Fahamu asili ya jina la Kitimoto

Mlenge

R I P
Joined
Oct 31, 2006
Posts
2,125
Reaction score
2,306
Mnamo mwaka 1995 hivi, palikuwa na uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi nchini Tanzania. Uchaguzi ule ulikuwa na ushindani. Nyakati hizo, runinga ndio zinaingia Tanzania-bara. Palikuwa ni kipindi kimoja cha mahojiano, kilijipatia umashuhuri sana. Kilikuwa kinaitwa "Kiti Moto". Mtangazaji, Pascal Mayalla , runinga ya DTV.

Wakati huohuo, walaji wa nyama-choma ya nguruwe walikuwa wakikutanika katika maeneo yao ya kujidai, na kujipatia kitoweo, huku wakiendeleza mijadala motomoto ya mwaka wa uchaguzi. Kuonyesha namna mijadala yao ilivyokuwa muhimu, waliita mikutaniko yao "Kiti Moto", jina ambalo lilipitia transmutation na kuwa kitimoto.

Jina la kitimoto likafunika majina mengine ya zamani, kama vile mbuzi-katoliki au Mkuu wa Meza.

Historia kwa manufaa ya vijana wa leo.
 
The kiti was moto.
 
kile kipindi kilikuwa kizuri sana! wakati huo Mrema ameshika siasa za Tanzania.

Pascall Malaya alijijengea umaarufu sana kipindi hicho sijui kwa nn kapotea kwenye ulingo wa habari na utangazaji mzuri.
 
Nakumbuka kipindi kilifungiwa baada ya kumualika Kakobe kwenye mahojiano
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…