EWURA toeni ufafanuzi wa katazo la kuuza mafuta kwenye vidumu

EWURA toeni ufafanuzi wa katazo la kuuza mafuta kwenye vidumu

pombe kali

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2014
Posts
282
Reaction score
561
Ni kitu cha ajabu na kushangaza, nina kimashine changu nyumbani ambacho kinatumia petrol, miaka yote nimekuwa nikinunua mafuta kwenye vituo

Siku za hivi karibuni nilienda kituo cha mafuta fulani nikaambiwa kuwa wamekatazwa na EWURA kuuza mafuta kwenye vidumu, nikaomba kumuona msimamizi wa kituo akaniambia kuwa hilo ni agizo. Nikamuuliza kwa generator yangu nitawezaje kujaza mafuta? Akanijibu kuwa natakiwa nilibebe Generator ndiyo niende nalo hapo kituoni

Nikaenda kituo kingine na majibu niliyopata ni yale yale, nikakutana na watu kadhaa ambao magari yao yamezima barabarani na wamekuja na vidumu ambao pia waliambiwa hawaruhusiwi kuweka mafuta kwenye vidumu

Ombi langu kwa mamlaka husika ni kuomba ufafanuzi rasmi kwa siye ambao tunatumia mashine ambazo hazitembei na tunahitaji kuweka mafuta.

Mhudumu lete bia nyingine

Pia soma > KERO - Mafuta ya Petroli kuuzwa kwenye madumu kisha kusafirishwa katika magari ya Abiria sio salama, EWURA -Dodoma mpo?
 
Watu wanaoishi maporini na Wana mashine za kusaga zinazosaidia jamii zao ,Kuna watu maporini Wana pikipiki zao na vyombo vingine vingi so na wao wawe wanabeba majenereta Yao,mamashine Yao,mapikipiki Yao Hadi mjini kuyaweka mafuta..aisee
 
Sheri nyingi ukijaza moja kwa moja unaibiwa kwa pamp wanaiminya...kidumu hawezi kukuibia! Mwanzoni nilidhani uongo Baadaye, usiku wa saa saba nikapita Sheri moja nikamkuta jamaa anakamua mafuta aliyobinya Mchana na kujaza kwa chupa za Maji kisha anawauzia boda boda!!!
 
Back
Top Bottom