Tunaangalia Uhusiano ulioko Afrika mashariki na sio kujaribu kupindisha nyuzi. Tafadhali! Tazama historia ya EA muongo moja uliopita na visa vya ugaidi na ujaribu kujifafanulia kuwa ugaidi umeingia EA. Sio suala la nani ametakasika akangara au nani muovu. Ni suala nyeti ambalo haliitaji kufanyiwa uchanganuzi bila kuzuia mafikira kuingiliwa na jazba zezote za kimitaa.
Mr.Kabaridi unachosema ni kweli wala tusijidanganye kwamba kuna nchi Africa Mashariki ambayo hiko salama dhidi ya -
determined TERRRORISTS, wenzetu wazungu usema a good terrorist ni
yule aliye kufa! Wala tusidanganye kwamba fujo fujo za watu wa Mombasa na watu wa Zanzibar hazina uhusiano wowote, hawa jamaa lao moja! Wewe mtu hata kama hataki muhungano kwa nini achome Kanisa!
Huu si wakati wakubezana na kutuniana misuri na kuzungumza mambo ambayo hayana mshiko - hili ni janga la sisi wote raia wa Africa Mashariki bila kujari tunatoka nchi gani, cha muhimu hapa ni kupeana mbinu za kujikinga na wendawazimu hawa ingawa sirahisi kujikinga 100%.
Niliwahi kuishi na mwanafunzi Mu IRISH kwenye council flat moja bila kujua kwamba alikuwa ni member wa IRA, tunapika tunakula, ku-study na kuzungumza mambo mengi tu lakini hakuwahi kunambia chochote kuhusu harakati zake! Mwisho mwishoni ndio kunieleza alikuwa nani - si hilo tu kanieleza kwamba Gaddafi alikuwa anawapatia silaha na explosives hatari wanazichimbia kwenye milima ya Lake Districts (North West) hakunieleza walikuwa wanatumia njia gani kizisafirisha kutoka Libya, nilishtuka sana!
Kutokana na mazungumzo na jamaa huyo, ndio nikajua mbinu zao na jinsi ya kujikinga/kuchukua tahadhali ya mapema sana kabla ya kupata majanga, mpago wenu wa kusambaza Camera za CCTV mji mzima zitasaidia kiasi lakini aliwezi ku-contain watu hawa na ingekuwa bora zaidi mkitumia IP Cameras badala ya hizi za mawaya ambazo zinaweza kuhujumiwa kirahisi. Wasomaji wanaweza kushangaa hivi jamaa huyu anataka kutueleza nini hasa!
Ninacho taka kusema humu ni kwamba kutokana na mambo niliyo wahi kuelezwa nimeona ni vizuri niwape mbinu wakina
Livefire, Moyo, Kabaridi (ntawatumia as a private message) ili waweze kuzungumza na wahusika (
POLICE/Usalama) huko kwenu tahadhali nyingine za muhimu wanazopashwa kuzichukua badala ya kutegemea CCTV tu
(najua kuna watu wengine vichwa ngumu wanaweza kusema sisi Wakenya tunajitosheleza hatuitaji mawazo yoyote kutoka Tanzania, si wote lakini wapo!).
Hapa tunasaidiana kwa kutoa mawazo ya kujenga/kusaidia katika usalama wenu na sisi,
remember two heads are better than one tukianza tena mambo ya kuchaganya changanya mambo au mmoja kujiona zaidi hawa watu watatumaliza. Tutakiane heri TU.