TANZIA Ex-Rhodesia leader Ian Smith dies

MzalendoHalisi

JF-Expert Member
Joined
Jun 24, 2007
Posts
4,679
Reaction score
1,612
Waziri Mkuu wa zamani wa Rhodesia- Ian Smith amefariki dunia! Hali ya Zimbabwe kwa sasa ni tete na ngumu kwa watu wengi. Je huyu Mzungu atakumbukwa Zimbabwe kwa lipi? Smith never believed Africans can rule themselves in 1000 years to come!

The former prime minister of Rhodesia, Ian Smith, has died aged 88.
The cause of his death is unknown but he had been ill for some time at a residential home in South Africa.
He illegally declared independence from Britain in 1965 and his white minority government led the country for 14 years amid international scorn and sanctions.

Following a bitter bush war with black nationalists, his government gave way to a new administration in 1979, leading to the creation of Zimbabwe.

Ian Smith's supporters continued to laud him as a political visionary and a man who understood the uncomfortable truths of Africa.

To his detractors, however, he was an unrepentant racist.

Mr Mugabe's deputy information minister, Bright Matonga, described Ian Smith as a man who brought untold suffering to millions of Zimbabweans.

"We offered him the hand of reconciliation which he never accepted. Good riddance," Mr Matonga was quoted by AFP news agency as saying.

The BBC's James Robbins says that to the end of his days Ian Smith was convinced that Rhodesians, black and white, would have fared better under his leadership than that of Robert Mugabe and his Zanu-PF party.
He died believing he had been vindicated by Zimbabwe's current crisis, with its massive inflation and unemployment.

Sidelined
Steeped in the colonial values of his Scottish immigrant father, Mr Smith was a born leader with a distinguished war record as an RAF fighter pilot, says our correspondent.

He helped to found the right-wing Rhodesian Front, which came to power in 1962, and when the-then prime minister, Winston Field, baulked at the prospect of seizing independence, the party turned to Mr Smith, who gave them what they wanted.

He became prime minister of the then self-governing British colony of Rhodesia in 1964. The following year he made his Unilateral Declaration of Independence and years of civil war ensued.

Ian Smith denied this was caused by the actions of his regime and insisted there was nothing wrong with five million blacks being ruled by 200,000 whites.

In the end, Mr Smith maintained, it was not his enemies who beat him, but apartheid South Africa's threat to cut Rhodesia's lifeline.

Margaret Thatcher's UK government brokered a peace deal in the Lancaster House talks in 1979 and a black-majority government took over Zimbabwe.

Ian Smith remained a key player in Zimbabwean politics until seats reserved for whites were abolished in 1987.

In retirement, Mr Smith was finally relegated to the sidelines.
 
Obituary: Ian Smith


more from the Times
Huyu ni mzungu aliyehakikisha wazungu wenzake wanaishi kwa jasho la waafrika wa Zimbabwe na kuendeleza dhuluma kwa kujiona wao ni bora kuliko binadamu mwingine yoyote.

Viongozi wetu wa kiafrika wanaona sifa kujipendekeza kama malaya kwa wazungu na kuendelea kuwapigia magoti na kuwaona wao ni bora kuliko sisi waswahili. Wanakubali kutumia rasilimali zetu kwa sababu ya peremende wanazopewa na kuingia mikataba ambayo inaendelea kuwanufaisha hawa vibaka. Ukuwadi wao inabidi tuupigie kelele.

Je, wanaweza kuiga mfano wa huyu mzungu na kuwawezesha waafrika wenzao?
 
Acha UPUUZI, huyu alikuwa BORA na bado ni bora hata akiwa amekufa kuliko MUGABE!
 
ahhh bana wee acheni aende akasalimie akina nyerere, iddi amini huko !
 
Jamani let him go in peace regardless of whatever bad he has done but he was in power by that time.

In deed he has done nothing good to be recalled by all africans apart from Zimbabwe people at large
 
Acha UPUUZI, huyu alikuwa BORA na bado ni bora hata akiwa amekufa kuliko MUGABE!

Kweli ni lazima tuelimishane, tusiwe wapuuzi wa kuchukia watu kutokana na rangi zao, racism is stupid. Smith ni binaadamu alikuwa na ushenzi wake, hata leo fanya Smith, lakini huwezi kumlinganisha Smith na Mugabe hata tone, Rhodesia ya Smith ilikuwa inazalisha chakula kilichokuwa kinaliwa na watu wa nchi nyingi tu za Afrika hata Ulaya kwenyewe, na Zimbabwe ya Mugabe watu wake wanakula Panya na haina chakula cha kutosha, export yake kubwa kwa sasa ni wakimbizi. Zimbabwes economy has been brought to its knees by ujinga wa Mugabe, watu wanasingizia Vikwazo vya uchumi(ukweli ni targeted sanctions), wanasahau kuwa hata Smith alikuwa kwenye vikwazo vya kweli na kwenye vita vya ndani, lakini he deliverd the goods. Let us be fair. Rest in peace Ian, God will bless you!
 
