Experience yako ya kwanza shule ya boarding!

Fibanochi

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2018
Posts
476
Reaction score
1,018
-Je hy shule ilikua chaguo lako? Kwa maana uliichagua mwenyewe?
- ulikua na picha gani kichwani mwako kabla ya kufika hy shule?
-ulipelekwa na mzazi/mlezi au ulikomaa mwenyewe?

Habari wakuu, ni matumaini yangu mko poa let's chit chat kdg .....straight to the point.....me binafsi nilipata bahati ya kusoma shule ya bweni 5&6 miaka km 13 nyuma, ilikua ni ya wavulana kwa advance na mchanganyiko olevel....hii ni shule kongwe na maarufu ya serikali kwa upande wa kaskazini mwa Tanzania, inapatikana ktk Moshi vijijini, katika tarafa sjui kijiji cha Kibosho.....naizungumzia Umbwe high school au mti safi kama inavyojulikana. Basi bwana nakumbuka kuwa na furaha sana baada ya kupata Joining instr. Form inayoonesha kuwa nimechaguliwa hy shule, niliipenda kwa kuwa kuna ticha fln janki enzi hizo alikua akitupigia mapindi ya Geog pale maeneo ya mwenye zilipo tuit maarufu...alikua akiisifia shule hiyo( ofcourse yeye alipita hapo pia) kuwa ni shule bab kubwa, mazingira mazuri , taaluma iko vzr , social issues n.k! Basi na Mimi sikufanya hajizi wakati wa kujaza form zile waliziita TCM 9 kama sikosei, pia nilisukumwa kuiweka hiyo shule as my first choice sababu ya hali ya hewa na landscape nzr inayopambwa na freestanding mount in Africa, the only and one Mt. Kilimanjaro , huwa napenda mazingira haya, mana hujihisi nipo ulaya..Ha ha ha ha.

Selection zikatoka- baada ya selection kutoka na kutambua kwamba natakiwa niende Umbwe secondary, maandalizi yakafanyika, nunua matranka/masanduku ya chuma, shopping ya vyakula hasa vitu kama sukari , siagi/blueband, Maziwa ya nido bi mkubwa akanitengenezea achali, nikanunua na nguo za kujikinga na baridi. Nakumbuka nilistruggle kutimiza mahitaji sababu, ndy kipindi mzee wangu alisimamishwa kazi ofisini kwake na hakuwa hata na senti ya kunipa, so naweza kusema bakuli lilitembea kiasi kwa ndugu na jamaa. Lkn kwa bahati mbaya halikuweza kutimiza mahitaji yote yaliyo orodheshwa....amount nzima kama sikosei ilikua kama 150k au 200k..ambayo hata robo ya pesa tunayowasomeshea watoto wetu ktk hizi shule za siku hizi haifikii..ama kweli mmb yamebadilika..in short watoto wa town wanasema ilipatikana pesa dusko....lkn kwa kuwa nilipenda shule alafu nilitoka kumwagwa na demu wng ha ha ha so mnajua mapenzi ya kiolevel au balehe yalivyo.., so ilinisukuma sana, nikasema wacha niende nitajua huko huko mbele ya safari, nakumbuka nilichelewa sana kureport shule. Basi nikachukua saibaba yangu kidume pale ubungo, nikatulia ndani ya siti huku kimoyo kinadunda na mawazo kedekede ya kama kweli ntapokelewa na ada nusu? Je nisipopokelewa nitafanyaje na ela watu tumeshawakamua mpk tone la mwisho, pia nikawa nawaza jinsi ya kufika huko "kibosho Umbwe" in short nilikua nahisi kupagawa ! Basi bwana Mungu siyo John , bus likafika Moshi mjini majira ya jioni hv saa 11 au 12 hv, nikauliza vihiace vya kwenda niendako , nikazama, safari ikaanza na hiace kadri ilivyokua ikiunguruna injini moyo ulikua wazidi kudunda, kadri gari nililivyozidi kwenda kuingia ndani ndani kupitia barabara ya kibosho, hali ya hewa ilizidi kubadilika...nikawa nahisi kaubaridi kwa mbaaaali................!!

