MINOCYCLINE
JF-Expert Member
- Apr 2, 2015
- 8,018
- 16,802
Ikumbukwe kuwa akiwa anaongea na Kipindi cha Michezo cha Wasafi FM na hata kile cha EFM Boss huyu kutoka Kampuni ya GSM inayoifadhili kwa Kuinyonya Kimapato Klabu ya Yanga Injinia Hersi alisikika akisema tena kwa Kujiamini kabisa kuwa kwa 100% Yanga SC inaenda kuwa Bingwa wa 2020/2021 VPL na isipotokea hivyo aulizwe na alaumiwe Yeye kwani walisajili Kiufundi.
Taarifa za ndani kabisa ambazo Mwandishi All - Rounder huwa ni rahisi Kuzipata kutokana na Mbinu zake zisizoshindikana za Kiuweledi zinasema kwamba tayari Mtoa Ahadi na Mbebwa katika Kiti cha Kifalme Uwanja wa Ndege JNIA Injinia Hersi kuona hilo halitowezekana tena hasa kutokana na Mwenendo mbovu wa Yanga SC na Simba SC inavyokuja kwa Moto amelipanga hili ghafla.
Muda wowote ule kuanzia sasa mtasikia baadhi ya Wanachama (hasa Makomandoo) wa Yanga SC ambao Injinia Hersi mwenyewe na GSM yake anawamudu kwakuwa huwa anawapa Pesa na Kuwasafirisha popote kule na Timu yao wataanza Kuzungumza katika Media na Mitandao mbalimbali kuwa Mwenyekiti Msola na Kocha Msaidizi Nizar Khalfan ni Mamluki na Mashabiki wa Simba SC.
Kutokana na Umasikini wa Pesa uliopo sasa Yanga SC huku GSM ikiachiwa na Uongozi wa Yanga SC kufanya hadi Kuratibu Kazi zote za Kiutendaji kwa Maelekezo yao hili la Injinia Hersi litafanikiwa na hawa Wawili (Mwenyekiti Msola na Kocha Msaidizi Nizar) watafukuzwa kisha Injinia Hersi atawazuga wana Yanga SC (ambao wengi wao uelewa wao ni hafifu) kuwa Ahadi yake iliharibiwa na Mamluki hawa Tajwa wawili hivyo wamvumilie na Msimu ujao Yanga SC itakuwa Bingwa iwe isiwe.
Hongereni GSM kwa Kuuza Jezi zenu na Kurudisha Pesa zenu na hadi kupata Faida hivyo sasa wala hamna tena Mpango wa Kuhangaika na Yanga SC ndiyo maana hata Mishahara ya Wachezaji mnawapa wale tu mliowasahili nyie (ambao 99% yao ni Majeruhi na Wabovu) huku wale Wachezaji Wazawa wa Yanga SC mkiwabagua katika kuwapa Stahiki zao na sasa wamesusa.
Polisi Tanzania tafadhalini msituangushe nanyi Kesho. Fanyeni kama Coastal Union walivyofanya ili Jangwani Moto uwake zaidi sana.
Kazi ipo!