Experience yangu ya kilimo cha vitunguu ni negative

father-xmas

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2010
Posts
971
Reaction score
1,117
Heshima kwenu viongozi wangu.

Wakuu natumai hamjambo na mnaendelea vyema na shughuli za ujenzi wa taifa letu.
Wakuu baada ya kusikia wengi wetu wakisifia sana kilimo cha vitunguu nikapata muamka na mimi nikaingia katika kilimo cha vitunguu.

Nilikodisha ekari sita pale Ruaha Mbuyuni.
Kwa kweli sitaki kusema mengi ila ninachoweza kusema ni kwamba kutajirika kwa kilimo cha vitunguu LABDA inawezekana lakini sio kiurahisi kama wengi wetu wanavyohubiri humu.

Kwa EKARI ZOTE SITA nilizolima nilivuna gunia mia moja na tano tu.
Gunia moja niliuza kwa shilingi elfu thelathini tu.
Nilivuna mwezi wa saba mwaka huu ,2014.

Nilitumia shilingi karibia MILIONI KUMI NA TATU kulima ekari zote sita halafu nilipovuna nikapata shilingi milioni tatu laki moja na elfu hamsini hivi.3,150,000 kutoka kwenye mavuno ya ekari zote sita.

Nilikua makini sana kutimiza mahitaji yote niliyoambiwa nikitimiza nitavuna na kupata faida.
Anayetaka kuingia kulima na aingie ila tuwaeleze wenzetu ukweli,hichi kilimo ni very risky.

Anyway,mwakani nitalima tena maana jamaa wamenishawishi sana wakidai hasara ya mwaka huu isinikatishe tamaa.Nashindwa kusema kama kinalipa au hakilipi kwa sababu nimelima mara moja tu.Matokeo ya mwaka kesho ndio yatanipa uamuzi wa kujikita kwenye kilimo au kujitoa na kuwaachia kina Malila.

Kitu nilichogundua ni kuwa watu wengi humu hawasemi ukweli kuhusu hichi kilimo.
 
Pole mkuu. Jee ulikuwepo mwenyewe kwa muda mrefu huko shambani au umelipa tuu watu wasimamie. I guess im trying to figure out labda majanja walivuna magunia mengine before you got there....ila again pole sana usikate tamaa
 
Pole mkuu. Jee ulikuwepo mwenyewe kwa muda mrefu huko shambani au umelipa tuu watu wasimamie. I guess im trying to figure out labda majanja walivuna magunia mengine before you got there....ila again pole sana usikate tamaa

Shukruni mkuu.
Nilikua nakwenda kila wiki.
Kila lilipofanyika jambo la muhimu mfano kutia mbolea kumwagilia madawa au palizi nilikuwepo mwanzo hadi mwisho.
Wakati wa kuvuna mpaka kuuza nilikuwepo.
Kwa kifupi sijapoteza pesa tu,bali nili invest muda wangu mwingi sana.
 
Pole sana kamanda,,M10 umezizika hivihivi!
Je wenyeji walikwambia shida ilikua nini? mvua nyingi au ?

Thank you mkuu.
Wenyeji wanachosema ni kwamba huu ni mwaka wa kilio kwa kila mtu.
Na sio mimi tu nimeshuhudia watu waliokula hasara kuliko hata mimi.
Kuna waliokata tamaa wakatekeleza mashamba yao hata kabla ya kufikia mavuno.
 
Acha kudiscourage watu wengine Mbona tulipata sawasawa na investment zetu
The issue here is the management basi,ukulima wa simu wtf you expect lazima utavuna mabua tu

Hongera sana mkuu.(
Sina lengo la kum discourage yeyote,hii ninayoongelea ni expirience yangu.
Hebu naomba uniambie wewe ulilima wapi,umevuna gunia ngapi kwa ekari,umeuza bei gani kwa gunia na uliuzia wapi.

Mkuu sifalima kwa simu kama unavyodai,nilikwenda mwenyewe front line.
Halafu pia ungeweza kutoa hoja bila kutumia hiyo ´wtf´
 
Ni kawaida ya watu kusifia jambo bila kutoa the risky side of it. Mi mwenyewe nililima ekari 40 za mahindi kibaigwa ndani...ile yanakaribia kupalilia ng"ombe from nowhere zikafagia shamba lote. hizi ni changamoto ambazo kwenye ujasiriamali zinatakiwa kuwa nazo makini. Pole sana mkuu, I understand. Hope Mungu atakureward next time kwa vile umefanya kazi.
 
Thank you mkuu.
Wenyeji wanachosema ni kwamba huu ni mwaka wa kilio kwa kila mtu.
Na sio mimi tu nimeshuhudia watu waliokula hasara kuliko hata mimi.
Kuna waliokata tamaa wakatekeleza mashamba yao hata kabla ya kufikia mavuno.
Kaka sijakuelewa, yani kilio kimesababishwa na nini?
 

Fanya analysis ya soko kujua mzunguko wake ukoje unaweza kurudi mwakani wakati uleule ukajikuta unaumia tena.Wanaopata faida ni wanaolima wakati wote kwa mzunguko hasara inafidiwa kipindi anapokutana na soko zuri.Hii kuotea once kuna probability ya kupata na kukosa.Hizi ni perishables na si kama madini ambapo once you get umetoka.
 
