Exclusive: Jay Dee afunguka, atoa sababu za kuitosa ndoa yake

mpwa mna valentine sie tuna after valentine

Wapi ndugu yangu! Sie tumebaki kuwaangalia vijana na valentine zao. More than two decade sio mchezo mkuu,hizo hekaheka tumezipitia na kuziacha sasa twasonga mbele.
 
Nimepitia kwenye account yake G kusoma comment daaa aisee nimeona watu wanamponda sana hadi nimesikia huruma!

Na wao tayari washatengeneza team...hao wanaoponda ni team komando bila shaka..kwa kubase na stori ya upande mmoja ndo wanasema maneno yote..
 

Una ubuyu mtamu! kama potential buy! cc:mimi
 

Yaah nakubaliana na wewe niliangalia kile kipindi jamaa alionyesha ukomavu wa hari ya juu sana. Hata kama walikuwa na matatizo yao lkn jalijitahidi kutunza siri za mahusiano yao au migogoro ya ndoa yao. lkn ukihijiwa unafula na kutohoa kila kitu ni jinsi gani unaonyesha uchanga, uzuri wa G hajajibu mpaka sasa yote anayoongea Jide huu ni ukomavu tosha. hata dogo dimond ananifurahisha anpokuwa haongelei swala lake na wema he is just focusing on his new relationship with zari.
Hamna haja ya kuongeleana vibaya wakati mlikuwa na good time some moment.!
Heaven on Earth nakutafuta: staturday Naja takwimu.
 
Yaani kamkomalia komando wetu mpaka bhasi....
Kuna jamaa yangu huwa anasema jide ndo msanii photogenic kuliko wote wakike,sasa Natalia ukisikiwa na huyo rafiki yangu sijui tu hahaha

Sura Yake Kama Nanasi( pineapple ) try to decorate pineapple .Akipaka make up its worse .ushawahi ona ako smile na selfie photo.Hizo pesa baadala ya kuwahonga wanaume achukue pesa abadilishe structure ya forehead na pua Yake isogezwe.she is ugly period
 
Last edited by a moderator:

Huyo ndo Pdidy... kataa kubali ni uandishi mahiri na wa kipekee humu Jf...
 

Wewe nimekushindwa....ila bora hujawa mnafki kwa hilo
 

taratibu tu utamuelewa........ huyo ndio Pdidy
 
Last edited by a moderator:
Mpwanimemjibu huyu pengine elimuyangu ukoowaowote wajumlishe namimbailiotumboni awana!!!else wako 2-4

hahaaaaaaa Mpwa mbavu zangu....... elimu yake ukoo wote hawana mie si nimemwambia

Mpwa sikuja Calabash niliamua kulala tu
 
mengine ongeza akiliyakonawwewee

Ni kweli lakini tambua kwamba "clarity of sentenses removes the barrier to communication!"; unapost thread ili watu wakusome na wakuelewe; dont do it for the sake of doing it; do it well; Ni ushauri tu ambao sio ushawishi mwenzangu; wala usijisikie vibaya.
 
Mpwanimemjibu huyu pengine elimuyangu ukoowaowote wajumlishe namimbailiotumboni awana!!!else wako 2-4

Mwenye elimu siku zote huwa anajiona hana elimu na anahitaji kujifunza na yupo tayari kukosolewa akajifunza zaidi???
Pdidy nafikiri elimu uliyonayo ni tofauti na hii tuliyoletewa na wakoloni🙄
 
Last edited by a moderator:
Pamoja mkuu MTK
Ombilitajadiliwa kwaufanisizaidi mpwa
 
Reactions: MTK
Mwenye elimu siku zote huwa anajiona hana elimu na anahitaji kujifunza na yupo tayari kukosolewa akajifunza zaidi???
Pdidy nafikiri elimu uliyonayo ni tofauti na hii tuliyoletewa na wakoloni🙄
Mpwa manenoyangu usiyachukulie serous ssana asilimia 80. Kufurahisha jukwaa ndoazao zisitengemae
 
Samahani Mkuu BIGU kama nimekuudhi usotoeshillingi nkapewa ban!!!m nimmoja wanaopenda kukosolewa sana else ningekuwa naban alfukumi!!huoni kila anaejisikiakumwandika pdidy anaruhusiwa na angalia kamanishawahi kumjibu MTU ovyo!!nanikijua nimemkosea mtuhumu amriyangu yakwanzaa nimsamahaa mpwa!!usihofu nozoeee mdogomdogo
 
Pdidy@naona Vidole vyako vinamatege hebu vipeleke nikafanyiwe wheel alignment
 
ADVERTISEMENT
Dar es Salaam. Mwanamuziki nyota wa kike nchini, Lady Jaydee jana aliamua kuwaburudisha mashabiki wake kwa staili ya kipekee; kuzungumzia kuvunjika kwa ndoa yake na Gadner Habash.

