The beginning of the end...
Siku kama ya leo mwaka 2012 klabu ya AC Milan iliwaaga nyota wake wapatao sita ambao waliitumikia timu hio kwa mahaba yaliotukuka.
Ilikuwa ni katika dimba la Sansiro ambapo ni nyumbani kwa miamba hio, tulishuhudia Kuagwa kwa nyota kama Gianluca Zambrotta , Pippo Inzaghi, General Gattuso, Dikteta wa kiungo Mark van Bommel, Sandro the Captain Alesandro Nesta and Uncle Clarence Seedorf.
Hatimae Milan ikawaaga wakongwe hawa kwa majonzi ya kufikia ukomo wa kuitumikia klabu hio lakini kwa furaha ya kubeba ubingwa wa nchi hio maarufu kama Scudeto.
Kwa sasa Nyota hawa wamesambaa Duniani kote huku wakitoa huduma ya ukocha katika vilabu mbalimbali.