Ex Mayor Jacob Boniface afutiwa mashtaka ya Ugaidi

Huyu mnyakyusa kapitia mengi sana katika umri mdogo.
Kuanzia ualimu, uanaharakati, udiwani, umeya, lupango, kutishwa na Spora Liana/DED, kesi za kubambikizwa, kuibiwa kura za ubunge na mwendazake sasa tupo naye mtaani tena. Hapo hata miaka 40 hajafikisha.
 
Abebaye roho ya ibilisi akiingia katika jamii, jamii yote huwa katika mahangaiko, mateso, chuki, mafarakano na utengano.

Ibilisi akitoweka, akiingia mwenye Roho wa Mungu, jamii hufirahia, hupata matumaini, upendo na umoja huongezeka, mafarakano hupungua, na afya za watu huimarika.

Rais Samia usimwache Bwana hata ukaugeukia uovu, baraka zitakujia, daima utembee na haki badala ya chuki na upendeleo, uishi katika ukweli badala ya unafiki, uukumbatie weledi na ustaarabu badala ya ujinga na ushamba.

Pole Boniface, upo huru siyo kwa sababu ya ujanja wako bali kwa sababu ya mkono wenye nguvu wa Mungu wetu, aliyeamua kuirejeshea furaha nchi yetu baada ya dhiki, mateso, uonevu na maovu mengi.
 
Barikiwa sana mtumishi
 
Isije ikawa yanatengenezwa mazingira ya kuja kubalance matukio kwa kumfutia mashtaka jambazi Sabaya
 
Angefungwa kwayo kama jiwe angeendelea kuwa mfalme
 
Makonda nae anatembea na walinzi na yule activist wa Jiwe jina lake nimemsahau nae anatembea na walinzi!!
 
Mtu wa Hai anaenda kusomewa mashitaka Arusha ili iweje?
Hai hamna mahakama? Na mkoa wa Kilimanjaro je?
Wameogopa mafuriko ya watu mahakamani.

Mahakamani ni sehemu ya kutoa haki kwa hiyo ni vizuri amepelekwa huko ili sasa akina Mbowe wawe wanaenda mahakamani kutoa ushahidi juu ya madai yao.
Mbowe asipoenda kutoa ushahidi mahakamani tutajua ni unafiki tu

Hata Mbowe alikaa Segerea kwa miezi nne na madawa ya kulevya yakaisha mtaani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…