Ezekiah oluochi: Wananchi msiwe na hofu,siku 21 ni chache mno kutunga kanuni za bunge maalumu

Ezekiah oluochi: Wananchi msiwe na hofu,siku 21 ni chache mno kutunga kanuni za bunge maalumu

FBY 2013

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2013
Posts
401
Reaction score
90
Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba Mwl. Ezekiah Oluochi amedai kuwa siku 21 ni chache mno kujadili rasimu ya Kanuni za Bunge la Muungano,Hivyo wananchi wasiwe na Hofu kua Bunge Maalumu la Katiba Limetumia Siku Nyingi kwa kutunga Kanuni pekee.Ameongeza kuwa kuna baadhi ya Nchi zimetumia hadi miezi 6 Kutunga kanuni pekee lakini hakutaja kua ni Nchi gani.

Chanzo: Mahojiano kupitia StarTV Kipindi cha MEDANI ZA KISIASA MDA HUU SAA 5:00 TAR 9/3/2014.
 
Anaitwa Ezekiel Oluochi. Sku zote huwa hana jipya. Muacheni afaidi tu hiyo offer ya mkuu wa nchi kwa kuwa puppet wa serikali ndani ya chama cha walimu Tanzania.
 
Kama ni hivyo atwambie pia ni siku ngapi zitahitajika kujadili katiba. Maana karibu nusu ya muda uliopangwa unaishia kutunga kanuni.
 
huwa anachangia kila kitu hata kama hakina maana,ni mtu anayependa publicity
 
Wananchi wasiwe na hofu watu waendelee kuingiza mshiko.
 
Kura siri, mikataba wazi, msimamo ni upi sasa , kweli upinzani Tanzania badoj
 
Tulikuwa hatumjuwi vzr lkn sasa tumemtambuwa,
 
Kwa maoni yake huyo Mwalimu anadhani itawachukuwa siku ngapi kujadili rasimu yote kama kanuni peke yake imachuwa ni kazi ya week 3? Na anakumbuka walipewa muda gani?
 
Huyu jamaa anapenda sana sifa, kwanza ni msaliti namba 2 nyuma ya mkoba sijui kikapu ndani ya chama chao cha walimu, tusitegemee mapya kutoka kwa watu kama hawa wanaoongozwa na njaa zao na si lolote.
 
Ukweli ni kwamba bwana Oluochi ameropoka hiyo kauli yake.

Kwanza sidhani kama ni sahihi kusema kila ambalo limefanywa na nchi zingine na sisi Watanzania tuige. Huo ni upuuzi.

Jambo lingine aelewe kuwa itakuwa ni aibu sana kwao kama wajumbe wa bunge maalumu la katiba kushindwa ku-meet time schedule ya kazi yao. Maana muda waliopewa ni siku si zaidi ya 70, sasa kama siku 21 zinatumika kwenye kanuni huo ni uwendawazimu.
 
Amedai kua Zile siku 70 hazijaanza yani ni mbali kabisa na Siku za Kutunga kanuni.
 
Kama ni hivyo atwambie pia ni siku ngapi zitahitajika kujadili katiba. Maana karibu nusu ya muda uliopangwa unaishia kutunga kanuni.

Amesema kua Zile siku 70 zipo palepale ni tofauti na siku za kutunga kanuni.
 
Amesema kua Zile siku 70 zipo palepale ni tofauti na siku za kutunga kanuni.

Duh, kwa hiyo ile bajeti ya siku 70 ilikuwa kiini macho tu!!? Na lile bunge letu la bajeti litakaa lini tena!!??
 
Back
Top Bottom