Amavubi
JF-Expert Member
- Dec 9, 2010
- 30,156
- 13,258
HISTORIA YA TOM MBOYA WA KENYA (1930-1969).
Moja ya matukio ya awali kabisa katika historia ya Afrika huru lilimpata aliyekuwa Waziri wa Mipango, Uchumi na Maendeleo wa Kenya Tom Mboya, takribani miaka 48 iliyopita. Ilikuwa ni siku ya jumamosi ya Julai 5, 1969 majira ya mchana akitoka katika duka moja la dawa lililokuwepo katikati ya jiji la Nairobi, Tom Mboya alipigwa risasi kadhaa na kufariki papohapo na mtu ambaye baadaye alikuja kujulikana kama Nahashon Isaac Njenga. Tom Mboya alikuwa ni mwanasiasa maarufu zaidi wakati huo na pia mmoja ya waasisi wa Chama cha Kenya African National Union (Kanu).
Thomas Joseph Odhiambo Mboya ‘Tom Mboya’, Mboya alizaliwa Agosti 15, 1930 katika eneo maarufu la ‘Kilima Mbogo’ karibu na Mji wa Thika, Maeneo hayo yalitambulika kama White Highlands wakati wa kabla ya uhuru wa Kenya. Baba yake Tom alikuwa ni mwangalizi wa mashamba ya katani katika eneo hilo la ‘Kilima Mbogo’.
Mnamo Mwaka 1942, Tom Mboya alijiunga na Shule ya Sekondari ya St Mary's(Yala) iliyopo katika jimbo la sasa la Nyanza. Shuleni alionekana mwenye nidhamu na uwezo wa hali ya juu katika masomo, Mwaka wa 1946, aliendelea na masomo yake katika taasisi ya Holy Ghost College ambapo alifaulu vizuri mitihani ya ‘Cambridge School Certificate’ .
Mwaka wa 1948, alijiunga chuo cha wakaguzi wa afya, kinachoitwa Royal Sanitary Institute's Medical Training School for Sanitary Inspectors jijini Nairobi, alifuzu na kupata ufadhili wa masomo(scholarship) toka Chama cha wafanyakazi cha Uingereza Britain's Trades Union Congress mwaka 1955 kusoma katika chuo cha Ruskin College, kilichopo Oxford.
Alirejea Kenya mwaka 1956, kipindi ambacho serikali ya kikoloni ilikuwa inapambana na vuguvugu la MauMau ambalo lilikuwa linashambulia likitaka Wazungu waondoke katika ardhi yao na kutoa uhuru kwa nchi ya Kenya. Alipoajiriwa kwenye Halmashauri ya Jiji la Nairobi, haraka alijiunga na Chama cha Wafanyakazi (African Staff Association) na baadae kuchaguliwa kuwa rais wa chama hicho ambacho kikaitwa Kenya Local Government Workers Union(KLGWU). Huu ulikuwa mwanzo wa Tom Mboya kujiingiza katika siasa. Walishirikiana kwa karibu na Rashidi Mfaume Kawawa ambaye alikuwa ni kiongozi wa vyama vya wafanyakazi nchini Tanganyika(Tanzania), Kwa wakati huo Vyama Vya Wafanyakazi(Trade Unions) vilikuwa na nguvu kubwa sana.
Alichaguliwa katika bunge ambalo lilikuwa na wabunge 8 tu Waafrika kati ya wabunge 50, Tom Mboya alipeleka miswaada mizito ya kutaka Waafrika zaidi waongezwe kwenye Bunge. Hakuridhishwa na jinsi Bunge hilo lilivyokuwa likiendeshwa, Mwaka 1957, alijihuzulu nafasi hiyo ya ubunge na kuanzisha chama chake mwenyewe kilichoitwa People's Congress Party(WCP)
Miaka hiyo alijijengea heshima kubwa ndani ya Afrika, alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa mkutano wa Waafrika ( All-African Peoples� Conference) nchini Ghana, ambao uliitishwa na Kwame Nkrumah ambaye alikuwa raisi wa Kwanza wa Ghana. Wakati huo Mboya alikuwa na umri wa miaka 28 tu.
Tom Mboya aliamini kuwa Afrika haiwezi kuendelea bila kuwa na vijana wenye elimu bora, Hivyo Mnamo mwaka 1959, alianzisha mchakato wa kupeleka Waafrika kusoma nchini Marekani, ambapo wanafunzi 81 walifaidika kwa mwaka wa Kwanza. Inasemekana pia alimsaidia Barack Obama Sir, baba wa Barack Obama, Rais mtaafu wa Marekani, kupata nafasi ya kusoma Marekani na walikuwa rafiki wakubwa. Zoezi hilo la Mboya zimvutia mno Rais John Kennedy wa Marekani mwaka 1960, kuongeza pia wanafunzi kutoka Uganda, Tanganyika (Tanzania) na Zanzibar, Rhodesia ya Kaskazini (ambayo sasa ni Zambia) Rhodesia ya Kusini (sasa ni Zimbabwe) na Nyasaland ambayo sasa ni Malawi. Mradi huo uliwezesha wanafunzi 230 wa Afrika kupata masomo nchini Marekani mwaka 1960 ambapo mamia zaidi walifuatia mwaka 1961.
Tom Mboya alijengea marafiki wengi na hata ilionekana ‘Mtandao’ wake ni mkubwa na uliwatisha wanasiasa wengi. Alipendwa sana na vijana na akawa zaidi maarufu sana mbele ya umma hivyo kila kukicha alizidi kupewa nyadhifa za juu.