Kwa muda mrefu kumekuwa na minong’ono kuwa wawili hao wametengana, lakini hakuna aliyekuwa tayari kuweka wazi kuhusu suala hilo.

Hata hivyo, jana, Jaydee, ambaye jina lake halisi ni Judith Wambura aliamua kutoa ya moyoni, akisema kuwa kwa sasa ametengana rasmi na mtangazaji wa kituo cha redio cha E-fm cha jijini Dar es Salaam.

Jaydee ambaye wakati mwingine huitwa ‘Jide’, kwa wiki moja sasa ameamua kujibu maswali mbalimbali kutoka kwa mashabiki wake kwenye mitandao ya kijamii.

Kati ya maswali aliyoulizwa na mashabiki wake ni kama ni kweli ametengana na mumewe na ni sababu za kutengana.

Kupitia ukurasa wake wa instagram, mwanadada huyo alisema: “Nimemvumilia vya kutosha, kuhusiana na tabia zisizokuwa na nidhamu wala heshima ya ndoa na sasa imefika kikomo.”

Msanii huyo anayemiliki Machozi Band, alibadili picha ya wasifu ya mtandao huo na kuweka jicho linalotoa machozi na kidole kikivuja damu.

Alisema kuwa yeye na Gadner hawajaachana kama ambavyo watu wanasema isipokuwa yeye ndiye aliyeamua kumuacha mwanamume huyo.

Hata hivyo, alipotafutwa kuzungumzia suala hilo, Gadner alisema: “Sina comment katika hilo.”

Aliongeza kusema: “Aliyezungumza ni mtu mzima na amefanya juhudi kuzungumza alichozungumza. Ku-comment kwa kupinga au kukubali ni kuzidharau juhudi zake.”

Meneja wa mwanamuziki huyo maarufu kama Rapa Wakazi, alisema kuwa kilichozungumzwa na kuandikwa na mwanamuziki huyo ni kati ya mwimbaji huyo na mashabiki wake, hivyo hakuna cha kuongeza.

Meneja huyo alisema ingawa mwanamuziki huyo hakuhusisha uongozi wakati anaandika, lakini hayo ni mawazo yake na yabaki kuwa hivyo.

Wakati Habash akisema hayo, Jide aliamua kufunguka na kusisitiza kuwa hatarudi nyuma kwa uamuzi aliouchukua. Na hii ni sehemu ya majibu yake:

Swali: Tumesikia umeachana na mumeo kweli au si kweli?

Jide: Hatujaachana, nimemuacha.

Swali: Kwa nini umeachana/ umemuacha mumeo?

Jide: Nimeamua kutokana na kuwa ndoa inatakiwa iwe na maelewano, furaha, amani na upendo… ila kwa bahati mbaya vyote hivyo havikuwepo, sikuwa tayari kuendelea kuishi kwa maumivu huku nikipretend (kwa maigizo), ili kuridhisha jamii.

Swali: Huoni kama umejishushia heshima kuachana na mumeo?

Jide: Sioni hivyo ila naona nilikuwa najishushia heshima zaidi kuishi na mume asiye na heshima… amekuwa akiwapa mademu (vimada) magari yangu na kuyagonga wakati nipo safari, ukiachilia mbali vipigo. Kifupi ilikuwa ndoa ya mateso.

Swali: Baada ya kuachana unatarajia kuolewa tena?

Jide: Ni mapema kujihakikishia kuolewa na mwingine, ila haimaanishi kuwa sitopenda tena. Nahitaji kuwa makini zaidi kuchagua mtu sahihi wa kumpa moyo wangu.

Swali: Uliwezaje kuishi na mume mlevi namna ile?

Jide: Nilidhani angebadilika, nilikuwa natoa nafasi, iliposhindikana nikaona isiwe tabu, kila mtu aubebe mzigo wake. Ukizingatia ananizidi umri miaka mingi, alitakiwa yeye anielekeze zaidi kuliko mimi kumwelekeza maisha mtu mzima.

Swali: Uliwezaje kuondoka?

Jide: Nilipoamua iwe basi, niliondoka bila kubeba kitu, nikasafiri kwenda Marekani, nikakaa huko mwezi mzima kurefresh (kujiliwaza) na kujipima kama ninaweza kumove on (kuendelea)? Niliporudi Tanzania sikukanyaga tena nyumbani mpaka muda huu ninatype (kuandika) na kupost (kutuma) majibu haya.

Kwa kifupi niliondoka bila kuaga sikuona sababu ya kuaga. Ahsanteni jamani, nafikiri nimejibu yote.

Jay Dee alichomoza kwenye anga za muziki baada ya kurudia kibao cha mwanamuziki nguli, Marijani Shabani cha “Zuwena” ambacho kilimpa umaarufu mkubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…