KANYEGELO
JF-Expert Member
- Nov 12, 2019
- 2,238
- 4,885
Kuna somo muhimu sana hapa:
ALLY HASSAN MWINYI, BABA WA HEKIMA!
Alipojiuzulu uwaziri wa mambo ya ndani ya nchi mwaka 1983 (kama sijakosea) nafasi yake aliteuliwa mzee mmoja kutoka Zanzibar anaitwa Mzee Natepe kushika uwaziri wa mambo ya ndani ya nchi.
Natepe alipoingia tu ofisini alimtaka waziri aliemtangulia kutoka katika nyumba ya waziri ili yeye aweze kukaa hapo kama waziri.
Ilikuwa shida kidogo maana Waziri alieondoka bado alikuwa anatafuta makazi lakini alitakiwa haraka kutoka na Natepe.
Ikampasa Mzee Mwinyi kutoka kwa haraka na siku anatoka pale nyumbani alikuwa amenunua mabati 150 na mifuko ya saruji 100 ya kwake, wala siyo mali ya Serikali.
Natepe alimkatalia kuvichukua akidai ni mali ya serikali; kweli Mzee Mwinyi akaviacha, akaondoka.
Baada ya miezi kadhaa tu Mzee Mwinyi akateuliwa kuwa Rais Zanzibar Natepe wakati anajifikiria jinsi ya kwenda kumpongeza na kumuomba radhi kwa aliyomfanyia, kabla ya kufikiria njia Mzee Mwinyi akaletwa bara mwaka 1985 kama Rais wa JMT.
Hapa sasa Natepe akajua kazi hana na atatimuliwa haraka iwezekanavyo tena na kutengwa na nyadhifa za JMT kwakuwa kuna mabaya ya wazi na ya sirini aliyomtendea Mzee Mwinyi.
Mzee Mwinyi baada tu ya kuapishwa kuwa Rais wa JMT wakati anateua Baraza la Mawaziri, akamteua tena Natepe kuwa waziri pale pale mambo ya ndani.
Siku ya kumuapisha akamwambia Natepe, siyo kwamba nakupenda sana, hapana, ila napenda kazi yako unavyofanya. Endelea kufanya kazi.
Siku moja Mzee Mwinyi yupo ikulu kapumzika, akaona malori yanaingia na akaambiwa mzigo wako huu Mh. Rais , akashtuka mbona sijaagiza kitu mie?
Ndipo akaambiwa umetoka kwa Natepe. Mzee Mwinyi akacheka sana akawaambia wasaidizi wake shusheni mabati 150 na saruji 100 hizo ndio haki yangu, zingine mrudishieni tu.
Hapa kuna masomo makubwa matatu. Vema viongozi wetu wa sasa wakajipambanua kwayo ili twende kwa weledi na umakini sana. Hata kwetu sisi wanadamu ni somo zuri sana la kujifunza.
Pia, soma:
www.jamiiforums.com

Kanusho la Taarifa yenye kichwa kinachosema "Kuna somo muhimu sana hapa:-Ally Hassan Mwinyi Baba wa hekima"
Familia ya Abdallah Saidi Natepe, inapenda kuutarifu umma kuwa habari zinazoenezwa kwenye mitandao ya kijamii na mtu anaejifanya kuwa anaelimisha kwa makala yake yasemayo "Kuna somo muhimu sana hapa " hazina ukweli wowote na zinafaa kupuuzwa. Mwandishi wa habari hii kwa makusudi au kwa kutokuwa...
Legacy ya Rais Ali Hassan Mwinyi (91 years) ni nini?
Rais mtaafu Mzee ALI HASSAN MWINYI ambaye nadhani ki historia ni mmoja ya watu wachache sana duniani ambao waliwahi kuwa rais wa nchi mbili tofauti. Al Hajj Mwinyi aliwahi kuwa Rais wa Zanzibar na Tanzania pia leo ametimiza miaka 91 toka azaliwe. Je GREAT THINKERS wa JAMIIFORUMS mnaweza...