Experience ya ajabu. Hivi ndivyo nifanyavyo ninapopata Mshahara

Utaratibu wako ni mzuri kulingana na aina ya mke ambaye unaye na iwapo unamjua vizuri, hope unanielewa vizuri nikisema UNAMJUA VIZURIIII....kuna aina ya wanawake mwanzoni mtaishi kwa amani kabisa tena utaifurahia ndoa ila once amekutana na mashoga wa saluni, sokoni, vibarazani na social media magroup ya whatsapp wakamjaza ujinga basi imekula kwako.
Jana wakati nipo kwenye basi narudi home kuna mzee mmoja wa makamo alikua anaongea kwa uchungu kuwa ameishi na mkewe miaka 28 na alikua na mfumo kama wako, mke akaubajetia vizuri mshahara wake wakafanikiwa kujenga nyumba mbili moja wakaipangisha na gari ya familia ya kutembea tu, wana watoto wanne na wa kwanza ni wa kiume ana miaka 26. Sasa mwaka jana akaanza kupata habari kuwa mke wake anaburuzwa na jamaa mmoja ambaye alimuhonga laki sita jamaa kufatilia akapata ushahidi wote ikamuuma sana maana anadai uwezo wa kumpa hiyo hela mke wake anao ila sijui tamaa au nini, na kumbe mtoto wa tatu waliozaa wote sio wake ni wa mwanaume mwingine. Hapo mbaba wa watu kapelekwa mahakamani mwanamke anataka talaka na wagawane mali pasu pasu, jamaa anasema anampenda sana mke wake angepata mtu wa kumuweka chini mke wake na kumkumbusha walipotokea kwenye chumba kimoja cha kupanga hadi kumiliki mali za sasa basi akili ya mkewe ikirudi yupo tayari kumsamehe na kusahau yote... Sikukatishi tamaa ndugu ila awali itakuwa na manufaa ila guarantee ya siku za usoni inaweza kuwa ndogo
 
H
Wachache sana watakao kuelewa hapa....mimi na miaka 10 katika ndoa....uzoefu unaonyesha mfumo dume ndiyo sahihi ktk maisha ya ndoa....ndoa haitaji ushauri mwingi, ila haipendezi uwazi uwe mwingi kwa mwanamke hasa mambo yanayohusu mali na kipato....maneno yangu siyo msaafu wala biblia ivyo akili kumkichwa.
 
Binafsi nimekuelewa sana.
Uzunguuzungu sijui wanaita usawa kuna wakati vilitaka kunitokea puani maana mwenzangu alianza kuota pembe.

Nilirudi nyuma na kuanza upya ili safari iendelee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli kwa huu mtindo wa kuweka kipato mezani una kheri nyingi sana na baraka. Ila unachangamoto nyingi sana ambazo hata mimi siziwezi. Mke wangu utanisamehe kwa kutokukushirikisha kila nikipata mshara,lakini nikiishiwa huwa nakufuata sana hii hali siipangi mimi,inakuja tu yenyewe.
 
kuna jamaa aliishirikisha familia
Yeye,mke ,mtoto wa kiume na watoto wao wa kike wakakaa sebleni kupanga mipango ya familia,bajeti na mambo mengine.
mkuu wa kaya alipoanza tu kuintroduce mada yake
akakutana na bonge la tusi la nguoni toka kwa mke wake alaf mbele ya watoto wao

ilikuw aibu kubwa kwakweli

hawa wanawake akili zao wanazijua wenyewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mfumo dume ndio uliokulea ukakua mpaka nawewe umeoa na una familia. Huoni kama babaako alifanya jambo la kishujaa mkuu! Thats the major key bro!

Wacha watu waponde ila mwanamke sio mtu wa kumuamini kwa namna yeyote. Ukilijua hilo huwezi kuanika michongo yako yote kwake maana she might use that against you akakumaliza!
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ mumeo anakupenda sana ila he never knows women better! Siwezi kumlaumu,the one you love the most might turn to be your worst enemy!
 
Mnaowapa hizo hela wake zenu na muendelee tu ila mkae mkijua no matter how your wives love you for doing that siku source ya kipato ikitetereka aidha mkashindwa kutimiza hilo au kipato kikapungua hamtabaki salama, you will indeed suffer the consequences!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…