Huyu alikuwa bora kuliko huyu mmachinga Mugabe na lip service zake kwa wamandingo wa zimbabwe anawaambia wako huru huku hawana chakula na wakijikuta wakimbizi,Zimbabwe ilikuwa kama nchi nyingine tuu za Ulaya ingawaje ubaguzi ulikuwepo lakini naamini ubaguzi ungepigwa vita kwa style ya America(civil rights movements) na kushare madaraka Zimbabwe ingekuwa mbali sana na ubaguzi ungeisha tuu...South Africa iko vile kwa ajiri ya hao hao makaburu na ubaguzi unaishia!
 

Atakumbukwa kwa hizi quotes
"In 1976 declared he didn't believe in black majority rule, "not in a thousand years"

"There will be no black rule in my lifetime,"
 
He may be right... Look at Mugabe... The guy is not too black to feel the pain of his people... Inflation, hunger, starvation, all in modern Zimbabwe... People remember having enough food when this Ian Right was in power... Mugabe should move out and retire for good. Hapa TZ napo ndipo panapoelekea, yaani uzungu umetawala... Look at the president; he can hardly sit and feel our pain. He is handsome in person and ugly at work! Lowassa, you're just another scumbag! Shein is OK so far!
 
Tangu niwe mtu mzima, kuna kitu kimoja nimejifunza: Ukishakuwa kiongozi wa nchi, no matter what you will do, expect criticism. Kuna wakati hua najiuliza kama kuna kiongozi anaweza kurest in peace bila lawama pamoja na kujitoa kwa ajili ya nchi yake. Simaanishi huyu Smith kwa sababu sijui mengi kumhusu, ni wazo tu.
 
1. Yaani Judy umeongea ukweli tupu! Hata unfanye nini wanadamu watakulaumu tu! I think it is a human nature to critisize viongozi- ni vigumu kweli kutaja jina 1 la kiongozi ambae halaumiwi!

2. Mugabe kweli ana makosa yake, Smith pia alikuwa na makosa yake.

3.Leo hata akichunkua Changivrai wa upinzani watu watamlaumu tu!
 
Zimbabwean: 'We were the enemy'

Kutoka jikoni.
 
--------------------------------------------------------------
Huyu alikuwa bora kuliko huyu mmachinga Mugabe na lip service zake kwa wamandingo wa zimbabwe anawaambia wako huru huku hawana chakula na wakijikuta wakimbizi,Zimbabwe ilikuwa kama nchi nyingine tuu za Ulaya ingawaje ubaguzi ulikuwepo lakini naamini ubaguzi ungepigwa vita kwa style ya America(civil rights movements) na kushare madaraka Zimbabwe ingekuwa mbali sana na ubaguzi ungeisha tuu...South Africa iko vile kwa ajiri ya hao hao makaburu na ubaguzi unaishia!
---------------------------------------------------------------

Du! Watu mna kumbukumbu ndogo kweli, hivi ni bora tuwe watumwa tulioshiba au huru wenye njaa?

Ndio Zimbabwe kuna na matatizo,lakini ikumbukwe kuwa Mugabe ndiye aliyeleta democrasia Zimbabwe.

Wafrika tuna kazi.
 
Du! Watu mna kumbukumbu ndogo kweli, hivi ni bora tuwe watumwa tulioshiba au huru wenye njaa?

Ndio Zimbabwe kuna na matatizo,lakini ikumbukwe kuwa Mugabe ndiye aliyeleta democrasia Zimbabwe.

Wafrika tuna kazi.

Uhuru una maana gani kama umekufa na njaa? ukiwa mtumwa halafu umeshiba utaweza kufikiria jinsi ya kujikomboa, ukiwa huru lakini una njaa huwezi kufikiri chochote maana yake ata uhuru wako wakufikiria unachotaka unakuwa umenyang'anywa. Matatizo ambayo mnayatukuza eti mimi niko huru wakati mwanao amelala na njaa hivi waafrika tumelaaniwa nini? hivi wewe Rubabi unasuuzika roho vipi kuona watoto wadogo kule Zimbabwe wanalala na njaa? eti fahari yako anayeleta njaa hiyo ni mtu mweusi mwenzetu!

