EWURA yaonya uuzaaji petrol kwenye madumu

PureView zeiss

JF-Expert Member
Joined
Sep 5, 2016
Posts
10,786
Reaction score
35,916
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetoa tahadhari kwa umma kutokana na kuongezeka kwa matukio ya milipuko ya moto yanayotokana na uhifadhi wa mafuta ya petroli kwenye vifaa visivyo salama kama madumu na chupa za plastiki.

Katika taarifa hiyo, EWURA imewaonya wamiliki wa vituo vya mafuta nchini kuhakikisha wanazingatia tahadhari za Usalama, Afya, Mali na Mazingira (HSE).

Taarifa hiyo iliyotolewa Septemba 16, 2024 na Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, ilisisitiza kwamba kanuni za biashara ya vituo vya mafuta, zilizowekwa kupitia Kanuni Namba 27 ya mwaka 2022, zinakataza matumizi ya vifaa visivyohusiana na mafuta kama vile madumu na chupa kwa ajili ya uuzaji au uhifadhi wa mafuta.

"Ni jukumu la wamiliki wote wa vituo vya mafuta kuhakikisha kuwa wanachukua hatua stahiki kuzingatia usalama wa jamii kwa kuzuia matumizi ya vifaa visivyokubalika kama vile madumu na chupa za plastiki kwa uuzaji wa mafuta ya petroli," ilisema taarifa hiyo.

Aidha, EWURA imeweka wazi kuwa wakaguzi wake watafanya ukaguzi wa kina kwenye vituo vya mafuta kote nchini ili kuhakikisha kanuni hizo zinaheshimiwa. Wamiliki watakaokiuka kanuni hizo watakabiliwa na hatua kali za kisheria, ikiwemo kufungiwa vituo vyao.

"Tunawahimiza wamiliki wa vituo vya mafuta kuepuka vitendo vinavyoweza kuhatarisha maisha ya watu, mali, na mazingira. Kutofuata kanuni hizi kunaweza kupelekea madhara makubwa," aliongeza Mkurugenzi Mkuu wa EWURA......wale jamaa zangu wa kutembea na vidumu kweli magari yao kama wanafunzi wataacha magari yao.
nyumbani
20240916_124847.jpg
 
1727451466313.jpeg

Mimi leo vijana wangu wamepeleka jenereta petrol station (sheli) kwa toyo. Sasa jirani yangu mashine yake inakunywa lita 100 na ilishushwa kwa crane. Kazi anayo
 
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetoa tahadhari kwa umma kutokana na kuongezeka kwa matukio ya milipuko ya moto yanayotokana na uhifadhi wa mafuta ya petroli kwenye vifaa visivyo salama kama madumu na chupa za plastiki.

Katika taarifa hiyo, EWURA imewaonya wamiliki wa vituo vya mafuta nchini kuhakikisha wanazingatia tahadhari za Usalama, Afya, Mali na Mazingira (HSE).

Taarifa hiyo iliyotolewa Septemba 16, 2024 na Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, ilisisitiza kwamba kanuni za biashara ya vituo vya mafuta, zilizowekwa kupitia Kanuni Namba 27 ya mwaka 2022, zinakataza matumizi ya vifaa visivyohusiana na mafuta kama vile madumu na chupa kwa ajili ya uuzaji au uhifadhi wa mafuta.

"Ni jukumu la wamiliki wote wa vituo vya mafuta kuhakikisha kuwa wanachukua hatua stahiki kuzingatia usalama wa jamii kwa kuzuia matumizi ya vifaa visivyokubalika kama vile madumu na chupa za plastiki kwa uuzaji wa mafuta ya petroli," ilisema taarifa hiyo.

Aidha, EWURA imeweka wazi kuwa wakaguzi wake watafanya ukaguzi wa kina kwenye vituo vya mafuta kote nchini ili kuhakikisha kanuni hizo zinaheshimiwa. Wamiliki watakaokiuka kanuni hizo watakabiliwa na hatua kali za kisheria, ikiwemo kufungiwa vituo vyao.

"Tunawahimiza wamiliki wa vituo vya mafuta kuepuka vitendo vinavyoweza kuhatarisha maisha ya watu, mali, na mazingira. Kutofuata kanuni hizi kunaweza kupelekea madhara makubwa," aliongeza Mkurugenzi Mkuu wa EWURA......wale jamaa zangu wa kutembea na vidumu kweli magari yao kama wanafunzi wataacha magari yao.
Tujenge vituo vya gharama nafuu. Kuuza mafuta kwenye madumu ni hatari kwa usalama wa maisha yetu lakini pia ni hatari kwa afya zetu.

Madumu yanayokubaliwa ni yale ya chuma (jerrycane) ambayo zamani mara nyingi unayakuta kwenye gari za off road. Yale hayana shida na moto.
 
Attachments

  • R (2).jpeg
    R (2).jpeg
    262.7 KB · Views: 9
Back
Top Bottom