Exclusive: TANESCO's Audited Report from PPRA

Kuna maswali mengi sana kuhusiana na Richmond kwenye hii document. Kwanzia page ya 40. Very very Interesting. Sijui ndio maana lowasa akashtuka?
 
Tender
PC/10/2006 for Emergency Power Supply from rental Gas Based Generating Plant of 100MW


Summary of issues in the tender

 
sina space kwenye comp. yangu ! haya nitadaunlodi hivyo hivyo mkuu !
 
Nilikuwa najiuliza kwa nini TANESCO iko taabani, sasa nina jibu?

Sasa, Wataalamu NetGroup walikuwa wakifanya nini kipindi hicho, maana complication zote ninauhakika waliziweka wao, Wabongo najua wazuri sana kuweka at least process and procedures kwenye makampuni?

Mimi Nashukuru kwa Report, maana ni Mwanzo Mzuri, ukijua tatizo ndio nusu ya kulitatua....
 
Tanzania yangu ... inaliwa na wajanja wachache wenye meno huku waksha hoi wakizidi kuliwa na kuumia. Kweli mwenye nacho huongezewa na asiye nacho huporwa hata kile kidogo alicho nacho!
 
Wazungu wa Net Group walisema, "Hivi Watanzania muna akili kweli?" kauli hiyo ikamponza Mzungu wa watu akaondolewa nchini. Hebu fikiria, mzungu anatetea maslahi yenu munamtimua wakati ule akiwa anaharibu mulimlinda kwa FFU. kazi kwelikweli
 
Halisi, kuna wenzetu ambao ati kwa vile mkoloni ni mweusi basi ni bora zaidi kuliko mzalendo mweupe!!
 
Anytime bro. Karibu

Ahsante sana invicible. Nilikuwa sioni muziki basi nikaenda kwenye search nikaingiza ASAP mambo yakajipa. Sasa itakuwa vizuri kama tutaupata muziki wa Mkapa na Yona kujipatia Kiwira na Muziki kati ya Mkapa/Yona na Tanesco.
 
mbona something is missing or its just me... Dowans walinunua mkataba wa RDC kwa kiasi gani?
 
patamu hapo.... Naendela kusoma hii braking news, sababu when the news brake out we brake in.

Duh...!! kaaazi kweli kweli, lakini tutafika tu. Naona kamgao ka kasungura ka Lowasa kaendela kwa mwendo mdundo. Ka sungura haka naona kameombewa dua, maana hakaishi na mgao bado unaendela......nani alisema lazima iwe ng'ombe!!!?.
 
Jamani PCCB wanaweza kutuambia ule upuuzi wao wa kuisafisha RDC waliupata wapi? Sasa hii si aibu kubwa sana kwa huyu bwana Hosea na timu yake? Kweli hii nchi kazi bado ipo! Kila mahali pameoza. I wish kama kunauwezekano Invicible tupatie na hiyo ripoti ya PCCB pia tuione.
 
Hahaha, watu mnanifurahisha. Ina maana mshaisoma yote hii kitu? Mbona wengine huwa wanadondoka sahihi mambo flani bila kuumiza vichwa?

Yangu mie macho
Invisible

Hii kitu niliisoma ndani ya dakika 80, nilibebaba laptop yangu na kujifungia board room, sikutaka kusubiri, nilipo fika page ya 30 nilipata kizungu zungu

kumbe ile tabia ya kukimbizana na mikata kwenye mikoba ya haikuanzia buzwagi


Kazi kweli kweli, siku yao inakuja tena yaja upesi..........siku hiyo fisadi ataitwa fisidi
 
Hii kitu nimesha isoma yote, it took me the whole day kuangalia, from excutive summary to last dot.

Wakubwa I hope mtamaliza sasa tuanze kumchambua huyu sungura.
 
Maumivu Haya ni Makali,Ewe Mola Wetu Tuhurumie!

KNKCU,

Pole sana mkuu. Long time sijakuona online na mkuu Yebo Yebo. Mlikuwa mkililia kupata madude kama haya na sasa mnayapata na mtu unajikuta unachoka pale unapoujua ukweli.

Inshallah, Mwenyezi Mungu atasaidia na mambo yataenda sawa endapo watanzania tutasaidia katika kutoa mapendekezo juu ya namna ya kuendesha nchi yetu tuipendayo - Tanzania.

Karibu
 
Nashukuru!
Dunia na Tabu Zake ndiyo inaninyima muda Lakini tunaomba Uzima Ipo siku Nchi itarudi mikononi mwa Viongozi wa Nyonge na si kwa Viongozi wa Vibepari uchwara. Na Masilahi ya Taifa ndiyo yatatawala maamuzi na Fikra zetu!
 
Invisible,
Shukrani DJ wetu kwa kutuporomoshea kibao kingine latest...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…