Facts kuhusu sisimizi πŸ“

-> Sisimizi wana nguvu za ajabu sana.

Wanaweza kubeba vitu hata vilivyowazidi uzito na ukubwa hata mara 10 hadi 50 zaidi ya umbo na uzito wake. Kiwango cha uzito ambao sisimizi anaweza kubeba inategemea na jamii yake. Mfano jamii ya weaver wanaopatikana bara la Asia , wanaweza kubeba hadi Kitu kizito mara 100 ya mwili wao.
 
Maisha ya sisimizi ni ya kitaasisi.
Sisimizi, Mchwa, Siafu, Chungu chungu, Nyuki nk wanaishi kwenye taasisi imara.
Taasisi zao zina watafuta chakula, walinzi nk.
Umoja wao ndiyo unaowapa nguvu kubeba vyakula vizito na kukabiliana na maadui zao.

Nje ya taasisi hizo wadudu hao wanaangamia haraka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…