini wa Tasnia ya Mafuta na Gesi Asilia hapa nchini. Mkondo wa juu unasimamiwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Petroli wa Mkondo wa Juu yaani “The Petroleum Upstream Regulatory Authority (PURA)”. Upande wa mkondo wa kati na wa chini unasimamiwa moja kwa moja na EWURA
MAMBO YA MSINGI
7. Sera, Sheria na Kanuni zinaainisha mambo kadhaa ya msingi katika kusimamia ushiriki wa watanzania katika miradi mbalimbali ya shughuli za petroli (mafuta na gesi asilia). Malengo makuu ya Sera, Sheria na Kanuni ni pamoja na:
9. Ndugu Waandishi wa Habari, kwa wakati wote mtaona taasisi kama Wizara ya Nishati, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Baraza la Taifa la Uwezeshaji (NEEC), Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) zikishiriki kwa njia moja au nyingine. Kwa sasa, taasisi hizi zinashirikiana kwa karibu kuweka mazingira sawa ya ushiriki katika Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi.
10. Kwa niaba ya Serikali, masuala ya sera, sheria na kanuni yanashughulikiwa na Wizara ya Nishati. EWURA inashughulikia masuala ya udhibiti wa shughuli za mafuta, bomba likiwa mojawapo. NEEC inajishughulisha zaidi na uwezeshaji wa Watanzania (kielimu, na kifedha) ili washiriki katika Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi. TPDC itashiriki kama mbia katika uwekezaji na upatikanaji wa mkuza wa Bomba la Mafuta Ghafi. Kwa kuwa sekta binafsi inatarajiwa kushiriki kikamilifu, sekta hiyo itaunganishwa na TPSF. Lengo kuu, ni kuhakikisha kuwa, kwa kuwa asilimia 80 ya bomba itajengwa Tanzania, angalau asilimia 60 ya gharama zote wakati wa ujenzi zinaingizwa kwenye uchumi wa Tanzania.
11. Mkutano wa tarehe 23 Februari, 2018 hapa Dar es Salaam, EWURA itafafanua vipengele mbalimbali vya Kanuni za Ushiriki wa Watanzania kwenye Mradi wa Bomba la Mafuta. Lakini pia, EWURA inao wajibu wa kutengeneza kanzidata (database) ya watoa huduma wa ndani (local suppliers and service providers) kwenye tasnia ya mafuta na gesi asilia. Tangazo la kuanza kwa usajili wa makampuni na watoa huduma wa ndani lilitoka tarehe 25 Januari 2018 kwenye magazeti ya Daily News na Habari Leo. Tangazo hilo pia lipo kwenye tovuti ya EWURA. Muda wa kujisajili ulifunguliwa tarehe 29 Januari, 2018 na utakamilika tarehe 28 Februari, 2018. Tunawaomba waandishi wa habari mpaze sauti ili Watanzania wengi wajisajili EWURA ili waweze kushiriki kwenye kinyanganyiro cha kupata watoa huduma wenye weledi, uzoefu na ari ya kutuoa huduma.
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA)
Dar es Salaam, Februari 2018

(a) kuwezesha uongezaji wa thamani ya bidhaa na huduma hapa nchini;
(b) kuzalisha ajira kupitia wataalam wa ndani na matumizi ya bidhaa na huduma za ndani, makampuni na huduma za kifedha za ndani;
(c) kuzalisha uwezo wetu wa ndani kupitia elimu, ujuzi, teknolojia, tafiti na maendeleo, na uvumbuzi;
(d) kuongeza uwezo na ushindani katika ngazi ya kimataifa wa wazawa na makampuni ya kizalendo kwenye Tasnia ya Mafuta na Gesi Asilia; na
(e) kushiriki na kusimamia miradi ya maendeleo na watanzania wenyewe.
8. Fursa zinazotarajiwa ni pamoja na hizi zifuatazo-(a) usafiri na usafirishaji wa watu na mizigo;
(b) huduma za ulinzi (private security);
(c) kuzalisha na kuuza mazao ya vyakula na mifugo;
(d) huduma za kupika vyakula na kutoa vinywaji baridi;
(e) huduma za malazi ya hotelini na dhifa ya wageni;
(f) vifaa na matumizi ya maofisini;
(g) huduma ya kuuza mafuta ya petroli na dizeli;
(h) huduma za utayarishaji mkuza (survey);
(i) ukodishaji wa mitambo (excavator na crane hire);
(j) kazi ya kuchimba mitaro na kujenga nyumba (civil works);
(k) huduma ya kupokea na kutuma mizigo (clearing and forwarding);
(l) kuuza malighafi za ujenzi zinazopatikana hapa nchini
(m) huduma za teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA);
(n) huduma ya kukusanya na kutupa taka (water and solid waste management);
(o) ujenzi wa barabara za muda na za kudumu (access roads)
(p) matengenezo ya mitambo mbalimbali na uuzaji wa vipuri;
(q) uchimbaji wa visima vya maji kwenye mkuza wa bomba la mafuta ghafi litakakopita;
(r) ukodishaji wa magari kwa ajili ya wafanyakazi wa mradi kama vile mabasi;
(s) ujenzi wa kambi za kuishi wafanyakazi wa mradi wakati wa ujenzi na nyumba za kudumu wakati wa uendeshaji;
(t) uuzaji wa majenereta (portable generators) kwa mahitaji ya dharura mara kwa mara;
(u) huduma za kiuhandisi na ushauri nasaa (engineering consultancies);
(v) ukodishaji wa ndege aina ya helicopter kutoka Tanga hadi Hoima;
(w) huduma za afya (madaktari, madawa, magari maalum ya wagonjwa) kwenye kambi za wafanyakazi;
(x) mavazi ya kiusalama mahala pa kazi (PPE equipment kama rain gear, hard hats, safety boots, na safety glasses);
(y) maghala ya kuhifadhia vifaa vya mradi (storage and warehouse);
(z) ujenzi wa fensi kuzunguka vituo vya kupashia moto bomba;
(aa) huduma za bima (insurance services);
(bb) huduma za kifedha (banking services); na
(cc) huduma za kisheria (legal services)