EWURA yashusha bei ya mafuta

EWURA yashusha bei ya mafuta

Wambugani

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2007
Posts
1,757
Reaction score
277
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), imepunguaza bei ya mafuta kuanzia leo katika mikoa yote nchini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Ewura, bei ya petroli imepungua kwa Sh. 126 kwa lita (asilimia 5.96), dizeli imeshuka kwa Sh. 32.48 kwa lita (asilimia 1.69) na mafuta ya taa kwa Sh. 50.74 kwa lita (asilimia 2.6).

Taarifa ya Ewura imesema kupungua kwa bei hiyo kumetokana na bidhaa hiyo kushuka katika Soko la Dunia na kuimarika kidogo kwa thamani ya Shilingi ya Tanzania dhidi ya Dola ya Marekani.

Bei hizo zinaanza kutumika kuanzia leo na punguzo hilo litahusu mauzo ya jumla na reja reja kwa mafuta yote nchini ikilinganishwa na toleo lililopita la Desemba 5, 2012.

Ewura imesisitiza kwamba bidhaa za mafuta zitaendelea kupangwa na soko, lakini kwa kuzingatia bei elekezi inayokuwa inapangwa na Mamlaka hiyo kwa kwa kuzingatia Sheria ya Mafuta ya mwaka 2008.

Imesema kampuni za mafuta zipo huru kuuza bidhaa hiyo kwa ushindani ilimradi bei hizo ziko chini ya bei kikomo kama ilivyokokotolewa na fomula mpya iliyopitishwa na Ewura ambayo ilichapwa kwenye Gazeti la Serikali Na. 454 la tarehe 23 Desemba 2011.

Mamlaka hiyo imevionya vituo vya mafuta kwamba visithubutu kuuza bidhaa hiyo bila kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja na adhabu kali itatolewa kwa kituo husika ambacho kitakiuaka maelekezo hayo.

Aidha, wateja wameshauriwa kudai stakabadhi ya malipo inayoonesha jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta yaliyonunuliwa na bei kwa lita.

Taarifa ya Ewura imewataka wateja kutumia stakabadhi hiyo ya malipo kama ushahidi wa endapo kutajitokeza malalamiko ya ama kuuziwa mafuta kwa bei ya juu kuliko bei kikomo, ama endapo atakuwa umeuziwa mafuta yenye kiwango cha ubora kisichofaa kwa Jiji la Dar es Salam petroli itauzwa kwa Sh. 1,993, dizeli Sh. 1,967na mafuta ya taa yatauzwa kwa Sh. 1,973.

Bei kikomo ya jumla kwa petroli kwa Jiji la Dar es Salaam itakuwa Sh. 1,918.60, dizeli Sh. 1,892.97, na mafuta ya taa Sh. 1,898.62 kwa lita moja.

Sikitiko
: Hivi lini watashusha bei ya mafuta ya taa yawe chini ya dizeli
 
Dahh afadhali mwezi huu angalau na mie nitatembeza ka vitz kangu
 
Mbona hii thread umeichelewesha. Mafuta yameshuka kufikia bei hiyo siku ya tano sasa.
 
Tuombe Mungu mgomo baridi wa wenye vituo usianze.
 
Back
Top Bottom