Heparin
JF-Expert Member
- Sep 24, 2021
- 242
- 1,141
"Kuna kitu naona kinapita mtandaoni ninafikiri cha katibu wa wilaya fulani, watu wanapiga kelele sana oooh ushindi ni lazima, sijui hivi sijui vile, hiyo inajulikana mbona! Ushindi wa Chama Cha Mapinduzi ni lazima, na CCM haina mpango wa kutoka madarakani kesho, kesho kutwa na miaka huko mbele. Sasa hatuwezi kuona aibu, sisi viongozi sisi wanachama kusema kwamba ushindi ni lazima, na inaendana na mipango, mikakati na mambo mengine yanayofanana na hayo, kwa hiyo hatuwezi kusita kuyasemea haya ya Chama Cha Mapinduzi kwa sababu ndiyo tunayoishi nayo"- Maganya.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Fadhili Maganya akizungumza na walimu Makada wa CCM mkoani Iringa.
Kauli hii ni mwendelezo wa kauli tata zinazotolewa na viongozi wa CCM kuhusiana na michakato ya uongozi na chaguzi za Tanzania.
Soma pia kauli zingine hapa: