Just Distinctions
JF-Expert Member
- May 5, 2016
- 3,230
- 6,742
Bidhaa zinazotengenezwa viwandani huwa na viambata mbalimbali ambavyo huzifanya kuwa na ubora na kudumu kwa muda ambao umekusudiwa bila kuharibika.
Pindi ule muda uliokusudiwa utakapovuka, bidhaa kama vinywaji, vyakula, dawa au vipodozi na nyinginezo nyingi huwa hazifai tena kwa matumizi ya binadamu.
Endapo bidhaa ambayo imeshaisha muda wake ikitumiwa, huweza kusababisha madhara mbalimbali kwa binadamu na wanyama, na kwa matumizi mengine huweza kutofanya ile kazi iliyokusudiwa.
Serikali kupitia Mamlaka zinazohusika na kudhibiti ubora wa bidhaa kama Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Mamlaka ya dawa na Vifaa Tiba (TMDA) imekuwa ikikagua ubora wa bidhaa mbalimbali ili kuhakikisha zinatengenezwa katika viwango na ubora ili kutomdhuru mtumiaji, na kila bidhaa inayotengenezwa kiwandani huwa na tarehe ya lini imetengenezwa na tarehe ya mwisho wa matumizi (Expiry date) ambayo ikivuka tu bidhaa hiyo huwa haifai tena kwa matumizi na inapaswa kuharibiwa.
Unaijuaje tarehe ya kuisha muda wa matumizi kwa bidhaa?
Tarehe ya kutengenezwa na Kuisha kwa muda wa matumizi bidhaa, huandikwa katika vifungashio vya bidhaa na huwa katika namna ifuatayo;
Tarehe ya kutengenezwa au Kupakiwa ( date of manufacture/ date of packaging) kwa kifupi huandikwa ‘MAN’, ‘P’, ‘MFG’ au ‘M’ ikifuatiwa na tarehe husika, ‘MAN’ AU ‘MFG’ husimama kama ‘Manufactured’, P ‘produced’ au ‘packaged’ na ‘M’ ni made.
Mfano ni MAN09/20 , P09/21, MFG09/21 au M09/21 inamaanisha bidhaa husika ilitengenezwa au kupakiwa mwezi septemba mwaka 2020.
Tarehe ya bidhaa kuisha ubora wake au itumike kabla ya. . . au isitumike zaidi ya tarehe (Expiry date/Best before/Use by date) kwa kifupi huandikwa ‘E’ au ‘EXP’ ikimaanisha ‘Expiry’ na ‘BB’ ni ‘best before’.
Mfano ni EXP06/23, E06/23 au BB06/23 inamaanisha bidhaa husika itaisha muda wa matumizi yake mwezi wa sita mwaka 2023.
Kutegemeana na ufinyu wa kifungashio, tarehe ya kutengenezwa bidhaa inaweza isiandikwe ila ya kuisha muda wake ni lazima iandikwe, na inaweza kuandikwa mwezi na mwaka pekee.
Picha : Mojawapo ya bidhaa zikionesha tarehe ya kutengenezwa na tarehe kuisha muda kwa matumizi yake.
Changamoto huwa wapi?
Watumiaji wa mwisho ambao ndio wanunuzi kwa kutojua au kutozingatia kuangalia tarehe ya kuisha kwa muda wa kutumika bidhaa, huweza kusababisha matumizi ya bidhaa iliyoharibika.
Wauzaji wa rejareja, kubuni mbinu ya kuuza bidhaa kwa rejareja kama maziwa ya unga, siagi au ngano bidhaa hizi hufunguliwa kwenye kifungashio chenye ujazo mkubwa na kisha kuuzwa kidogo kidogo kwa kipimo maalum. Kwa wafanyabiashara wasio waaminifu wanaweza kutumia mbinu hii kuuza zile zilizokwisha muda wake.
Tofauti na bidhaa kama Sukari, mafuta ya kula, ngano na nyinginezo ambazo hununuliwa mara kwa mara kutokana na kuhitajika kwa matumizi ya kila siku changamoto huja katika bidhaa nyinginezo zisizo na uhitaji sana kwenye soko au kutokuwa na desturi ya kutumika mara kwa mara na wananchi wa kawaida.
Kuna madhara gani ya kutumia Bidhaa iliyokwisha muda wake?
Madhara ya kutumia bidhaa iliyokwisha muda wake ni mengi na yanaweza kuwa makubwa au kiasi kutegemea na aina ya bidhaa iliyotumika , Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa na mtandao wa eatthis mwaka 2020 inasema bidhaa iliyokwisha muda wake inaweza kusababisha kizunguzungu, kichefuchefu, kuharisha na hata kuunguruma kwa tumbo kutegemea na jinsi ilivyoharibika.
kupitia taarifa iliyochapishwa na mtandao wa drugs.com ambao huchapisha taarifa mbalimbali za masuala ya afya, katika taarifa ya mwaka 2021 ambayo imehakikiwa na Mtaalamu wa afya Ann Leighan, imesisitiza wagonjwa kutotumia dawa zilizokwisha muda wake kwani inaweza kusababisha ngozi kuchubuka kama ni ya kupakaa na madhara mengineyo mwilini ikiwa ni ya kumeza.
