Ni kweli Masebu kasema hayo? kama mambo yataachwa yalivyo sasa, tutegeme tatizo kubwa la upatikanaji wa mafuta kuanzia miezi miwili au mitatu ijayo maana inawezekana makampuni makubwa ambayo huingiza mafuta yameshaanza kufanya cancelation ya order zao za mafuta kwa miezi inayokuja.Principles nzuri za biashara zataka kila kitu kifanyike wazi na hapo sasa ewura ndio wanatakiwa kuwa kweli regulator. Naona kwa hii issue ya sasa, Ewura imeamua kutumia mabavu kupitisha formula ile ili mafuta yashuke bei. Kwanini tusianze na kupunguza dermurage cost ambazo kwa kweli zipo ndani ya uwezo wetu? Hivi meli husubiri kwa muda mrefu kiasi gani kabla ya kushusa mafuta KOJ na nani analipia gharama za ucheleweshaji huo?
Kwa mtazamo wangu mimi kama KOJ iko congested, serikali ingeingia ushirika na makampuni ya mafuta kujenga bomba lingine la kushushia ili kuondoa gharama zisizo za lazima.
Approach ya sasa inaleta matatizo mengi kuliko unafuu maana nina shaka sana na upatikanaji wa mafuta siku za baadae kama hali itakuwa hivi.