Experience ya kulelewa na mama wa kambo

Experience ya kulelewa na mama wa kambo

MtotoKautaka

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2018
Posts
373
Reaction score
895
Nawasalimu ninyi nyote, Mungu mkubwa nipo salama.

Nipo hapa leo kuwapa experience yangu niloipata kutoka kwenye kulelewa na mama wa kambo (step mother)

1. Ukiwa na akili darasani KUSHINDA watoto wake imekula kwako utateswa mpka ujute kuzaliwa.

2. Watoto wake wakiwa vikojozi hafu wewe hukojoi kitandani basi ndugu yangu wewe akhela yako utaanza kuniona hapahapa duniani

3. Ukiwa na nyota ya kupendwa na watu hasa wageni wanaokuja home kuwasalimia yani wakawa wanakupenda sana wewe over watoto wake mzee baba/bibi utakiona cha mtema kuni.

4. Ukiwa una adabu (siyo kiburi/mgumu) kazi unayo utageuzwa mtumwa

5. Ukiwa mtundu mtundu mwepesi kujua vitu kuzidi watoto wake ndugu yangu umeisha

6. Ukiwa una kipaji flani hafu watoto wake hawana let's say kucheza mziki au mpira hafu watotoze wakawa wapowapo tu basi utasema.

Vituko nilivyowahi kufanyiwa na sitovisahau

1. Nilitoka skul nina njaa kinoma hafu ilitakiwa nile fasta nirudi remedial, nilipofika home nikaambiwa hakuna msos nipike mwenyewe hafu watoto wake washakula na wapo skul. Skul hapakuwa mbali na home kwahyo watoto wake walikuwa wanatoroka lisaa kabla ya kutoka wanaenda wanakula then wanarud shule.

2. Siku moja nilikuwa naumwa, kanipa vidonge bila ya kula then kaondoka zake harusini home nilibak pekeangu wasingekuwa majirani ningekufa

3. Mama mzaz alinishonea shat la kitenge watoto wake wakalichukua wakalipaka mchuzi wa samak wakaenda kulipachika kwenye shimo la panya likaharibiwa na panya Kwa kutafunwa

4. Nilipewa zawadi kwa kuwa mwanafunz wa pili kwenye mitihani zile zawad zilipofika home kesho yake sokuziona tena na sikujua zilienda wapi

5. Mtoto wake mkubwa alinipiga na ubao akanichana lip ya juu, nikaona uvumilivu umenishinda nikachukuwa wembe nikamchana kwenye shavu nilipigwa nusu kuuwawa.

Ni mengi mengine ni ya ajabu nisingeweza kuyaweka bayana........

Uzi umeisha.
 
Umenikumbusha mbali sana,nilikua naishi kwa baba mkubwa mke wake alikua na mtt wa kiume huyu dogo alikua anipendi hata kidogo chakula tulikua tunakula kwa pamoja ila yeye hataki kukaa karibu na Mimi hata kidogo na ninapopamba mboga hyo sehem yeye hapambi ilikua ni shida sana!
Dogo alikua na matusi sana kijana navumilia TU.

Siku Moja likizo tukaenda nyumbani kwetu Kijiji huko Mkoa X huko ndyo kwetu na ni chimbuko la wazazi wetu na wazazi wangu wote wapo huko na mama alikua maejifungua kadogo 2000's. Sasa yule Dogo akajichanganya eti anampiga yule Dogo ambaye tulimkuta anatambaa sijui sababu ilikua ni nini aisee nilimzibua Kofi Moja matata sana Hadi vidole vikajichora kwenye shavu lake nafikiri ingelikua ni hichinkipindi Cha utandawazi angepiga picha na kumpigia simu mama yake na baba mkubwa sizani kama ningendelea kuishi dogo alikua kutwa mzima na alizila kula mchana nikajisemea kimeumana.

Tulivyorudi nikawa na wasi wasi lakini baada ya masiku kupitia dogo akawa anarudia Tena upuuzi wake bi mkubwa ambaye mama yake akaniambia huyu usimchekee mzibue kama ulivyomzibua mkiwa kwenu, nikajisemea moyoni kumbe habari zilifikaaa.

Hivi sasa dogo tunafanya kazi wilaya Moja na ananizamu kubwa sana juu yangu hakuhi kuniamkia kipindi Cha utototl wake alianza baada ya kuja kufanya kazi huku nilipo na nilimpokea vizuri sana Hadi hivi sasa humwambi kitu kibaya kinachonihusu na akakuamini Hadi Hadi wazazi wake alienda kumwambia kaka ni mtu mzuri sana.

Siku Moja baba mkubwa ananipogia simu mdogo wako anakusifu ulimpokea vizuri! Aisee hyo siku nilibwabwaja nilimchana Mzee kinoma!
Nilimuliza kwa kwa hyo mulikua na wasisi kwa nini huyu ni mdogo wangu au mlikua na wasiwasi kwa matendo mliyonitendea mnazani na Mimi nitarudisha kwa huyu dogo!?
Dingi akasema acha kukumbusha hayo yalishapita nitakupigia baadae. Hyo siku nilitema nyongo.
 
Hivi kwanini imezoeleka mama wa kambo ana roho mbaya?

Roho mbaya ni tabia ya mtu , kuna mama wa kambo wako poa kuliko hata mama wa kuzaa..

Kuna dogo baba yake alifariki na akaachwa na mama wa kambo , lakini alilelewa na yule mama kama mtoto wa kumzaa..

Akamsomesha na sasa ana maisha yake..
 
Dogo alidhani hautafika mbali
 
Hivi kwanini imezoeleka mama wa kambo ana roho mbaya?

Roho mbaya ni tabia ya mtu , kuna mama wa kambo wako poa kuliko hata mama wa kuzaa..

Kuna dogo baba yake alifariki na akaachwa na mama wa kambo , lakini alilelewa na yule mama kama mtoto wa kumzaa..

Akamsomesha na sasa ana maisha yake..
It's true lakin kwa upande wangu sikuwa na hiyo bahati
 
Back
Top Bottom