Fàhamu hatua za kufata kupata msamaha wa kodi kwa watumishi unapoagiza gari nje ya nchi

Godface

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2020
Posts
211
Reaction score
561
Kutokana na watu wengi kutokuwa na elimu hasa ya vyombo vya moto na wengine wakitamani kumiliki gari ,ukiwa kama mtumishi wa umma kuna utaratibu upo umewekwa wazi leo nakumulikia mwanga karibu maelezo kuhusu taratibu muhimu ambazo watumishi wa umma wanatakiwa kuzingatia wanapohitaji wanapohitaji msamaha wa ushuru kwenye vyombo vya usafri (Magari na pikipiki).

Maelezo haya yanazingatia sheria husika za kodi pamoja na Matangazo ya Serikali yaani GN. Na. 520 na 522 za mwaka 1995.

2.0 Lengo la msamaha wa ushuru kwa watumishi wa umma Lengo la msamaha wa ushuru kwenye vyombo vya usafri kwa watumishi wa umma ni hatua za makusudi zilizochukuliwa na Serikali katika kuboresha ufanisi katika utendaji kazi. kwa kuwasaidia usafri hususani kwenda kazini na kurudi nyumbani kwao.

3.0 Maana ya Mtumishi wa Umma.Mtumishi wa umma ni mtu ambaye anashika ofsi ya umma kwa kuteuliwa, kuchaguliwa au yuko kwenye mkataba wa ajira katika Serikali Kuu, Serikali za Mitaa, Taasisi na wakala za Serikali ikiwa ni pamoja na Mashirika ya Umma.

Shirika la umma ni lile ambalo asilimia 50% au zaidi ya matumizi yake yanatokana na ruzuku ya Serikali. Asasi na taasisi zingine zisizo za kiserikali hazihusiki na utaratibu huu kwa mujibu wa sheria. Mtumishi wa umma ambaye kwa mujibu wa sheria anafaidika na msamaha wa ushuru katika vyombo vya usafri ni yule mwenye ngazi ya mshahara ya TGS D au zaidi kwa upande wa Serikali au inayolingana na hiyo kwa upande wa Taasisi zingine za Serikali na mashirika ya umma.

4.0 Aina ya vyombo vya usafri vinavyohusika na msamaha Kwa mujibu wa sheria, vyombo vya usafri vinavyohusika na msamaha huu bila kujali kama chombo kimenunuliwa hapa nchini au nje ni hivi vifuatavyo:- [emoji419](a) Magari [emoji419]•Magari madogo aina ya saloon. [emoji419]•Magari aina ya pick – up yenye uwezo wa kubeba [emoji419]mzigo usiozidi uzito wa tani mbili. Magari mengine ambayo hayabebi zaidi ya abiria tisa.•Gari lenye ujazo wa injini usiozidi 3,000. •Gari lenye umri chini ya miaka kumi tangu lilipotengenezwa bila kujali miezi.(b)Pikipiki za aina zote. [emoji3533]

5.0 Ushuru unaosamehewaMtumishi wa umma ambaye ametimiza masharti yote yanayotakiwa kwa mujibu washeria na taratibu zilizowekwa anasamehewa kulipa ushuru wa forodha (import duty) tu. Kodi na ada zingine kama Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), ushuru wa bidhaa (Excise duty) na ada za usajili atatakiwa kulipa. Zingatia:Mtumishi wa umma akinunua gari lenye umri wa miaka kumi au zaidi toka kutengenezwa hatapata msamaha kabisa. [emoji3533]

6.0Masharti ya kuzingatia kwa mtumishi wa umma. Ikumbukwe kuwa Serikali ina nia njema kwa watumishi wake kutoa upendeleo kwao kwa njia ya msamaha wa ushuru wa forodha kwenye vyombo vya usafri. Hivyo ni vema masharti yafuatayo yakazingatiwa: -

(a) Kibali cha msamaha kinachotolewa ni kwa ajili ya mtumishi wa umma anayehusika na sio mtu mwingine yoyote. Ni kosa kisheria kwa mtu yeyote asiye husika kufaidika na msamaha huu, na wala chombo cha usafri chenye msamaha wa ushuru hakiruhusiwi kutumika kwa shughuli za biashara.

