Strong ladg
Senior Member
- Jul 15, 2021
- 170
- 445
Jeshi la Mali limefanikiwa kumuua kiongozi wa juu wa kundi la kigaidi linalowashambulia raia katika eneo la kaskazini la nchi huyo.
Katika taarifa iliyotolewa kupitia televisheni ya taifa, jeshi la Mali limesema lilifanikiwa kumuua Fahad Ag Al Mahmoud pamoja na viongozi wengine muhimu saba mnamo tarehe 1 Disemba 2024 baada ya kuwashambulia kwa droni.
Jeshi la Mali limefanikiwa kupata ushindi dhidi ya magaidi tangu lichukue madaraka baada ya mapinduzi. Ushindi muhimu na unaokumbukwa zaidi ni kukombolewa kwa mji wa Kidal mnamo Novemba 2023 ambao ulikuwa umeshikiliwa na magaidi kwa takribani miaka 10.
Majeshi ya Ufaransa pamoja na yale ya kulinda amani ya umoja wa mataifa hayakufanikiwa kupata ushindi dhidi ya magaidi licha ya kuwepo nchini Mali kwa karibu miaka kumi.
Picha: Kiongozi aliyeuwawa.
CHANZO: Shirika la habari la Mali( ORTM)