Pre GE2025 Ezekia Wenje awajia juu wanaotukana adai "Tuweke akiba ya maneno"

Pre GE2025 Ezekia Wenje awajia juu wanaotukana adai "Tuweke akiba ya maneno"

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kanda ya Victoria na Mtia nia wa nafasi ya Umakamu Mwenyekiti wa chama hicho bara Ezekia Wenje akizungumza na wanahabari siku ya Ijumaa Januari 3, 2025 mkoani Mwanza, amesema;

"Chama (CHADEMA) ni kikubwa kuliko mtu yeyote, hii dunia wote tutapita. Hiki chama mmekijenga nyinyi kwa gharama kubwa, nimesema wengine wamefariki, wamepata ulemavu, wamefirisika. Kuna maisha baada ya huu uchaguzi, mkishatukanana sana mkararuana, hivyo huyo mgombea wetu wa Urais tunakwendaje kumnadi na tumeshamtukana? Huyo Mwenyekiti wetu wa chama atakayepatikana atatuongozaje na tumeshamtukana? Tunadi wagombea wetu tukitaka lakini tuweke akiba ya maneno, kuna maisha baada ya uchaguzi "- Wenje.
 
Back
Top Bottom