Tamko hilo la EWURA linalofafanua kuhusu taarifa yao ya Septemba 4, 2023 linakuja muda mfupi tangu Waziri Mkuu akiri Bungeni kuwa kuna changamoto ya upatikanaji wa Nishati hiyo katika baadhi ya maeneo Nchini.
Kupitia taarifa yake kwa Umma,
#EWURA imefafanua inaposema akiba ya Mafuta iliyopo inatosha kwa siku 19 maana yake inakidhi mahitaji ya Kisheria yanayotaka Maghala ya Hifadhi kuwa na Mafuta yanayotosha kwa siku 15.
Aidha, EWURA umeongeza kuwa inaposema mafuta yanatosha kwa Siku 19 haina maana baada ya siku hizo kutakuwa hakuna Mafuta Nchini.