EXIM BANK wameishiwa pesa? BOT chunguzeni uzani wa PESA wa Bank hii.

EXIM BANK wameishiwa pesa? BOT chunguzeni uzani wa PESA wa Bank hii.

saggy

Senior Member
Joined
Nov 12, 2008
Posts
153
Reaction score
70
Jana jumanne na Leo Jumatano wateja wa EXIM bank wanaotaka kuchukua Fedha zao ndani ya Bank wamekuwa wakizuriwa na wahudumu wa Bank katika matawi wawili ya katikati ya jiji la Dar es salaam kwa kizingizio cha matatizo ya Systema wakati huohuo wakiendelea KUPOKEA fedha za Wateja wanaotaka kuweka..

Jana nimeshuhudia wateja katika Tawi la Clocktower wakilandalanda bila matumaini baada ya kugomewa kuchukua PESA kwa kisingizo cha Systema,mteja Mmoja aliulizwa ni kwanini anataka kuchukua Pesa yote kwenye Akaunti yake na akaambiwa aje baadaye mchana.Mimi natoa wito wa mambo yafuatayo:-

1. Bank ya EXIM wauambie UMMA wa Tanzania kama Wamefilisika ili wananchi wasijepoteza Fedha zao ama lasivyo tutawashitaki kwa kushikiria Fedha zetu bila sababu ya msingi,matatizo ya System ni YENU wenyewe na si makosa ya Mteja.

2.BOT kupitia Kitengo cha Banking Supervisory kilichoko BOT fanyeni uchunguzi wa uzani wa Kifedha wa Bank hii ili kuokoa Fedha za Watanzania Masikini walioweka Visenti vyao EXIM Bank.

3.Nawaonya Bank ya EXIM Kwamba Hatua Kali za Kisheria zitachukuliwa na mimi mwenyewe nimeanza kuandaa Kesi ya madai ya TSH.50m Kwa ajili ya HASARA niliyopata kutokana na kuzungushwa kupewa Pesa Zangu.

Nawasilisha
 
Mi ndo nime-deposit vijisenti vyangu jana, mbona unanitisha?
 
washtaki hao wakome kujikomba kwa serikali ja wasanii maana najua watakuwa wamemkopa Mkullo kiasi kikubwa tu cha pesa.
 
Inaweza kuwa kweli ni tatizo la network. Mbona inatokeaga kwenye mabank makubwa pia?? Haiwezekani bank ifikie hali hio BOT wasijue haiwezekani. Kuna interbanking transaction(over night borrowing) za mabank wanaofanyaga treasury dep.
 
Nafikiri ni tatizo tu la sysytem. Hii benki imeonyesha mafanikio makubwa hivi karibuni mpaka ikaaminiwa na Wanorwegian kuipa pesa nyingi kwa ajili ya miradi mbalimbali. Pia wameendelea kufungua matawi mikoani kwa kasi kuonyesha kuwa pesa wanazo za kutosha. Pia Dar matawi yanaongezeka kila mara na hivi karibuni watafungua tawi Buguruni kama bado halijafunguliwa tayari. Na isitoshe hii benki ni mojawapo ya benki zenye wateja wengi wahindi ambao ndo wenye pesa nyingi hapo kwetu Bongo.
 
Duh, ntazimia nikose wa kunimwagia maji l.o.l
Yaani hili tatizo kwao limekuwa COMMON sasa, kuna kipindi nafikiri ni mwaka jana... walishindwa kutoa huduma karibu wiki nzima kwa hayo hayo mambo ya system. Jamani wasije potea na hivyo vibaru (vipesa) vyetu.. mi nawapenda tu coz hakunaga foleni
 
Back
Top Bottom