Exclusive: Tevez afunguka alivyoteswa, kudhalilishwa

Exclusive: Tevez afunguka alivyoteswa, kudhalilishwa

Hussein Massanza

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
1,016
Reaction score
2,195
EXCLUSIVE! Kile kisa cha mtalaka wa mwimba taarab mahiri Bongo, Aisha Ramadhani Nkongo ‘Isha Mashauzi', Jumanne Hassan ‘Tevez' kuteswa na kudhalilishwa nchini Afrika Kusini kisa kikidaiwa ni kudhulumu mzigo wa wafanyabiashara wenzake kimeingia awamu nyingine!

Kwa mara ya kwanza Gazeti Pendwa la Amani Tanzania limeweza kuzungumza na Tevez kwa dakika arobaini na tano kutokea nchini humo ambako anauguza majeraha.

KWANZA SIKU YA TUKIO

Kabla Tevez hajasimulia kilichompata na hali yake kwa sasa, ni muhimu kukumbuka kuwa, tukio hilo ambalo lilikuwa habari ya Jiji la Dar es Salaam, lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo picha zake zilizagaa zikimuonesha akiwa amefungwa kamba huku mwili wake ukiwa umetapakaa damu na majeraha kadhaa.


AMANI LAMSAKA

Kwa vile habari za tukio hilo ziliandikwa na baadhi ya vyombo vya habari bila kupata balansi (uwiano) na Tevez mwenyewe, Amani liliingia kazini kumsaka mhanga huyo usiku na mchana.


MSIKIE SASA

Akizungumza kwa hisia kali na gazeti hili juzi, Februari 3, mwaka huu kutoka Mji wa Durban, Afrika Kusini, Tevez alisema:

"Kusema ukweli tukio lililonikuta watu huko nyumbani (Bongo) wanalitafsiri tofauti sana. Nimesikia kwamba wanasema eti nilidhulumu mzigo wa mtu, ndiyo maana niliteswa! Si kweli."


‘Tevez' akiwa salama nyumbani kwake.
UKWELI NI UPI?

"Ishu iko hivi, mwenyeji wangu hapa Durban, anaitwa Ibra, ndiye ambaye alinipokea siku nilipotua hapa.
"Huyu bwana inaonekana ni tamaa. Aliniundia njama, aliita wenzake na kuniteka kisha kunitesa sana wakidhani nina pesa nyingi.

"Niliteswa sana kwa kweli. Kama mlivyoona picha. Nilidhalilishwa sana, lakini katika yote ukweli sijadhulumu mzigo wa mtu."


ULICHOPOTEZA KATIKA UTESWAJI

"Katika mateso yangu, walifanikiwa kunipora Dola za Marekani elfu 14 (kama shilingi milioni 22) na Randi za Afrika Kusini elfu 3 (shilingi 480,000) zikiwemo simu zangu mbili aina ya Samsung na Nokia ambazo nilikuwa nazitumia sana kuwasiliana na watu wangu muhimu."


HAIKUWA KAZI RAHISI

Tevez akazungumzia jinsi jamaa walivyomkamata: "Jamaa siku wananiteka usiku kiukweli nilipambana nao sana hadi wanafikia hatua ya kunizidi nguvu na kunifunga kamba. Nilikuwa nimewachapa kwelikweli ila kwa vile walikuwa wengi na walikuwa wakitumia silaha nilijikuta nikiishiwa nguvu baada ya kunipiga na kitu kizito kichwani nikapoteza fahamu, nilipojitambua ndiyo nikakuta wamenifunga kamba."


KINACHOKUUMA NINI?

"Tukio linaloniuma zaidi ni yule jamaa ambaye anaonekana katika picha amekaa jirani na mimi, hana shati. Alinichoma pasi mgongoni, namchukia sana lakini nimemwachia Mungu."


‘Tevez' akiwa na mwanaye.

KUHUSU KUKATWA NYETI, KUFANYIWA KITU MBAYA

Tevez: "Nasikia watu huko Tanzania wanazusha eti nimekatwa nyeti, si kweli kabisa. Mimi nimepigwa na kuchomwa pasi wala hakuna kitu kama hicho zaidi ya kunichoma na pasi.
"Nimesikia wengine wanasema nimetobolewa macho, huo ni uzushi wa watu tu! Mimi niko safi na hali yangu ya kiafya inaendelea vizuri."


SABA WAMEKAMATWA

Tevez tena: "Nashukuru sana serikali ya huku wameweza kunisaidia kwani mpaka sasa ninapoongea na wewe Musa Mateja hawa jamaa wamekamatwa saba.

"Jana (Jumatatu) walifikishwa mahakamani na kusomewa mashitaka ya kunishambulia na kupora fedha. Wanatarajiwa kurejea tena mahakamani baada ya siku 7, ingawa nimeambiwa kesho (jana Jumatano) wataletwa Polisi Central ya huku kwa ajili ya mimi kuwatambua zaidi."


BONGO LINI TEVEZ?

"Bongo natarajia kurudi Alhamisi (leo) au Ijumaa (kesho) kama mambo yangu yatakuwa kwenye mstari ila pia sasa hivi natarajia kuwasiliana na balozi wetu ili nijue kama ana taarifa zangu na namna ambavyo ataweza kunisaidia kama kiongozi wangu."

HALI YAKO KWA SASA

"Kusema ukweli naendelea vizuri ni majeraha tu ambayo hata hivyo yanakauka. Ila hili la pasi mgongoni ndiyo linasumbua kwa mbali, lakini naamini litakaa sawasawa."


Chanzo:
GPL
 
Mmh kwahiyo kipigo chootee hikoo na huo udhalilishwaji lengo ilikuwa ni kumpora pesa tu!!!?
:what:
 
Aisee unga unatoka bongo unaenda South Africa...yaonekana hapa bongo Kuna magodauni ya kuhifadhi sembe...mhhh kazi IPO...
 
Alivamiwa na vibaka kwa hiyo itakuwa
 
Kama nanihiii imesalimika hapo sawa! Hicho ndicho cha kustua!
 
kwani angekatwa angepona? unakufa fasta tu.

By the way kama watu wanakupora ...si wanachukua vyao tu? kukutesa kunahusikaje?

Huyu ni mzee wa sembe aache kuzuga hapa
 
Dola za Marekani elfu 14 (kama shilingi milioni 22) na Randi za Afrika Kusini elfu 3 (shilingi 480,000)
Unatembea na Cash kwenye Wallet ndani ya nchi ya watu lazima naye huyu jamaa ni mwizi!
 
uongo kabisa jamaa hajui ata kusema kusema uongo sasa kama kuna kese inaendelea unakuja kufanya nini bongo nani atatoa ushahidi.

huyu jamaa inabidi akamatwe airport .rafik zake wa karibu wanasema ni unga na mazingira yalijionyesha
 
Teves kwa Maelezo take ni alhamisi atarudi nchini sasa hizo picha kapiga akiwa wapi nyumbani au south Africa. Na aliyeweka kasema yupo nyumbani kwake
 
Teves wewe ni muongo. Walijuaje kama una hela zote hizo
 
Back
Top Bottom