JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Mgombea Kujitoa
Kwa mujibu wa Kifungu cha 48 cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, Mgombea anaweza kujitoa kugombea kwa kuwasilisha kwa Msimamizi wa Uchaguzi yeye mwenyewe barua ya kujitoa pamoja na tamko la kujitoa alilotoa mbele ya Hakimu.
Nakala ya barua ya kujitoa ipelekwe Tawi la Chama kilichomdhamini kabla ya saa kumi na mbili kamili (12:00) jioni, siku inayofuata baada ya siku ya uteuzi.
Endapo Mgombea atajitoa baada ya muda uliowekwa Kisheria atapoteza dhamana ya fedha alizoweka kwa Msimamizi wa Uchaguzi. Kwa mujibu wa kanuni ya 34(2)(b) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge za mwaka 2020 Mgombea akijitoa baada ya siku ya Uteuzi, Chama chake hakitapata nafasi ya kuweka Mgombea mwingine.
Kufariki Kwa Mgombea
Kwa mujibu wa Kifungu cha 49 cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, endapo Msimamizi wa Uchaguzi atajiridhisha kuwa Mgombea yeyote amefariki baada ya saa kumi kamili (10:00) jioni ya siku ya Uteuzi na kabla ya muda wa mwisho wa upigaji kura, atasitisha Uchaguzi katika Jimbo husika na kutoa taarifa Tume ili ipange tarehe nyingine ya Uteuzi wa Mgombea wa Chama ambacho Mgombea wake amefariki.
Kutokuwepo Kwa Mgombea
Kwa mujibu wa Kifungu cha 50 cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, endapo baada ya Uteuzi hapatakuwa na Mgombea yeyote kwa sababu ya Kifo, Kujitoa, au sababu nyingine yoyote kama vile kutojitokeza kwa Wagombea, Msimamizi wa Uchaguzi ataitaarifu Tume ili isitishe Uchaguzi katika Jimbo husika na kupanga tarehe nyingine ya Uteuzi wa Wagombea kwa mujibu wa Sheria

Upvote
2