(b) Msamaha utasitishwa na ushuru uliosamehewa utatakiwa kulipwa mara moja iwapo mtumishi wa umma ataacha kuwa mtumishi wa umma kabla ya miaka minne kupita tangu tarehe ya kupewa msamaha, au [emoji91] iwapo atahamisha umiliki au kuuza chombo hicho cha usafri kwa mtu mwingine.[emoji91]

(c) Msamaha utatatolewa kwa chombo kimoja tu cha usafri katika kipindi cha miaka minne. Baada ya muda huo kupita, mtumishi wa umma anaruhusiwa kuomba msamaha mwingine, lakini ni lazima ushuru ulipwe kwa chombo cha usafri cha zamani kwa kiwango cha uthaminishaji kama ilivyoainishwa na Idara ya Forodha. Thamani itakayotumika kukokotoa kodi husika ni thamani ya chombo hicho wakati kilipoingia nchini; mmiliki anapaswa kutunza nyaraka zote za chombo hicho cha usafri vizuri.

Hivyo basi, ili mtumishi wa umma astahili kupewa msamaha mwingine baada ya miaka minne kupita ni lazima aambatanishe maombi yake na stakabadhi ya malipo ya ushuru kwa ajili ya chombo cha usafri cha zamani toka TRA [emoji3533]

7.0 Watumishi wa umma ambao wako masomoni Mtumishi wa umma ambaye anaendelea na masomo yake hapa nchini au nje ya nchi haruhusiwi kupewa msamaha wa ushuru hadi pale atakapomaliza masomo yake na akaendelea na utumishi wa umma.Isipokuwa mtumishi wa umma anayesoma nje ya nchi anaweza kutumia msamaha wa mkazi anayerejea nchini(returning resident) iwapo ameishi nje ya nchi miezi kumi na mbili au zaidi na chombo hicho cha usafri amekimiliki kwa miezi kumi na mbili au zaidi.

8.0 Taratibu muhimu za kufuataKujaza fomu ya maombi (Nakala nne) ambayo ni lazima iwe na viambatanisho vifuatavyo:-
(a) Magari yanayoagizwa toka nje nchi
i. Barua ya utambulisho toka kwa mwajiri,
ii. Salary Slip ya mwezi wa karibu,
iii. Barua ya kuajiriwa kazini/Barua ya kupandishwa Cheo,
iv. Nakala ya kitambulisho cha kazi,
v. Anatakiwa pia kuambatanisha picha nne (4) za “passport size “kwenye fomu ya maombi,
vi. Kuambatanisha namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN),
vii. Kumbukumbu za ununuzi au uingizaji wa chombo husika cha usafri hapa nchini. maelezo yote kwa kina na vielelezo vyote vinavyohusiana na gari mfano namba ya Injini na ya Chasis, Ujazo wa Injini (cc), CIF value nk kabla ya kupeleka maombi yako TRA.“

Pamoja TunajengaTaifa Letu” Source (TRA WEBSITE ) KAMA UNASWALI AU HAUJAELEWA WASILIANA NA TRA KWA ANWANI ZIFUATAZO Email pepe: info@tra.go.tz Simu zao call center 0800110016 watumiaji wa TTCL NA VODA +255 786 800 000 Kwa Watumiaji wa Airtel +255 713 800 333 Kwa Watumiaji wa Tigo Niwatakie asubuhi njema Mwisho niwatakie Asubuhi njemaView attachment Msamaha wa ushuru kwa vyombo vya usafiri kwa watumishi wa umma.pdf sent from HUAWEI
 
Hii ni nzuri japo bado sio mtumishi wa umma! Ila kwa mf km anataka kuchukua ist akisamehewa atalipia mil 5 badala ya mil 7 au ukiangalia pichani hapo! Na je akitakiwa nunua gari mbili haitakubalika au
20201021_100135.jpg
 
