Facts chache kuhusu birthday yangu

smarte_r

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2013
Posts
4,564
Reaction score
12,014
Mwenyezi Mungu akipenda inshallah mwezi wa 12(tarehe sitaji) mwaka huu(2019), nitaingia rasmi katika kundi la wahenga. nitatimiza miaka kadhaa ya kuzaliwa kwangu.

kiufupi uhenga sio jambo la kufanyia dhihaka bali ni kitu la kujivunia kwa sababu sio watu wote wa kizazi changu wamebahatika kufika umri ambao mimi nimefika mpaka sasa.

mwaka huu pekee, nimezika rafiki zangu sita ambao wote walizaliwa katika muongo mmoja sawa na mimi.

binafsi najihisi mwenye bahati kuzaliwa katika kipindi ambacho wengine hukiita golden era. ni golden ara kwasababu ni nyakati ambazo dunia ilishudia mapinduzi mengi ya kimziki, sayansi, siasa, tamaduni nk.

na hizi ndio baadhi ya facts kuhusu birthday yangu.

nilizaliwa siku ya ijumaa mida ya alasiri katika moja ya hospital kubwa sana ambayo inapatikana ndani ya jiji moja maarufu hapa east africa.

kwa wale wanaomini katika masuala ya unajimu, nyota yangu ni mshale(sagittarius)

kama nitafika salama au hai katika siku ya birthday yangu, basi nitakuwa nimeishi duniani siku 14,151. pia nitakuwa nimeishi masaa 339,624.

siku niliyozaliwa, rais wa taifa kubwa duniani la marekani alikuwa ni jimmy carter kupitia chama cha democrat.

masaa machache baada kuzaliwa kwangu, mwanamziki nguli wa miondoko ya country duniani, kenny rogers alikuwa anatamba na kibao chake kitamu sana cha lady.

wakati nazaliwa, secret valley ilikuwa ndio movie iliyokuwa inaongoza kwa kutazamwa zaidi duniani kwenye kumbi za cinema.

kwa wale wapenda soka, wiki moja baada ya kuzaliwa kwangu, club ya liverpool iliongoza kwa idadi ya magoli mbele ya aston villa katika division ya kwanza ya ligi kuu ya england.

wakati nazaliwa, john d. rockefeller
ndio alikuwa mtu tajiri zaidi duniani.

nitaongeza facts zingine kadili nitakavyopata mda.
 
Sawa mhenga wetu, Karibu sana kwenye umri wa mtu mzima. Natumaini unakula uwekezaji wako muda huu.
 
hongera mkuu kwa kukaribia uhengani more life more blessing
 
Unatimiza 40 bado kijana.
Ruge aliondoka na 49 mkawa mnasema bado kijana mdogo sana
 
hivi utu uzima ni miaka mingapi ndugu zangu maana hii ni fikrishi pia
 
Umeshindwa nini kusema umezaliwa mwaka 1981.Na unafikisha miaka 38
 
kila la heri uzima tu ndo muhimu....

Age is just a number
 
kwa uliyoyaandika upo karibu kufa trust me
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…