Extra-port charges (imported car)

Izo zote unazohitaji kuanzia shipping line, wharfage hauwezi kufanya Mwenyewe Hadi umtafute clearing forwarding agent kwa sababu yeye ndio ana access yakukufanyia iyo huduma
 
Mie mara ya kwanza niliagiza mwenyewe online. Hizi gharama za TPA hata hazikufika laki 5. Ilikuwa 2014.

Mwaka huu sikutaka usumbufu. Nilichagua gari, nikaenda Enhance Auto kwenye ofisi zao. Niliwalipa Enhance Auto gharama zote ikiwepo clearance na delivery.

Walipokuja kunipigia ni kulipia TRA, kisha baada siku chache nikapigiwa nikachukue chombo.
 
Agent fee kumbe ata 200k wanakubali? Duh nimetoka kupigwa 300k juzi tu.
Yes ni makubaliano tu haipo fixed na kuna baadhi ya magari huwa wanatamani tu kuafanya kazi maana kuna gaps kibao bandarini wananufaika kuliko hiyo agency fee. Agent ndio midle man kati yako mteja na Tra
 
Utamu wa crown umenifanya nipotee huku
Any way nazani soon ntaandika
 
Agent fee kumbe ata 200k wanakubali? Duh nimetoka kupigwa 300k juzi tu.
Sio kupigwa mkuu hiyo ndio bei elekezi kinachotokea ni makubaliano afu ukizingatia kampuni zipo nyingi ushindani ni mkubwa so mtu hawezi kuacha hela.. So Next time tuwasiliane maana na mie nipo kwenye hiyo tasnia tunaweza fanya chini ya hapo
 
Yes ni makubaliano tu haipo fixed na kuna baadhi ya magari huwa wanatamani tu kuafanya kazi maana kuna gaps kibao bandarini wananufaika kuliko hiyo agency fee. Agent ndio midle man kati yako mteja na Tra
Kwenye gari hamna gaps nyingi vitu vinakuwa vimenyooka ila kwenye kontena ndio kuna neema kidogo.
 
Unapoagiza gari likifika tegemea hizi kodi yaani zipo tu.

1.Kuna Total tax
-(Humo ndani kuna vi kodi vingi hii ipo tu kwenye website ya TRA) na iko based na CIF yako agent anajua lakufanya hapa😀 na unalipia kwa Control no. na ni vizuri ukalipia week mbili kabla meli haijafika ili iwahi kusoma kwenye System.

2.Kuna Shipping line cost
- hii invoice inatoka pale gari inapofika bandarini na kupelekwa bandari kavu (ICD) na kupata possition, zipo nyingi bandari kavu inategemea umetumia meli gani na hii pia haupigwi maana kuna invoice unapewa na unalipa pale pale cash na iko based na CBM yaani ukubwa au nafasi iliyochukua ya gari.
*Nililipa 122k

3.Port charges
-Hii pia unalipia cash au kwa Bank sio control no. maana kuna sheet kabisa inaonyesha hiyo gharama na iko based na CBM yaani ukubwa au nafasi iliyochukua ya gari.

*Nililipa 272k

4.Wharfage cost
-Hii ni ya TRA na bila hii hutoi gari😀 japo hela ndogo sana wengi wanakwamaga hapa pale inapochelewa kusoma kwenye mfumo wa TRA,na iko based na (CIF*1.6%)+VAT utakachopata ndiyo hiyo gharama.
*Nililipa 156k

5.Utaanda 32k kwa ajili ya vibao vya plate no. Ku print na kuna jamaa wa kufunga 3k hadi 5k inategemea umeongea nae vipi.

Ukimaliza hizo gharama unapata delivery order pale (ICD) yaani bandari kavu unachukua gari yako unasepa.

NOTE; Hivyo vitu huwa anafanya agent sio wewe atakuwa tu anakwambia unatoa hela unalipia.

Kwa ujumla hizo gharama hapo hazifiki hata 600k kwa gari ndogo hizi.

*Uoga wetu wabongo ndiyo maana tunapigwa sana tupende kufanya vitu wenyewe na kujifunza.

- Siko vizuri kwenye uandishi ila naamini nimetoa mwanga.
 
Aiaeee
Shukran sana kwa elimu hii ya bure, kumbe it is very possible kupata gari for 20 milioni kama ukiagiza mwenyw na gari hiyo unaeza shangaa ukapigwa hata 30 milioni kama ukienda showroom😅😅
 
Aiaeee

Shukran sana kwa elimu hii ya bure, kumbe it is very possible kupata gari for 20 milioni kama ukiagiza mwenyw na gari hiyo unaeza shangaa ukapigwa hata 30 milioni kama ukienda showroom😅😅
Sana naumia sana nikiona mtu anapigwa kizembe eti anaogopa kuagiza gari mwenyewe na unakuta anajiita ana Degree sasa sijui hizi elimu zinatusaidia nini😡​
 
Sana naumia sana nikiona mtu anapigwa kizembe eti anaogopa kuagiza gari mwenyewe na unakuta anajiita ana Degree sasa sijui hizi elimu zinatusaidia nini😡​
Na ndio maana showroom sikuiz ni nyingi sana, wana wanakula supernormal profit, lakini pia knowledge gap ya wengi inawafanya washindwe kujua vitu vingi mno, elimu yetu tunashindwa kuiingiza kwenye application, sheeenzi zetu
 

Asante sana mkuu elimu hii watu hawana
Ukicheki huu uzi mwanzo nlipewa vitisho mara niandae 1.6m wengine walisema bila 2m pembeni gari haitoki

Lakini mwisho haikufika hata laki 6[emoji23]

Wamejazana story za vijiweni[emoji28]

Tuendelee kuelimishana
Tuendelee kuagiza magari wenyewe[emoji1420]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…