Katika hali ya ubora zaidi tunashauriwa mama mjamzito kufanya vipimo vya mawinbi sauti katika kila baada ya miezi mitatu.
Vipimo vya mawimbi sauti vya kisasa kabisa vina uwezo wa kujua ni kwa jinsi gani mtoto tumboni anavyoendelea ( ukuaji wa urefu, unene na uzito), mtoto amekaaje na jinsia yake, pia umri wa mtoto aliye tumboni kwa siku na wiki. Na hina uwezo wa kutambua lini mama mjamzito atajifungua
Sasa la mama mjamzito kujifungua inategemea na afya na tabia yake.
-Kama ana afya bora ataweza kujifungua katika makadirio ya siku zake za kujifumgua.
-Kama tabia yake ni kukaa tu kizembe, atachelewa kujifungua, kwani uchangamfu wa mama kwenye kufanya kazi na mazoezi vina mchango mkubwa sana kwenye kujifungua.