Si ndio hayo hayo mtu kule kwetu anatuingiza kwenye mikataba ya kutuua na watu wanafurahia kisa aliyefanya hivyo mwenzetu? Mimi bwana realistic kama mtu anaweza kutuendeleza tukasoma tukapata ajira na kuwa na maisha bora mimi nafuraia bila kujali rangi ya ngozi yake, na kama mtu anapora mchana kutwa ninakasirika na kuja juu hata kama huyu mtu ni mweusi mwenzangu.

Ushauri wa bure kuwashangilia washenzi eti kisa wana rangi nyeusi ya ngozi, upuuzi mtupu huu.

Halafu eti Mugabe ndie aliyeleta demokrasia Zimbabwe!? hivi unajua demokrasia wewe? kuna democrasia Zimbabwe?
 
FD,
Acha UPUUZI, huyu alikuwa BORA na bado ni bora hata akiwa amekufa kuliko MUGABE!
Kumbe unakubaliana na maneno ya Mbowe aliposema afadhali ya Mkoloni! Tena basi, Mbowe alikuwa very specific kwa kitu gani - HUJUMA YA UCHUMI.

Wanabodi, pleease!

Kama mlikuwa hamfahamu mateso ya Wazimbabwe weusi chini ya utawala wa Kaburu Ian Smith, bora kukaa kimya kabisa.

Propaganda nyingi zimesemwa, kama zilivyokuwa zikisemwa chini ya utawala wa Kaburu huko South Africa, eti tangu Mandela kaingia, ujambazi umekuwa kwa asilimia 100 na nchi sio salama tena. Bahati tu Mandela hakubeba uchafu kama wa Mugabe.

Mugabe ni kiongozi aliye wasaliti wananchi wake, lakini napokluja sikia watu mkisifia Ian Smith kwa sababu kuna baadhi ya vijana wa Kizombabwe waliozaliwa miaka ya 70 wakimsifia... What do they know really?

Guys, hivi kweli ni afadhali mtu kuwa jela penye uhakika wa chakula kuliko kuwa huru lakini huna chakula!...

I mean, tusijaribu kabisa kulinganisha washenzi wawili ambao wote wanaua kwa njia tofauti. Nilikuwa mmoja kati ya Watanzania wa kwanza kwenda Zimbabwe siku ya Uhuru wao, na sidhani kama kulikuwa na mweusi hata mmoja aliyekuwa na madaraka/cheo ama nafasi kuongoza sehemu yoyote ile. Kifupi, hakuna mweusi aliyeweza kushop ktk maduka yao, iwe kwa uwezo ama ruksa!

Acheni jamani, hata kama hapakuwa na Apartheid kama South Africa, lakini huyu mshenzi aliua Waafrika vibaya sana, na dharau yake kwa mtu mweusi huwezi kuipa kipimo hata kidogo. Tena inasikitisha zaidi sifa zinapotoka kwa weusi wenyewe!

Mugabe ni mshenzi, na tutamhukumu kwa mabaya yake, lakini sio kwa kulinganisha na Simba mla nyama mwingine!

Nakuombeni isomeni hotuba ya Mugabe - UN. Ondoeni picha ya nani kayasema, bali chukueni ukweli aliozungumzwa.
 
Mkandara hapa unatwist mambo, hakuna anayesema kuwa Smith alikuwa Mungu. Smith naye alikuwa na ushenzi wake. Alichokuwa akisema wakati ule kilikuwa na ukweli wake, japo hakukisema kwa njia inayostahili. Wazimbabwe wengi hawakuwa na uwezo wa kuchukua nchi na kuendeleza kama ilivyokuwa, na ukumbuke kuwa wakati ule ubaguzi wa rangi ulikuwa ni mtindo kwa watawala. Hakuna anayesema kuwa alikuwa sahihi kwa asilimia zote, na yeye naye alikuwa na ushenzi wake.

Lakini ukiangalia kipindi chake cha utawala cha miaka 15, na kipindi cha utawala cha Mugabe tangu nchi hiyo ipate uhuru, utaona tofauti kubwa. Usijidanganye na hotuba iliyosomwa na Mugabe kwenye UN. Mugabe amefilisika kisiasa na ana hofu kubwa ya kuhukumiwa anapoondoka madarakani, ndiyo maana anang'ang'ania madaraka.

Smith aliua watu takriban 30,000 kwenye mapambano na wafuasi wa Mugabe, wengi wao walikuwa Waafrika. Lakini Mugabe ameuua weusi wengi vilevile, karibu nusu ya idadi ya watu. Kwa maoni yangu, wote ni wauaji, lakini muuaji mmoja aliweza kuendeleza uchumi ambao uliwafaidi wote, weusi na weupe. Lakini uchumi wa sasa wa Mugabe unawanufaisha viongozi wenzake tu.