kupitia taarifa iliyochapishwa na wavuti ya Panganifm ya mwezi novemba, mwaka 2019 ikielezea kukamatwa kwa shehena ya bidhaa zilizokwisha muda wake katika wilaya ya Pangani baada ya ukaguzi uliofanywa na idara ya afya kwenye maduka ya jumla na rejareja, Taarifa hiyo imemnukuu Afisa Afya Mohammed Nyati akisema bidhaa ikiisha muda wake wa matumizi hugeuka sumu na huweza kusababisha madhara tofauti ikiwemo kansa na hivyo kuwasihi wananchi kuchukua tahadhari kabla ya kununua bidhaa.
Nini Kifanyike ili kuzuia matumizi ya bidhaa zilizokwisha muda wake?
Kwa Serikali:
i. kupitia Mamlaka husika kama TBS na TMDA na nyinginezo, huhakikisha bidhaa zinazotumika zimefikia viwango stahiki na pia isisitize maelekezo ya kwenye vifungashio yaandikwe katika lugha inayoeleweka na wengi mfano Kiswahili.
ii. Kwa kushirikiana na wadau wengine ikiwemo taasisi zisizo za kiserikali, wataalamu wa afya na vyombo vya habari watoe elimu kwa umma wa namna ya kuangalia na kukagua tarehe ya bidhaa husika ili watambue endapo bidhaa imekwisha muda wake wasitumie.
iii. Serikali iendeleze utaratibu wa kufanya uhakiki madukani ili kuhakikisha kuwa bidhaa zinazouzwa hajizaisha muda wake na endapo wafanyabiashara wakikutwa wanafanya hivyo wapewe adhabu kali.
Kwa Wafanyabiashara;
i. Wahakikishe kuwa bidhaa zote walizonazo zipo kwenye muda sahihi wa matumizi kwa kukagua hifadhi walizonazo na kuhakikisha bidhaa inayouzwa haijaisha muda wake.
ii. Endapo mfanyabishara akigundua bidhaa imekwisha kwa muda wake basi waziteketeze ili kuepusha kuwadhuru watumiaji wa mwisho.
Kwa walaji/watumiaji wa mwisho;
i. wahakikishe tarehe ya kuisha muda wa matumizi kwa kila bidhaa wanayonunua kabla ya kuondoka dukani na wakatae endapo watatambua imekwisha muda wake.
ii. ikiwa kuna sehemu ya biashara ambako wanaona wana desturi ya kuuza bidhaa zilizoisha muda wake basi watoe taarifa kwa serikali kupitia polisi au mamlaka yoyote iliyo karibu nao kwa msaada zaidi.
iii. Wateja wasikubali kununua bidhaa ambayo haioneshi muda wa mwisho wa kuisha matumizi yake na endapo itakuwa imefutwa basi wakatae bidhaa hiyo.
iv. Wajenge utamaduni wa kukagua tarehe ya kuisha kwa ubora wa bidhaa (expiry date) hata baada ya kununua, kwani inaweza kuharibika baada ya kutotumiwa kwa kipindi kirefu ikiwa nyumbani hivyo ni muhimu kukagua.
Hitimisho
Jukumu la kukagua ubora wa bidhaa linagusa pande zote kwa mtengenezaji kuhakikisha anatengeneza bidhaa bora katika mazingira yaliyo sahihi na serikali kupitia mamalaka iliyozikabidhi dhamana ya kukagua ubora huo kuhakikisha bidhaa inafaa kwa matumizi.
Mfanyabishara naye ana wajibu wa kuhakikisha bidhaa anaitunza katika mazingira mazuri na hauzi bidhaa iliyoisha muda wake. Na mtumiaji wa mwisho anapaswa kuhakikisha bidhaa anayouziwa bado haijaisha muda wa matumizi.
Pia ukiachana na tarehe ya mwisho ya kutumika kwa bidhaa (expiry date) mtumiaji wa mwisho anapaswa kuzingatia maelekezo mengine yaliyoandikwa kwenye kifungashio cha bidhaa husika, ikiwa pamoja na namna sahihi ya kuhifadhi bidhaa yake kama ambavyo baadhi ya bidhaa husika huelekeza mfano hupaswi kuweka bidhaa hii katika sehemu yenye joto kuzidi centigredi kadhaa, hifadhi kwenye jokofu, epusha miale ya jua ya moja kwa moja, au ikifunguliwa isitumike zaidi ya siku thelathini tangu kufunguliwa na maelezo mengineyo, hii itaepusha madhara kwani bidhaa hata kama tarehe ya kuisha ubora wake itakuwa bado haijafika, kutoitunza jinsi inavyotakiwa huweza kuisababishia kukosa sifa za matumizi na hivyo kumdhuru mtumiaji endapo itaharibika.
Je ushawahi kukumbana na changamoto ya Bidhaa iliyokwisha muda wake? Je ulichukua hatua gani?

Upvote
3