Ni kweli mkuu. Mimi nimelima Ruaha kwa miaka mitatu misimu 6 nimeamua kuacha kwasababu kila mwaka siwezi hata kubreak even lakini wenyeji wanakupa hope kwamba msimu ujao utapata hela.

Kilimo cha pale ni kigumu sana gharama ziko juu sana labour ya shida sana pia.
 
Gunia 105, kama ungepata chanja ukaviweka mpaka mwezi wa kwanza|pili hasara ingepungua sana.
 
Mimi nimelima maharage taga heka moja kwa simu,nimepata hasara ya laki 2
 
Mkuu Mangi muitiro. Umepata hasara sawa.. je umefanya jitihada gan kujua hiyo hasara uliyoipata imesababishwa na nn.. coz unavyosema kwamba wenyeji wamekuambia msimu ujao utapata unafanya kama vile unajaribu kubahatisha...
 
Last edited by a moderator:
Mimi naogopa sana kuingia shambani maana ni kilio sana bora biashara zingine kulima walimr mie nitanunua toka kwa wakulima
 
Heshima kwenu viongozi wangu.

Anyway,mwakani nitalima tena maana jamaa wamenishawishi sana wakidai hasara ya mwaka huu isinikatishe tamaa.

Mkuu milioni 10 kuzipoteza sio jambo dogo.., pia huo muda uliopoteza ni priceless..; sasa unavyosema utalima tena ni kama kubahatisha sababu ukifanya kitu kile kile ulichofanya mwaka huu huenda matokeo yakawa yaleyale...

Kwa ushauri mimi naona kwa yoyote anayeanza kufanya kitu chochote kwa kuanzia ni bora aanze kidogo kidogo.., hii itakupa experience na wewe kujionea mambo yanavyokwenda. Sababu mkuu just imagine haujawahi kuuza alafu ghafla una gunia mia na kitu.., alafu jambo lenyewe ni perishable hata wanunuzi wataona desperation na inaweza kupelekea wewe kuuza bei ya kutupa.

Pili nimeshaona wabongo wengi kitu kama kina faida sana kwa wakati fulani basi inapelekea kila mtu kufanya kitu kile kile.., hii inapelekea supply kuwa kubwa sana ghafla na huenda zile bei zilizozoeleka zikashuka..

Kwahio mkuu Ushauri kama Utalima tena...

  • Anza kidogo ili upate uzoefu.., hata ekari moja kwanza watu wakujue na ufahamu mwenendo wote mpaka wa soko
  • Tafuta soko kwanza ujue kabisa unauzia wapi na uwe na plan B..., yaani kama soko likiwa baya hakikisha unao uwezo wa ku-store kwa muda mpaka bei zitakapopanda
  • Kama Kilimo chako kinategemea hali ya hewa (na sio umwagiliaji) basi kuwekeza pesa nyingi ni kama kamali
  • Katika Hesabu zako za kupata faida weka the worse case scenario.., yaani fikiria kwamba mfano bei ikiwa mbovu kuliko zote bei ni kiasi gani ?, alafu hii ndio pigia hesabu
  • Ukisikia fulani kauza labda yeye anao mtandao wake.., madalali mara nyingi ukiwa hauna mzigo wanasema lete hakuna neno na kama unautoa mbali siku ukiuleta wanaanza story za kwamba mzigo mara mbovu au kuna malori yameingia toka vijijini kwahio kuna mzigo wa kumwaga n.k. (hii yote ni kujaribu kushusha bei na wanajua hauna jinsi utashusha tu..) Point yangu hapa hakikisha kabla una sehemu za masoko zaidi ya moja ili moja likikataa basi lingine unaweza kufanika..

Zaidi ya hapo hakuna tofauti na mtu anayeweka pesa zake kwenye Betting Manchester United inapocheza na Chelsea ukitegemea mmojawapo ashinde
 

Well said mkuu... hayo uliyoyasema ni ya msingi. Watu wengi wanaingia kwenye masuala mbali mbali bila kutulia na kufanya maamuzi ya busara... yaan mtu akishakuwa excited kwa maneno ya watu baass anazama mzigon tu...
 
kweli kabisa mkuu father-xmas watu hawatoi maelezo ya faida na upande wa hasara pia, wana base upande wa faida tu na hapo ndipo upotoshaji unapotokea.

Kuna jamaa yangu mwaka huu alilima kilimo cha nyanya, kwa kusikia maneno ya upande wa faida wa hiki kilimo, baada ya kuvuna amepata hasara sana, sababu ya bei kuwa chini tofauti na mategemeo.

Ushauri: bora tufanye tafiti binafsi kabla ya kuweka nguvu zetu humo. pia ni vizuri tukaanza na ekari chache kwa majaribio ili kuepuka hasara kubwa.
 
Last edited by a moderator:

Mkuu umenikumbusha kilichonipata mwaka jana nilipolima pale RUVU. Wenyeji walinipa moyo sana kuwa nitavuna lakin hakuna nilichoambulia. Iliniuma sana lakin maisha yanaendelea...!!
 
Pole kwa hilo. Nadhani next time upunguze eka. Lima 3 hivi. Pia badili msimamizi. Inshaalah utafanikisha. Mie nimejaribu first time eka 1.5 na ndo ninaendelea. Nasika best time kupanda na mwezi wa pili wa tatu.

Mie nalima kidika. Wewe unalima eneo gani kule ruaha mbuyuni?

Wasalaam
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…