Ilipofika mwaka 1960, Mboya alikubali kuunganisha chama chake cha People's Congress Party na chama cha Kenya Independent Movement kisha kuunda Kenya African National Union (KANU) ambacho kilikuwa na taswira ya kitaifa. Yalikuwa ni maandalizi muhimu sana kushiriki katika mkutano wa Lancaster (Lancaster House in London) ambapo Kenya ilikubaliwa kupata uhuru wake. Mboya aliongoza ujumbe huo kama katibu mkuu wa KANU.
Baada ya uhuru wa Kenya mwaka 1963, Mboya alichaguliwa kuwa mbunge wa jimbo la kati Nairobi. Aliteuliwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria, na baadaye Waziri wa Uchumi, Mipango na Maendeleo.
Aliandika kazi mbalimbali ikiwemo "kikao Paper 10" on Harambee na Tennents of African Socialism. Zilichukuliwa kama kazi zilizoweka kanuni na taratibu za kiungozi katika maadili.
Tukio la Mauaji yake:
Ni katika Mtaa wa Independence Avenue (ambao sasa ni Moi Avenue), mchana wa saa 7, siku ya Jumamosi Julai 5, 1969 ambapo Mboya akitoka kwenye duka la dawa(Pharmacy) alipigwa risasi kadhaa na mtu ‘Asiyefahamika’ lakini baadae akajulikana kuwa ni Nashon Isaac Njenga Njoroge.
Wakati huo, Mboya alikuwa na umri wa miaka 39 tu, alifariki papo hapo. Shughuli zote zilisimama katika mji huo. Baada ya tukio hilo kuliibuka fujo mbalimbali katika maeneo ya nchi. Haikuwa rahisi kujua haraka ni nani aliyempiga risasi Tom Mboya ambaye alikuwa kipenzi cha watu. Scotland Yard(Majasusi toka Uingereza) walipelekwa Kenya ili kusaidia uchunguzi na kutoa matokeo juu ya aliyehusika hasa na mauaji hayo, iligundulika ni Nashon ambaye alikuwa ametorokea Japan. Alirudishwa na kushtakiwa.
Kuna nadharia nyingi ya sababu ya mauaji haya;
i. Inaelezwa ni chuki tu dhidi ya Tom Mboya, alionekana ni wazi kuwa atachukua madaraka baada ya Rais Jomo Kenyatta. Hii ingewanyima nafasi wengine waliokuwa wanainyemelea.
ii. Kuna wanaohusisha misimamo yake ya kijamaa na kifo chake, wakati viongozi wengi wakiupinga mfumo huo yeye alitaka ‘Ujamaa’ ndio uwe dira ya chama cha KANU hata mara kadhaa kuliibuka mijadala mikali ya ndani.
iii. Kuna nadharia inayohusisha serikali ya wakati huo na kifo cha Mboya, Hii ni nadharia iliyodhihirika Raisi Jomo Kenyatta alipohudhuria mazishi ya Mboya huko Kisumu. Watu wengi walifanya vurugu na kubwa na kusababisha majeruhi wakiamini kuwa walikuwa serikali Kenyatta ilihusika katika kifo hicho. Tom Mboya lionekana ni kama ni tishio kwa serikali iliyopo madarakani.
Lakini pia Baada ya kukamatwa kwake, Njoroge(Mhusika) alisikika akisema: �Kwa nini mnanisumbua na hamuendi kuuuliza Mabwana wakubwa? Hii ni kusema kuwa alitumwa na serikali.
Pamoja na hilo, Kuna taarifa iliyochapishwa gazeti la Time magazine siku ya tarehe 5 Desemba 1969 kuwa Njoroge alifariki tarehe 8 Novemba 1969 majira ya saa tisa usiku. Lakini hakuna taarifa zozote zilizokuwa zimetolewa mpaka gazeti hilo lilipofichua. Hakuna ripoti iliyowahi kutolewa hadharani juu ya kifo chake ingawa inaelezwa kuwa alihukumiwa kifo baada ya ushaidi kukamilika. Gazeti la Nchini Canada, linaloitwa Ottawa Citizen liliripoti kuwa Njoroge alilazimishwa kukubali kesi na ndio maana aliropoka kuwa waulizwe wakubwa.
Mwishoni; Kuna wanahistoria wanaamini Tom Mboya aliuliwa makusudi ili kuchonganisha serikali Kenyatta na wananchi hasa toka katika kabila la waluo(Wajaluo). Hili lilifanyika na maadui wa Kenya ambao walijua wazi wakimuua Mboya itachochea zaidi chuki ya ukabila kati ya Wagikuyu(Wakikuyu-Kabila kubwa zaidi alilotokea Jomo Kenyatta) na Waluo(Wajaluo). Hii ingesababisha Kenya isitawalike kama zilivyokuwa nchi nyingine zilizopata uhuru wakati huo.
Wakati anauawa, Tom Mboya, alikuwa ni Waziri wa Mipango ya Uchumi na Maendeleo. Pia alikuwa ni mmoja wa wanasiasa waliokuwa wanapewa nafasi kubwa ya kuja kuwa rais wa nchi hiyo baada ya Kenyatta.
Mboya aliacha mke anayeitwa Pamela na watoto watano. Walifunga ndoa mwaka 1962. Pamela alirithiwa na kaka wa marehemu Tom Mboya aitwaye Alphonce Okuku ambapo walipata mtoto mmoja aitwaye Tom Mboya Jr. Thomas Joseph Odhiambo Mboya ‘Tom Mboya’ alizikwa katika kaburi maalum kwenye Kisiwa cha Rusinga. Kaburi hilo lilijengwa mnamo mwaka 1970.