Extra-port charges (imported car)

Mrejessho:

Gari imefika nmetoa lakini sio gharama zile humu JF

Watu walizisema ..daah anyway ukiomba ushauri humu sio wote wanajua [emoji28]
Tujulishe ukweli wa hizo gharama ili zitoe mwongozo mzuri Kwa wanaotarajia kuagiza gari nje.

Pia itapendeza ukisaidia kujua gharama za forodha pamoja na kampuni nzuri ya kutoa gari bandarini.
 
Sawa ngoja nikipata muda ntakuja kuwapa watu the whole experience jinsi nlioanza kuchagua gari mpaka imenifikia mkononi gharama zote

Lakini Clearing agent ambaye amenitolea gari within 24 hr toka meli imeshushwa tena kwa bei rahisi sana

Ni TRIMEX CLEARING AND FORWARDING

nlikutana nao instagram tu lakini nimewapenda
 

Safi sana [emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]

Gharama zao zikoje hao TRIMEX CLEARING AND FORWARDING, je si wasumbufu????
 
Huku kwetu mambo yanabadilika badilika , zamani tbs walitoa ruksa magari kukaguliwa nje ya nchi kwa niaba yao , siku hizi wanakagua wenyewe yakifika Tanzania .
Mara ya mwisho ulishuhudia huu ukaguzi wa TBS lini?

Ni kweli huu utaratibu ulikuwepo. TBS walikuwa wanakagua magari na yalikuwa hayatoki hadi tatizo litatuliwe.

Mwezi Jan 2023 gari ya rafiki yangu ilikaguliwa na TBS na ripoti ikaonesha matairi yameisha. Ilibidi tufunge tairi mpya ndio gari ikatoka pale Beforward.

Ila kwa sasa utaratibu umebadilishwa tena.

June 10 nilienda kuchukua gari Enhance Auto baada ya kuwa cleared. Ukaguzi uliofanyika na kupata certificate ni wa EAA kwa niaba ya TBS na ulifanyika Osaka, Japan.
 

Attachments

  • Screenshot_20230626-011056.png
    114.5 KB · Views: 31

Mkuu humu JF watu wajuaji sana,

Mi nliambiwa hivohivo lakini gari yangu imefika nmesubmit ile EAA tbs ya Japan wala haijakaguliwa tena

Kiukweli hata zile port charges walizosema sio kweli

Watu walinambia niandae 1.5m kwa crown[emoji23]

Lakini hazifika hata laki6 daah nmebaki nacheka tu
 
Nataka niandae uzi wenye experience nzima nlivoagiza gari mwenyew mpaka kufika mkononi bila kupitia Agent

Gharama zote ntaweka hapa
Watu waacha kuogopa,tunatishana sana

Kumbe mambo ni tofauti,nmeagiza mwenyew nimesave karibu 5M kama ningeenda yard zetu pale mjini kati[emoji28]
kwa wale wazee wa clip Insta.Anyway ile biashara ya watu
 
Gari ya mwisho kukagua tbs ni april 2023
 

Andaa huo uzi usisahau kuni attach kwenye uzi
 
Yaani kwa kufanya hivyo utakuwa umesaidia sana Mkuu.

Wengi wetu kwa sasa tumejaa roho za kwa nini hivyo hatutaki kueleza ukweli zaidi ya kutishana pasipo sababu za msingi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…