Kuwasili Shuleni- baada ya mwendo kama wa dakika 45 hv tukawasili kituo changu, panaitwa kwa rafaeli , basi nikashuka na mabegi na tranka langu, safari ya 1km kuelekea shuleni ikaanza....aiseeee hapo nilijihisi nipo katika ulimwengu mwengine kbs, sababu nilitoka Dar jua lilikua nyuzi joto 27 au zaidi, na kuja kwenye hali ya hewa ya nyuzi joto 15 kuchuka chini , ilikua ni changamoto sana, lkn kwakuwa niipenda hali ile hewA haikuwa shida kwangu, kitu pekee katk umbali niliotembea wa 1km niliona ni migomba na mibuni tu, watu walikua wachache mnoo.....aiseee wamissionary sjui waliwaza nn kwenda kujengA shule kule... Nikafika shuleni majira ya saa moja hv au zaidi , kulikua na ukimya mkubwa eneo la shule nikaja fahamu baadae kuwa wanafunzi walikua prepo! Basi nikareport kwa mkuu wa shule msaidizi alikuwa "mtawa" au sister km tulivyozoea kuwaita, akaomba joining nikampa, akataka list ya vifaa vilivyoagizwa kama slasher, ndoo nk, nikampa, akataka ada na michango mengine hapo moyo ukaongezeka kunadunda.......mara nikaskia mbona umeleta pesa kdg sana, nikamwambia Madam.....kabla sijamaliza akanambia sasa skiliza kijana, sisi hatutokupokea leo mpaka utakapotimiza kila kitu, nitakuelekeza sehemu ukaweke vitu vyako kisha ufate pesa imagine....nikajitetea kuwa natokea mbali na nauli sina.......aisee mama Yule hakunielewa, nilichofanya nikachukua pesa kdg ya "pocket money" na kuliamsha asbh yake, nikakata ticket ya elfu saba hadi Dar................

Itaendelea....... huko mbele ndipo kwenye drama za shule za bweni sasa!
 
MKUU MI NAKUMBUKA SIKU YA KWANZA NAPELEKWA PALE NYEGEZI SEMINARY NA MAMA YANGU.
Nikaripoti na kusajiriwa kisha Mama akaondoka,nikaanz kumlilia.Baadae nikakabidhiwa kwa DOM LEADER nae akanikabidhi kwa ROOM READER ambae alikuwa ni Form 2.
Aisee nilijuta baada ya kufikishwa chumbani.Niliambiwa nipige pushapu 100 na kusali Rozary.
hayo ndio yalikuwa mapokezi yangu ya siku ya kwanza wakuu
 
Me experience nimeipata kwa kusimuliwa tu polen sana mmepata tabu sana hahaahaha
 
nakumbuka nilipelekwa boarding ya wasichana aisee nilikuwa nawabonyeza tuu.
shikamoo dada miriam kwa kunipokea.
 
Nilichaguliwa kidato cha kwanza shule moja iliyoko mjini.. na mimi natokea kijijini hakuna umeme, siku hiyo umeme ukakatika shule form one tukaambiwa tuchukue ndoo tukachote umeme..
 
Nilienda Advance shule moja ya serikali aisee nilikaa miezi 3 nikahama nikarudi zangu privAte
Shule haina maji.vyoo vinanuka watu wanaongia uchi kabsa ili nguo zisinuke
Hakuna libraly,darasa kama banda la mbuzi,kuamshana asubuhi kudeki na kufagia
Wakati nilizoea private m1 kwa mwaka unasoma kama upo nyumbani
 
Daaa Mimi ilikuwa paroma secondary nimeenda pale kidato cha tatu kutoka shule ya kata duu nilikuja kuzoe fimbo na nikawa m babe kwel wakat nilikuwa mpole
 
Mimi sikuwahi pata tabu boarding kabisa .
O'level na Advance pia .
Mother wangu alikuwaga mwalimu shule ya boarding afu nilikuwa naishi kota za shule so maisha ya boarding nilikuwa nayaona na kuyaexperience since niko standard one .

Mazingira ambayo nilikulia pia vijana walikuwa wakorofi sana .wakati naanza form nilikuta ma brother wengi wakitaa wako form 3 so life was easy.

Ila advance madogo wa O level waliniotea wakanichapa Converse zangu na dickies yangu.
 
nilichaguliwa maswaaaa girls yaaan kipind hiko shinyangaaa uchawiii umeshikaa chat yaaan nikawa na lala na baibo
 
kwa kumlilia mama tu, ulistahili push up 100000
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…