kwel mkuu hujakosea bora uchukue mazao uadd valueKulima Tanzania ni kazi kubwa sana.
Masoko sio ya uhakika.
Nimekuwa nikifuatilia kwa muda mrefu sana kuhusu kilimo cha vitunguu, kila mtu akitoa uzoefu wake. kila mtu anatoa taarifa zake, wengine za kutia moyo na wengine za kukatisha tamaa. Hivi ukweli ni upi jamani, maana mpaka sasa nimeshindwa kuelewa kwamba ni kilimo chenye faida au hasara?
Pole sana mkuu,mimi naungana na wewe,kwakweli kilimo cha kutegemea soko la walaji wa moja kwa moja
ni hasara.Namaanisha kilimo kinacholipa ni kile cha kuuza viwandani ambapo unapeleka mzigo mzima na unauza.
bila risk ya kuharibikiwa na bidhaa yako.
Binafsi nina uzoefu na kilimo cha mihogo,nilikodi shamba na kulima kule kisarawe,ukweli mihogo ilikubali
msimu wa kuvuna ukawa ni wakati wa mwezi wa ramadhani,ukweli ni kwamba wanunuzi wa jumla wanaokuja shambani wanataka wakulalie,niliamua kuuleta muhogo mwenyewe mjini nikajikuta napata hela ya wachimbaji na mafuta ya gari na kubaki na mihogo iliyokosa soko nimetengeneza unga nakula mwenyewe.
Wenyeji wananiambia mwakani soko linaweza kuwa zuri nisikate tamaa.
Nilichogundua ni kwamba wenyeji wananufaika na hiyo mitaji yetu hivyo hata siku moja hawawezi kukukatisha tamaa
maana wao ndo wanalima unawalipa,wanapalilia unawalipa,wanavuna unawalipa.soko unatafuta wewe
uwe umepata umekosa wao hawana hasara wanakusubiri msimu ujao.
Kwa ufupi kilimo cha kutegemea soko la mtu kwa mtu na risk,labda mazao ambayo tayari yana viwanda vya kusindika.
Heshima kwenu viongozi wangu.
Wakuu natumai hamjambo na mnaendelea vyema na shughuli za ujenzi wa taifa letu.
Wakuu baada ya kusikia wengi wetu wakisifia sana kilimo cha vitunguu nikapata muamka na mimi nikaingia katika kilimo cha vitunguu.
Nilikodisha ekari sita pale Ruaha Mbuyuni.
Kwa kweli sitaki kusema mengi ila ninachoweza kusema ni kwamba kutajirika kwa kilimo cha vitunguu LABDA inawezekana lakini sio kiurahisi kama wengi wetu wanavyohubiri humu.
Kwa EKARI ZOTE SITA nilizolima nilivuna gunia mia moja na tano tu.
Gunia moja niliuza kwa shilingi elfu thelathini tu.
Nilivuna mwezi wa saba mwaka huu ,2014.
Nilitumia shilingi karibia MILIONI KUMI NA TATU kulima ekari zote sita halafu nilipovuna nikapata shilingi milioni tatu laki moja na elfu hamsini hivi.3,150,000 kutoka kwenye mavuno ya ekari zote sita.
Nilikua makini sana kutimiza mahitaji yote niliyoambiwa nikitimiza nitavuna na kupata faida.
Anayetaka kuingia kulima na aingie ila tuwaeleze wenzetu ukweli,hichi kilimo ni very risky.
Anyway,mwakani nitalima tena maana jamaa wamenishawishi sana wakidai hasara ya mwaka huu isinikatishe tamaa.Nashindwa kusema kama kinalipa au hakilipi kwa sababu nimelima mara moja tu.Matokeo ya mwaka kesho ndio yatanipa uamuzi wa kujikita kwenye kilimo au kujitoa na kuwaachia kina Malila.
Kitu nilichogundua ni kuwa watu wengi humu hawasemi ukweli kuhusu hichi kilimo.
Mkuu pole,
Mchana huu niko Iringa mjini nimefika mara moja kisha narudi porini. Niko na jamaa yangu mmoja, yy alilima pawaga karibu na kijiji cha Mloa, nimetoka huko leo. Ni kwamba jamaa wanalia pia, kitunguu kimewaliza. Wakati napandisha huku Iringa na mdau wangu mmoja alinionyesha plot yake ya vitunguu swaumu pale Isele/Masukanzu Ilula. Kijana aliyekuwa pembeni alisema Ruaha mwaka huu ni kilio sana kwa kitunguu maji.
Waliolima mahindi pia hali sio nzuri, mpunga ni mwingi balaa. Naomba usikate tamaa, ila angalia sana manpower unayotumia. Leo jioni nitakuwa na jamaa, nitajaribu kumuuliza nini kimetokea ghafla. Nikupongeze sana kwa kurudisha feedback.
Malila mashamba ya miti bado yanapatikana? kuna jamaa alinielekeza kwako,
Kujiingiza kwenye kilimo ni sawa na kubet roho yako porini kwenye simba na dubu huku ukitegemea kutoka salama.
Kujiingiza kwenye kilimo ni sawa na kubet roho yako porini kwenye simba na dubu huku ukitegemea kutoka salama.
Pole kwa hilo. Nadhani next time upunguze eka. Lima 3 hivi. Pia badili msimamizi. Inshaalah utafanikisha. Mie nimejaribu first time eka 1.5 na ndo ninaendelea. Nasika best time kupanda na mwezi wa pili wa tatu.
Mie nalima kidika. Wewe unalima eneo gani kule ruaha mbuyuni?
Wasalaam
Hapo kina sehemu yamefanyika makosa labda ungetuambi wapi umekosea. Mana ukisema umevuna gunia 105 ttu kwa heka Sita haniingi akilini naamini kabisa kuwa Kuna kosa la usimamizi tu
Mkuu pole,
Mchana huu niko Iringa mjini nimefika mara moja kisha narudi porini. Niko na jamaa yangu mmoja, yy alilima pawaga karibu na kijiji cha Mloa, nimetoka huko leo. Ni kwamba jamaa wanalia pia, kitunguu kimewaliza. Wakati napandisha huku Iringa na mdau wangu mmoja alinionyesha plot yake ya vitunguu swaumu pale Isele/Masukanzu Ilula. Kijana aliyekuwa pembeni alisema Ruaha mwaka huu ni kilio sana kwa kitunguu maji.
Waliolima mahindi pia hali sio nzuri, mpunga ni mwingi balaa. Naomba usikate tamaa, ila angalia sana manpower unayotumia. Leo jioni nitakuwa na jamaa, nitajaribu kumuuliza nini kimetokea ghafla. Nikupongeze sana kwa kurudisha feedback.
Mimi nimelima maharage taga heka moja kwa simu,nimepata hasara ya laki 2
Ndio yanapatikana, bei ni Tsh 60,000/ kwa eka moja. Unapata shamba lilipo shamba langu.Kazi kwako