Exclusive: Jay Dee afunguka, atoa sababu za kuitosa ndoa yake

Heaven on Earth

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2013
Posts
37,226
Reaction score
26,687
NO: 10

SWALI: Tunasikia umeachana na mume ni kweli au uzushi?

JIBU : Hatujaachana niliamua kumuacha

SWALI: Kwanini umeachana/umemuacha mume?

JIBU : Nimemuacha kutokana na kuwa Ndoa inatakiwa iwe na maelewano, furaha, amani na upendo, ila kwa bahati mbaya vyote hivyo havikuwepo, sikuwa tayari kuendelea kuishi kwa maumivu huku niki pretend ili kuiridhisha jamii.

SWALI: Huoni kama umejishushia heshma kuachana na mume?

JIBU : Sioni hivyo, ila naona nilikuwa najishushia heshima zaidi kuishi na mume asie na heshima, anaeweza kutongoza na kushika wanawake makalio wakati mi niko jukwaani naimba. Kuwapa mademu magari yangu waendeshe na kuyagonga wakati niko safarini.

Ukiachilia mbali vipigo. Kutembea na wahudumu wa restaurant yangu. Ushahidi ninao; niliwahi mkuta anawashika mapaja na akakiri kosa. Bado kupigana na kuwatusi wateja pia. Kifupi ilikuwa ni ndoa ya mateso!

SWALI: Baada ya kuachana unategemea kuolewa tena?

JIBU : Ni mapema kujihakikishia uolewaji mwingine, ila haimaanishi kuwa sitopenda tena. Nahitaji kuwa makini zaidi Kuchagua mtu sahihi wa kumpa moyo wangu.

SWALI: Kwanini usirudiane na mumeo?

JIBU : Siwezi kurudi nyuma tena, huwa nina misimamo thabiti. Mpaka kuamua kuondoka na uvumilivu nilionao mjue ni maji ya shingo. When i say never, I mean Never.

SWALI: Uliwezaje kuishi na mume mlevi namna ile?

JIBU : Nilidhani angebadilika, so nilikuwa natoa nafasi. Iliposhindikana nikaona isiwe tabu, kila mtu na aubebe mzigo wake. Ukizingatia ananizidi umri miaka mingi, alitakiwa yeye anielekeze zaidi kuliko mimi kumuelekeza maisha mtu mzima.

SWALI: Uliwezaje kuondoka?

JIBU : Nilipoamua kuwa na iwe basi, Nilitoka bila kubeba kitu. Nikasafiri kwenda USA, nikakaa huko mwezi mzima ku refresh na kujipima kama kweli ntaweza ku move on? Niliporudi Tanzania sikukanyaga tena nyumbani, mpaka muda huu nnapo type na ku post haya majibu. Kwa ki fupi ni kuwa nili ondoka bila kuaga, sikuona sababu ya kuaga.

Asanteni jamani, nafikiri nimejibu yote.
 
Matokeo ya kutumia pesa kupata wanaume ndo haya. Gadna roho yake ilikuwa kwa Fauzia, secretary wa
Joseph Kusaga. Gadna pale alikuwa kafa kaoza and it was real love sababu Gadna hakuwa na kitu na
Fauzia alikuwa kasecretary tu.

Akaja Jide na mihela yake pakawa hapakaliki. Gadna akamwacha Fauzia akaenda kwa jide coz of money but
after few months akaona hawezi ishi bila Fauzia akarudi tena kwa Fauzia
wakaendelea na mapenzi yao ya kimaskini.

After few months akaona mapenzi bila hela sio matamu sana akaona bora aende kwenye hela akarudi tena kwa Jide.

Hapa naongelea around 2002 hivi jamani.
Clouds fm palikuwa hapakaliki ni machozi na ngumi tu. Jide alikuwa akimuona Gadna na fauzia analia mpaka kamasi zinamtoka tena mbele
za watu na akipata mwanya
anamrukia Fauzia anamchapa kama kamzaa kisa Gadna.

Gadna alikuwa anashindwa kuwa na uamuzi maana
one side kuna pesa, the other side ndo roho yake ilipo. Kuna siku nakumbuka enzi za Blue palms Jide alimkuta Gadna na Fauzi hapo, Gadna akawa anajifanya kama hamuoni Jide
vile yupo busy na malovey dovey na Fauzia. Jide aliangua kilio mbele za watu kama kafiwa tena kipindi hiko ndio video ya machozi aliyo act
Frank Gonga imetoka.
akawa anamtuliza Jide asianzishe vagi, for some reason Jide akamsilikiza Frank sababu ni Mkurya mwenzie. Jide kateseka na Gadna
even before ndoa,

toka wanadate ilikuwa ni relationship ya mateso ila
aliamua kung’ang’ana na kumuhonga Gadna. Like always, in the end money
won and Gadna married JIDE.
Problem is he never fell in love with her alikuwa pale kimaslahi na alikuwa anawaambia watu hana stimu kabisa na Jide ndo maana alikuwa anatia tia nje kila siku.


Lesson to learn today: money cant buy you love. Happy Valentines wana Jf
 
It is crapy, action and reaction are equal and opposite yeye sia alimchukuwa mwanaume wa mwanamke mwenzie. Hana lolote yeye alivyo jiona ana fame akamuona bwana wake hana lolote na kumng'ang'ania mwanaume wa mwanamke wa mwenzake sasa anajifanya kwamba mwanaume ndio tatizo hata yeye pia tatizo. Kwanza hayo ni maneno ya upande wake anajitetea uweanda akiitwa mwanaume apo ata umbuka. Pia ujinga kusema kwa watu swala la mapenzi baada ya kuachana mbona hakusema wakati wa mapenzi motomoto
 
Haaaaaa bora umpigie asije kuwa harudi kimoja.... na wewe ni kicheche kama Gardner Lol

No, sio kicheche lakini haka ka style ka wanawake kuondoka ka wanaenda sokoni vile kumbe ndo harudi tena na huku kufunguka namna hii katatuweka wanaume kwenye wakati mgumu sana mwaka huu.

sababu kuna uzi mwingine na flora mbasha ye aliondoka na elfu mbili tu,kama yupo vile, kumbe huyoooooooo mpaka leo
 

Pamoja na yote Jide hana furaha.
 
kweli ndoa zinazidi kuwa ngumu kiasi hiki...
 
Alitoa wasaa wa fans wake kwenye page yake ya insta siku ya jumapili, akawa anajibu machache machache Yalikua maswali 10 na hili ndio lilikua swali lake la mwisho

Okay..Amefanya poa , ila mimi sijaipenda kabisa hii kitu alivyoiprizent .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…