Ex-GF kajitangaza anao, napata kero vibaya

Nenda kapime ujue afya yako na uondokane na huo msongo wa mawazo!!
 

Hongera sana mkuu hasa kwa kujitolea kwenda kupima, wewe ni balozi mzuri... na pia pole kwa wasiwasi!!!
 
Hongera sana Mtu B, sasa uhamasishaji. Pole sana kwa zigo la wasiwasi.
 
hauko peke yako kaka! nenda kapime tu ndio utaujua ukweli wote
 
Mkuu,bila kurefusha hadithi, nenda kapime, vinginevyo utaishi kwa wasiwasi na utajitia maradhi ya fikra bure(stress)

naungana na julius, wala usippate hofu ya bure na wala usijepe matumaini kuwa uko -safe wakati huna uhakika. la muhimu hapa ni kupata vipimo vya kitaalamu, UKIMWI haupimwi kwa macho kaka, nenda kapime upate uhakika, kama unao pole sana lakini kuna namna ya kuishi na ukimwi na ukaendelea na shuhguli zako kama kawaida, na kama huna utajua namna ya kujikinga na kuwa mwangalifu zaidi katika mahusiano, mbona simple tu kama kumsukuma mlevi vile!??
 

Ni maoni yako lazima yaheshimiwe, lakini je ukisikia dawa ipo tayari utakuwa radhi kujitangaza? ni swali tu na pole kwa masaibu yote vumilia si wanasema time will tell?

.....................................
Amani yetu inatumiwa vibaya
 
Mtu B wala usiwe na hofu, Ngoma sio big deal, watu kibao wanayo na wanaendeleza maisha kama kawaida. Wewe kapime ili ujue status yako then uangalie what next baada ya kujijua kama ni HIV negative au positive.

Mimi binafsi namjua mtu ana ngoma sasa yapata 20 + yrs na ukimuona mpaka uambiwe hvhv humjui na ni kiongozi fulani kule shidefa plus au shilika gani sijui yale ya mwanzomwanzo....... so dont ever loose hope maisha yapo upande wako acha huzuni zisizo na mpango.

............................................
Amani yetu inatumiwa vibaya
 
Hongera sana Mtu B, ukweli ni kwamba nilipoanza kushuka na thred sikusoma tarehe hivyo michango yangu iliyotangulia ilikuwa ya kukutia nguvu. na sasa baada ya kukaribia kufika stand yaani mwisho wa thred ndoo nikagundua tofauti (Mambo ya kutumikia Taifa usiku)...
kwa mara nyingine hongera na pole kwa msukosuko wa mawazo naamini chakula kilikuwa hakishuki kwenye kipindi cha mpito.

...................................
Amani yetu inatumiwa vibaya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…