Ex-soldiers na elimu yetu ya Tanzania

Ex-soldiers na elimu yetu ya Tanzania

GAS STATE

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2017
Posts
1,770
Reaction score
954
Asalam wakuu

Kwa wale waliobahatika kusoma elimu ya sekondari nchini mwetu kuna somo moja la historia, ndani yake kuna sura moja maarufu ya harakati za kudai uhuru barani Afrika ikiwemo Tanzania/Tanganyika.

Harakati hizi zilichochewa na sababu kadhaa za ndani ya nchi na nje ya nchi, mojawapo ni juhudi za askari wa zamani waliopigana vita kuu II ya dunia(EX-SOLDIERS).

Wanahistoria wanaamini kuwa askari hawa wa zamani walichochea harakati za kudai uhuru barani na katika nchi zao kama vile

i) Undwaji wa vyama vya ukombozi
ii) Kuwaaminisha wenzao kuwa wazungu hawana lolote wanakufa kama wao
iii) Michango ya kipesa katika kuendeleza harakati
iv) Kuwaaminisha wenzao juu ya uchumi wa ulaya unaojengwa kwa kuwanyonya waafrika hatimaye harakati zilipamba moto na uhuru kupatikana.

KINACHONISIKITISHA

Historia yote ya sekondari juu ya askari hawa hakuna kitabu wala mwandishi yeyote aliyetaja majina ya askari hawa mbaya zaidi waandishi wa Tanzania nao wameshindwa kumtaja huyu mtu ABDULWAHID SYKES kuwa ni miongoni mwao na alifanya makubwa juu ya uhuru. SYKES alikuwa ni

a/ Kiongozi wa TAA
b/ Katibu mkuu wa TANU
c/ Mjumbe wa kamati kuu TANU
d/ Mfadhili wa TANU

Pia ni askari aliepigana vita kuu ya dunia, baada ya kurudi ndipo kudai uhuru kulianza. najiulliza JE
-Wanahistoria wa Taifa hili hawamjuwi huyu afande?
Kama wanamjuwa kwanini hawekwi kama mfano ili wanafunzi wamjuwe? hakuna mwanafunzi wa sekondari ambaye ukimuliza mfano wa ex soldier anaweza kukupa. HAYUPO.
-wanamjuwa lakini hawataki atajwe? maana hakuna kitabu cha sekondari kinachomtaja huyu katibu kama kipo kitaje nikanunue leoleo

Point hii ilinipa wakati mgumu kwani sikuwa na mfano wake na kwa moyo wa dhati natoa shukrani za dhati kwa MOHAMED SAID kwa kutujuza mfano wake.
Elimu tunayopewa mashuleni ina mapungufu mengi mno ila huenda ndio mkakati wao wanafunzi wasijuwe lakini je ina tija?

akhsante MO SAID kwa kututoa tongotongo za ex soldiers
 
Yote hayo yalifanyiwa mikakati makusudi kidogo kidogo kuyafuta na kuyaondoa ktk historia ya Tanganganyika si Ex solders tu hata akina Mirambo .Mkwawa , na akina Kidawe machief hawa, vita ya Majimaji vyote hivyo ilikuwa ni chimbuko la kudai uhuru na kukataa kutawaliwa lakini vimefutwa ktk history ya nchi hii. Kwanini? uko mkakati maalumu toka serikali ya julius kambarage, kuwa kizazi cha watanganyika watakao kuja baadaye wamtukuze na kumuenzi Juliasi k. Nyerere kama yeye ndie chimbuko la uhuru wa Tanganyika na baadaye kupewa UTAKATIFU. na UBABA wa Taifa,
 
Back
Top Bottom