Fact Check: Chuo kilichompa udaktari wa heshima Mbunge Musukuma ni cha kitapeli, hakiko authentic

Fact Check: Chuo kilichompa udaktari wa heshima Mbunge Musukuma ni cha kitapeli, hakiko authentic

Kingsmann

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2018
Posts
4,805
Reaction score
17,850
Inasikitisha sana tunapoona viongozi waandamizi wa nchi hasa wabunge wakikubali kununua cheap doctorates kutoka vyuo vya kitapeli(rogue colleges). Hiyo inakupa picha kwamba hawa viongozi wetu hawajui hata kuangalia authenticity wakati kila kitu kipo online.Kwanza hiki sio chuo maana hakina address, hakina majengo na wala hakina makao makuu yanayoeleweka. Ni taasisi ya kijanjajanja tuu iliyoanzishwa na matapeli kwa ajili ya kuwatapeli watu wanaotaka umashuhuri nafuu hasa wa udaktari bila kutumia jasho.

Hiki chuo kilichowapa udaktari wa heshima Mbunge Musukuma na wenzake kina kashfa ya siku nyingi ya kuuza hizi degree za heshima. Ukweli ni kwamba wanauza na sio wanatoa bure ama kulingana na mafanikio uliyonayo katika nyanja husika, wakati vyuo vyenye heshima zake na vinavyotambulika huwa vikitoa degree za heshima basi vinatoa na kiasi cha pesa ambayo kwa hapa Tanzania huwa ni pesa ndefu sana.

musukuma.JPG



musu.jpg


Soma hii habari iliyoandikwa mwaka 2018 na C-HUB MAGAZINE ambapo walielezea namna hiki chuo cha kitapeli kinavyouza hizi degree za heshima kwa waafrika.


"Baadhi ya Wanigeria mashuhuri huko London, ambao wengi wao ni viongozi wa jamii, wanasheria na waigizaji wa Nollywood wamenaswa katika udaktari bandia wa heshima kwani uhalisi wa taasisi hiyo na tuzo zake zimetiliwa shaka.

Heshima hiyo iliyofahamika kwenye jamii mwaka jana imeuza zaidi ya tuzo 20 kwa Wanigeria wengi kati ya mwaka wao wa mwisho na sherehe ya mwaka huu. Wasomi wanaojali walitilia wasiwasi tuzo hizo wakati picha zilipoibuka za wapokeaji wa tuzo ya heshima ya mwaka huu zilikuwa na umuhimu wa kutiliwa shaka. Wakati hadithi hiyo ikiendelea kuibuka, inakadiriwa kwamba waliopokea zawadi walikuwa wamelipa kila mmoja, kiasi cha pauni 2500 (karibu shilingi milioni 8 za kitanzania) kupokea heshima hiyo.

Wasomi wanaendelea kuhoji uhalisi wa shirika linalotoa heshima kama hiyo na kwa nini lazima iwe Wanigeria wengi. Kwa mujibu wa mwanataaluma mmoja, kutokana na kulitazama gauni hilo, cheti ambacho kina mihuri mbalimbali na jina la chuo, mtu yeyote mwenye chembe yoyote ya uungwana atafanya uchunguzi wa kina kabla ya kukubali upuuzi huo.

Chuo hicho, Academy of Universal Global Peace ambacho kinadai kuidhinishwa na serikali ya Uingereza, Marekani, na India pamoja na Umoja wa Mataifa kinasemekana kuanzishwa na 'Mtukufu' wake Dk. Madhu Krishan mwaka wa 1985, ambaye inadaiwa kuwa pia ni Rais wa Asia 'Power Ministries Intl, Inc. Marekani na anashikilia nyadhifa kadhaa katika mashirika mengi ya kimataifa, baina ya serikali. Dai la heshima kwa jina la mwanzilishi linaendelea na kuendelea, hata hivyo, swali ambalo bado halijajibiwa ni je, ni chuo kikuu gani kimeidhinisha taasisi hii kutoa udaktari wa heshima?

Inakuwa mbaya zaidi kadri maelezo yanavyojitokeza. Ingawa chuo kikuu hicho kinadai kuwa na uhusiano na Umoja wa Mataifa, Tume ya Athari za Kielimu za Umoja wa Mataifa, Tume ya Ulaya, Power Ministries International na Shirika la Amani Ulimwenguni, hata hivyo madai haya yaligunduliwa kuwa sio kweli. Inayoitwa AUGP pia haihusiani na Tume ya Ruzuku ya Chuo Kikuu (UGC) au taasisi yoyote ya kitaaluma ya India.

AUGP, inadai kuwa na makao yake makuu Amerika, hata hivyo haijafahamika ni wapi Marekani makao makuu yapo, wanadai sasa yamehamishiwa Chennai. Mwenyekiti wa Kimataifa wa AUGP, Dk Madhu Krishan, husafiri kimataifa. Hapo awali alikuwa anakaa Amerika kwa miaka kadhaa lakini sasa ana makazi huko Chennai, kwa hivyo makao makuu yako Chennai kwa sasa.

Wakati uchunguzi wetu ukiendelea, ukweli unabakia kuwa, sifa za "chuo" kinachotoa udaktari huu, ziko chini ya wingu la tuhuma. Kufuatia baadhi ya machapisho yao ya mitandao ya kijamii ambayo yanadaiwa kuwa sehemu ya Chuo Kikuu cha Westminster, tumefikia Chuo Kikuu cha London kwa maoni kuhusu uhusiano wao na AUGP na ikiwa wanajua kuhusu udaktari unaouzwa."


AUGP.png


AUGP SCAM.png




20180731_114409_0001.png



Chuo Kikuu kilichopo Japan kinachoitwa United Nations University kiliwahi kukanusha pia madai ya AUGP baada ya kuadai wana ubia kati yao. Hii yote inazidi kuthibitisha kwamba hii ni taasis ya kitapeli.


UNU.JPG



Hakuna anayepinga hawa waheshimiwa wetu kupata hizo degree za heshima, ila ziwe zinatoka kwenye taasisi zenye heshima na halali. Hizi degree za heshima zinazitolewa na mtu mmoja, tena amesafiri kutoka huko alipo eti kuja kutoa udaktari wa heshima ni utapeli na ni aibu kwa taifa kuwa na viongozi wa namna hii.

Rais Kikwete mwaka 2015 alitunukiwa udaktari wa heshima katika sheria kutoka Chuo Kikuu cha Newcastle cha nchini Australia, na ukiangalia authenticity yake na hii ya akina Musukuma utagundua ni mbingu na ardhi.


KikweteAus.JPG



KikweteAU.JPG



Kikwete.JPG





Kikwetee.JPG




KikweteSalma.JPG




KikweteNewcastle.JPG


Soma zaidi hapa: Chhattisgarh minister laps up fake honour
 
Na wanaouziwa hizo PhD fake ni Waafrica tu. Hii ngozi nyeusi ina laana
 
Back
Top Bottom