Hii ni nzuri japo bado sio mtumishi wa umma! Ila kwa mf km anataka kuchukua ist akisamehewa atalipia mil 5 badala ya mil 7 au ukiangalia pichani hapo! Na je akitakiwa nunua gari mbili haitakubalika auView attachment 1606999
Unaruhusiwa gari moja tu mpk miaka minne ipite tena ndio unaweza kununua jingine

sent from HUAWEI
 
Kutokana na watu wengi kutokuwa na elimu hasa ya vyombo vya moto na wengine wakitamani kumiliki gari ,ukiwa kama mtumishi wa umma kuna utaratibu upo umewekwa wazi leo nakumulikia mwanga karibu maelezo kuhusu taratibu muhimu ambazo watumishi wa umma wanatakiwa kuzingatia wanapohitaji wanapohitaji msamaha wa ushuru kwenye vyombo vya usafri (Magari na pikipiki).

Maelezo haya yanazingatia sheria husika za kodi pamoja na Matangazo ya Serikali yaani GN. Na. 520 na 522 za mwaka 1995.

2.0 Lengo la msamaha wa ushuru kwa watumishi wa umma Lengo la msamaha wa ushuru kwenye vyombo vya usafri kwa watumishi wa umma ni hatua za makusudi zilizochukuliwa na Serikali katika kuboresha ufanisi katika utendaji kazi. kwa kuwasaidia usafri hususani kwenda kazini na kurudi nyumbani kwao.

3.0 Maana ya Mtumishi wa Umma.Mtumishi wa umma ni mtu ambaye anashika ofsi ya umma kwa kuteuliwa, kuchaguliwa au yuko kwenye mkataba wa ajira katika Serikali Kuu, Serikali za Mitaa, Taasisi na wakala za Serikali ikiwa ni pamoja na Mashirika ya Umma.

Shirika la umma ni lile ambalo asilimia 50% au zaidi ya matumizi yake yanatokana na ruzuku ya Serikali. Asasi na taasisi zingine zisizo za kiserikali hazihusiki na utaratibu huu kwa mujibu wa sheria. Mtumishi wa umma ambaye kwa mujibu wa sheria anafaidika na msamaha wa ushuru katika vyombo vya usafri ni yule mwenye ngazi ya mshahara ya TGS D au zaidi kwa upande wa Serikali au inayolingana na hiyo kwa upande wa Taasisi zingine za Serikali na mashirika ya umma.

4.0 Aina ya vyombo vya usafri vinavyohusika na msamaha Kwa mujibu wa sheria, vyombo vya usafri vinavyohusika na msamaha huu bila kujali kama chombo kimenunuliwa hapa nchini au nje ni hivi vifuatavyo:- [emoji419](a) Magari [emoji419]•Magari madogo aina ya saloon. [emoji419]•Magari aina ya pick – up yenye uwezo wa kubeba [emoji419]mzigo usiozidi uzito wa tani mbili. Magari mengine ambayo hayabebi zaidi ya abiria tisa.•Gari lenye ujazo wa injini usiozidi 3,000. •Gari lenye umri chini ya miaka kumi tangu lilipotengenezwa bila kujali miezi.(b)Pikipiki za aina zote. [emoji3533]

5.0 Ushuru unaosamehewaMtumishi wa umma ambaye ametimiza masharti yote yanayotakiwa kwa mujibu washeria na taratibu zilizowekwa anasamehewa kulipa ushuru wa forodha (import duty) tu. Kodi na ada zingine kama Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), ushuru wa bidhaa (Excise duty) na ada za usajili atatakiwa kulipa. Zingatia:Mtumishi wa umma akinunua gari lenye umri wa miaka kumi au zaidi toka kutengenezwa hatapata msamaha kabisa. [emoji3533]

6.0Masharti ya kuzingatia kwa mtumishi wa umma. Ikumbukwe kuwa Serikali ina nia njema kwa watumishi wake kutoa upendeleo kwao kwa njia ya msamaha wa ushuru wa forodha kwenye vyombo vya usafri. Hivyo ni vema masharti yafuatayo yakazingatiwa: -

(a) Kibali cha msamaha kinachotolewa ni kwa ajili ya mtumishi wa umma anayehusika na sio mtu mwingine yoyote. Ni kosa kisheria kwa mtu yeyote asiye husika kufaidika na msamaha huu, na wala chombo cha usafri chenye msamaha wa ushuru hakiruhusiwi kutumika kwa shughuli za biashara.