Mbowe alisema ni heri mkoloni, nadhani wakati wa ukoloni Watanganyika walikuwa na maisha bora kuliko sasa. Hata ukiangalia shule walizosoma, hospitali walizokwenda, na mishahara waliyopata Watanganyika wakati wa ukoloni, inaonesha kuwa kiuchumi walikuwa huru kutoka kwa serikali na umaskini kuliko sasa. Sasa hivi, Tanzania ina uhuru kutoka kwa utawala wa kisiasa, lakini uchumi unawanufaisha watu wachache sana. Kwa hiyo, Mbowe alikuwa na hoja, si mjinga. Ukumbuke anaongoza chama cha siasa, na waliomchagua hawakumchagua mjinga.
 
Bongolander,

Nadhani sijaelewa ujumbe wako vizuri. Unataka kufafanua nini? Nimesema wapi kwamba mnafananisha Ian Smith na Mungu? Je, unajua maana ya "Uungu" na jinsi neno hilo linavyotumiwa?

Ndugu yangu, maelezo yako yanadhihirisha wazi kuwa wewe ni kijana mdogo, kufikiri kuwa ubaguzi wa rangi ulikuwa mtindo ni jambo la kusikitisha zaidi, hasa kutoka kwa mtu mweusi. Kwa ufupi, ninajaribu kuwa kama mpatanishi wa hoja zinazotolewa hapa ili tuweze kuheshimu umuhimu wa jiji hili. Naomba radhi sana, lakini tafadhali kumbuka kuwa watu wa kila aina hufuatilia mazungumzo yanayofanyika hapa na wengine wanaweza kuamini kuwa tunawakilisha fikra zetu kikamilifu. Nia na madhumuni yangu ni kuhimiza watu kuwa makini kidogo, hasa linapokuja suala kama hili. Si lazima uchangie ikiwa huna uhakika na yaliyotokea zamani.

Labda nijieleze kwa ufupi, ni kwamba tunapojaribu kulinganisha mambo, ni bora zaidi kutumia mfano wa mema dhidi ya mabaya. Ian Smith hawezi kamwe kuwa mfano mzuri hata kidogo, ingawa tunakubaliana kuwa Mugabe ni kiongozi mbaya. Ni mambo gani mazuri ambayo Wazimbabwe walikuwa nayo? Je, ni hadithi zinazosimuliwa na vijana waliozaliwa miaka ya 70 baada ya Mugabe kuwa madarakani? Sasa labda tuseme hata mateso ya Mugabe ni mtindo kwa sababu ndivyo ninavyoona kwa viongozi wengi wa Kiafrika.

Ni ajabu jinsi watu weusi wanavyotafuta njia za kuupamba utumwa au ukoloni hadi kufikia hatua ya kubadilisha historia ili kuficha aibu zetu. Ukitembelea Zanzibar leo, mahali ambapo watumwa walikuwa wakiuzwa, wamebadilisha kabisa na eneo hilo sasa lina mmiliki Mzungu ambaye ameondoa minyororo na vitu vyote vinavyohusiana na historia ya utumwa. Na sisi kwa kiburi tunajivunia kuonyesha majumba ya Sultani na jinsi alivyotawala nchi yetu, lakini hatuzungumzii utumwa, kwa sababu tunahisi ni aibu na siyo fahari.

Nina uhakika kuwa ni wachache humu ndani wanaofahamu kuhusu Vita ya Majimaji, viongozi wetu wa jadi, na jinsi walivyopinga ukoloni. Lakini haya yote tumeyafukia na badala yake tumekumbatia zaidi mambo kama yale aliyofanya David Livingston.

Kwa mtazamo huo, je, kizazi kijacho kitakuwa na kumbukumbu gani isipokuwa kumtukana kila mtawala anayekuja na kusifia wakoloni?
 
Mkandara,

Al in all ila mi naona UWEZO wa kujitawala hatuna. Tuna matatizo mengi mnnoo!
 
FD,
Al in all ila mi naona UWEZO wa kujitawala hatuna. Tuna matatizo mengi mnnoo!
Nimekuelewa vizuri sana hapo kama hutatumia mfano ule pale nyuma. Kifupi kilichotufanmya kuombe Uhuru wetu ni kuondokana na Kutawaliwa, iwe na mzungu ama mtu mweusi lakini kwa bahati mbaya viongozi na wanasiasa wetu wametaka kuchukua pale alipoachia Mkoloni, Leadership kwao ni RULE... hakuna kabisa nafasi ya rule of law.
Hata hivyo bado nina matumaini na kizazi hiki kipya ikiwa wataweza kuipokea historia yetu na kuitazama mapungufu yake kisha kutafuta ufumbuzi badala ya kufungiwa elimu ktk pakacha bila kufahamu kilichomo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…