(b) Msamaha utasitishwa na ushuru uliosamehewa utatakiwa kulipwa mara moja iwapo mtumishi wa umma ataacha kuwa mtumishi wa umma kabla ya miaka minne kupita tangu tarehe ya kupewa msamaha, au [emoji91] iwapo atahamisha umiliki au kuuza chombo hicho cha usafri kwa mtu mwingine.[emoji91]

(c) Msamaha utatatolewa kwa chombo kimoja tu cha usafri katika kipindi cha miaka minne. Baada ya muda huo kupita, mtumishi wa umma anaruhusiwa kuomba msamaha mwingine, lakini ni lazima ushuru ulipwe kwa chombo cha usafri cha zamani kwa kiwango cha uthaminishaji kama ilivyoainishwa na Idara ya Forodha. Thamani itakayotumika kukokotoa kodi husika ni thamani ya chombo hicho wakati kilipoingia nchini; mmiliki anapaswa kutunza nyaraka zote za chombo hicho cha usafri vizuri.

Hivyo basi, ili mtumishi wa umma astahili kupewa msamaha mwingine baada ya miaka minne kupita ni lazima aambatanishe maombi yake na stakabadhi ya malipo ya ushuru kwa ajili ya chombo cha usafri cha zamani toka TRA [emoji3533]

7.0 Watumishi wa umma ambao wako masomoni Mtumishi wa umma ambaye anaendelea na masomo yake hapa nchini au nje ya nchi haruhusiwi kupewa msamaha wa ushuru hadi pale atakapomaliza masomo yake na akaendelea na utumishi wa umma.Isipokuwa mtumishi wa umma anayesoma nje ya nchi anaweza kutumia msamaha wa mkazi anayerejea nchini(returning resident) iwapo ameishi nje ya nchi miezi kumi na mbili au zaidi na chombo hicho cha usafri amekimiliki kwa miezi kumi na mbili au zaidi.

8.0 Taratibu muhimu za kufuataKujaza fomu ya maombi (Nakala nne) ambayo ni lazima iwe na viambatanisho vifuatavyo:-
(a) Magari yanayoagizwa toka nje nchi
i. Barua ya utambulisho toka kwa mwajiri,
ii. Salary Slip ya mwezi wa karibu,
iii. Barua ya kuajiriwa kazini/Barua ya kupandishwa Cheo,
iv. Nakala ya kitambulisho cha kazi,
v. Anatakiwa pia kuambatanisha picha nne (4) za “passport size “kwenye fomu ya maombi,
vi. Kuambatanisha namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN),
vii. Kumbukumbu za ununuzi au uingizaji wa chombo husika cha usafri hapa nchini. maelezo yote kwa kina na vielelezo vyote vinavyohusiana na gari mfano namba ya Injini na ya Chasis, Ujazo wa Injini (cc), CIF value nk kabla ya kupeleka maombi yako TRA.“

Pamoja TunajengaTaifa Letu” Source (TRA WEBSITE ) KAMA UNASWALI AU HAUJAELEWA WASILIANA NA TRA KWA ANWANI ZIFUATAZO Email pepe: info@tra.go.tz Simu zao call center 0800110016 watumiaji wa TTCL NA VODA +255 786 800 000 Kwa Watumiaji wa Airtel +255 713 800 333 Kwa Watumiaji wa Tigo Niwatakie asubuhi njema Mwisho niwatakie Asubuhi njemaView attachment 1606946 sent from HUAWEI
wangesamehe kodi zote zinazohusiana na kuagiza gari ingekua vzr zaidi
 
Hii ni nzuri japo bado sio mtumishi wa umma! Ila kwa mf km anataka kuchukua ist akisamehewa atalipia mil 5 badala ya mil 7 au ukiangalia pichani hapo! Na je akitakiwa nunua gari mbili haitakubalika auView attachment 1606999
Hii valuation calculator huwa iko hivyo hata kama gari imenunuliwa chini ya amount hiyo ya calculator???

Mfano unakuta CIF ni dola 6,500 halafu evaluation calculator inasoma CIF 7,500.
 
Back
Top Bottom